MASUNGA MASELE AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU Kada wa Chama Cha Mapinduzi Masele Masunga, amechukua fomu kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Segerea wilaya ya Ilala mkoa Dar es Salaam. Masunga Masele amekabidhiwa fomu hiyo Juni 30,2025 na Katibu CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yared ili aweze kupata ridhaa ya kuteuliwa aongoze wananchi wa Segerea. Akizungumza ccm Wilaya ya Ilala Masunga Masele amesema kuwa amepata msukumo kutoka kwa Wananchi wa Jimbo la Segerea kumtaka agombea kwa madai kuwa bado kuna mambo yanatakiwa kuongezewa nguvu ili kuwaletea maendeleo wananchi. Alisema kuna matatizo mbalimbali yanayoilikabili Jimbo hilo ikiwemo ukosefu wa ajira kwa Vijana,huduma za afya, Elimu na ubovu wa baadhi ya miundombinu ya barabara .