DKT. DOTO MASHAKA BITEKO ACHUKUA FOMU JIMBO LA BUKOMBE






Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea Ubunge katika Jimbo la Bukombe.


Dkt. Biteko amechukua fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Ndugu. Leonard Yesaya Mwakalukwa mapema leo Juni 29, 2025.


Zoezi la uchukuaji fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI