RC CHALAMILA:SHULE ZIPO TAYARI KUPOKEA WANAFUNZI 2026 ‎



‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

‎MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wanafunzi wote waliopangiwa kuanza kidato cha kwanza kuwa tayari kuanza masomo ifikapo Januari mosi, 2026.

‎Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Chalamila amesema maandalizi ya ufunguzi wa shule yamekamilika kwa asilimia kubwa, huku akisisitiza kuwa changamoto za miundombinu zilizokuwa zikijitokeza miaka ya nyuma zimeshapatiwa ufumbuzi.

‎Amesema mkoa unatarajia kupokea jumla ya wanafunzi 95,323 watakaoanza masomo ya sekondari, huku Serikali ikihakikisha kuwa miundombinu ya madarasa na samani (madawati) inakidhi idadi hiyo bila kuwepo kwa vikwazo.

‎"Dar es Salaam tuko tayari. Maandalizi yote yamekamilika na hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi au kusoma katika mazingira magumu. Tunatarajia kupokea wanafunzi zaidi ya 95,000 na kila mmoja atapata haki yake ya elimu kama ilivyopangwa," alisema Chalamila.

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI