RC CHALAMILA:MIILI KUANZA KUTOLEWA BILA MALIPO

 


Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

SERIKALI imesisitiza kuwa miili ya wagonjwa wanaofariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini, itatolewa bila malipo na kwa haraka ili kuwawezesha ndugu na jamaa kufanya taratibu za mazishi bila usumbufu.

‎Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa agizo hilo leo jijini hapa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maboresho ya huduma za jamii na usimamizi wa utu wa binadamu.

‎Chalamila amesema hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto zinazowakumba wananchi katika kipindi cha majonzi, hususan wale wanaokosa uwezo wa kugharamia huduma mbalimbali baada ya kufiwa na wapendwa wao.

‎"Lengo ni kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu wa ziada wanapokuwa katika kipindi kigumu cha kuondokewa na ndugu zao. Mwili unapaswa kutolewa mara moja ili taratibu za mazishi ziendelee," amesema  Chalamila

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI