Posts

Showing posts from March, 2026

UBORESHAJI WA HUDUMA ZA WATEJA: MBUNGE BAGAMOYO AKABIDHI MAGARI KWA TANESCO

Image
Lengo ni kupunguza muda wa kushughulikia hitilafu na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wateja* Asema TANESCO imeimarika, imetoka katika kutengeneza hasara* 📍Bagamoyo, Pwani Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. Subira Mgalu leo Machi 03, 2026 amekabidhi magari mapya kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa lengo la kuimarisha huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika kuwahudumia Wateja wilayani Bagamoyo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ofisi ya TANESCO Bagamoyo, Mhe. Mgalu amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kwa wakati, kwa ubora na kwa uhakika zaidi. “Magari haya yatawezesha mafundi na wahandisi wa TANESCO kuwafikia wananchi kwa haraka pale panapotokea hitilafu au changamoto za umeme. Tunataka kuona muda wa kushughulikia matatizo unapungua na huduma inaboreshwa,” amesema Mhe. Mgalu. Amesisitiza kuwa, hivi sasa TANESCO imeimarika katika utoaji ...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SALOME MAKAMBA AKUTANA NA MKURUGENZI WA Go PLANT EMMANUEL LIKIDA KWA LENGO LA KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MAANDALIZO YA MIJADALA

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amekutana na Mkurugenzi wa Go Plant Tanzania Bw. Emmanuel Likida kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana katika maandalizi ya Mjadala (Debate) wa Clean Cooking Solutions utakaowahusisha wanafunzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma.  Katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadili umuhimu wa kuwajengea vijana uelewa wa mapema kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, athari za matumizi ya nishati zisizo safi kwa afya na mazingira, pamoja na fursa zilizopo katika ubunifu na ujasiriamali wa suluhisho za upishi safi. Mjadala huo unatarajiwa kuwa jukwaa la kielimu na kimkakati la kukuza uelewa, kuchochea fikra bunifu, na kuibua mabalozi vijana wa Nishati Safi katika jamii. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 03,2026 katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

GEN'Z WAJIFUNZE AMANI ILIVYOSAIDIA USTAWI NA MAENDELEO YA NCHI- MANG'ATI

Image
  Vijana wa Kata ya Pugu, Wilayani Ilala Mkoani Dar Es Salaam wamehimizwa kusoma na kuijua Historia ya Tanzania na hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa nchini, msingi ukitajwa kuwa amani, utulivu na usalama unaoshuhudiwa kote nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Frank Mang'ati, Diwani wa Kata ya Pugu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa maendeleo na ustawi wa wananchi, akibainisha pia wajibu wake mkubwa katika kuhakikisha amani inaendelea kutawala katika eneo lake la kiungozi. "Mimi kama kama Kiongozi nawajibika kuhakikisha amani inakuwepo Pugu na huwezi kuongoza vyema kama amani hiyo hakuna. Amani ndio tunu ya Taifa letu na tunapaswa kuijali na kuienzi kwani amani na Utanzania wetu ndio inayotuunganisha." Amesisitiza Mhe. Mang'ati. "Sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, tunao wajibu wa kuhakikisha nchi yetu inastawi na kushamiri katika amani. Wito wangu kwa Vijana almaarufu kama GenZ, Tujifunze tujue Taifa letu lilipotoka...

CRC YADAIWA BILIONI 4.7 NA TRA,MALI ZAKE ZIKISUBIRI KUPIGWA MNADA KUFIDIA DENI LA BENKI LA BILIONI 26.

Image
Na. Mwandishi wetu, Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA inaidai zaidi ya shilingi bilioni 4.7 kama malimbikizo ya kodi kampuni ya Continental Reliable Clearling (CRC), fedha ambazo kampuni hiyo imezichepusha kwa matumizi binafsi badala ya kulipa kodi ya Watanzania  Hii inaibuka ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kampuni hiyo ya CRC kugonga mwamba kuitumia Mahakama Kuu ya Tanzania kama kichaka cha kukwepa kulipa madeni, kwa mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya kampuni hiyo iliyoyapeleka dhidi ya benki za Equity Kenya na Tanzania na kuiagiza kampuni hiyo kulipa madeni waliyokopa na kuacha ujanja ujanja. Kufuatia uamuzi huo, tangazo la mnada wa mali za kampuni hiyo lililotolewa katika magazeti ya Mwananchi na The Citizen ya tarehe 19 mwezi wa pili kupitia kampuni ya udalali ya Adili Auction Mart Limited, lilithibitisha kuwa mali za CRC zinakwenda kuuzwa ili kufidia deni la benki linalofikia Shilingi bilioni 26. Hata hivyo, wakati harakati za mnada huo wa njia ya zabuni uliopangwa k...