WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*
Majina ya vigogo hao watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) — *Mhe. Paul Makonda*, *Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima*, na *Mhe. Jumaa Aweso* — yameanza kutajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuteuliwa kuwa *Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania*, endapo mabadiliko ya uongozi yatahitajika baada ya uchaguzi mkuu.
Wananchi na wachambuzi wa siasa wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mabadiliko yoyote katika safu ya juu ya uongozi wa serikali. Majina haya yameibuliwa kutokana na rekodi zao za kiuongozi, weledi na umaarufu ndani ya chama na serikali.
*Paul Makonda*
Aliwahi kuwa *Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam* na baadaye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Anajulikana kwa kauli thabiti, utendaji wa haraka, na uwezo mkubwa wa kushawishi makundi ya vijana.
*Dkt. Dorothy Gwajima*
Ni *Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum*. Amewahi pia kushika Wizara ya Afya. Ana rekodi nzuri ya utumishi wa umma, na ni mtaalamu wa utawala wa afya kwa zaidi ya miaka 20.
*Jumaa Aweso*
Ni *Waziri wa Maji*, anayesifika kwa usimamizi wa miradi mikubwa ya maji vijijini na mijini. Amejipatia umaarufu kutokana na ukaribu wake na wananchi na uwezo wa kusimamia utekelezaji wa sera
Je ni yupi anafaa endapo ikitokea kama inavyosemekana* ?
*#Makonda2025 #DorothyGwajima #JumaaAweso #WaziriMkuu #Uchaguzi2025 #CCM #TanzaniaYaSasa #SamiaSuluhu*
Comments
Post a Comment