IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan, akichukua fomu ya kugombea ubunge kwa mara nyingine kutoka kwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni, Amos Richard, katika ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni.

Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Idd Azzan amechukua fomu ya kutia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam.


Akizungumza leo Juni 29, 2025 baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama ch Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Amos Richard katika Ofisi za CCM za Wilaya hiyo Azzan ameomba ridhaa Chama kimpitishe aweze kugombea nafasi hiyo.


Azzan ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, amesema alikuwa kimya Kwa muda Mrefu kwa sababu Jimbo lilikuwa tayari na Mbunge lakini Kwa sasa baada ya Miaka mitano sasa Jimbo liko wazi na Chama kimeweka Demokrasia ya kila mwenye nia kuchukua fomu.




Comments

Popular posts from this blog

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI