KAMPUNI PLATIUM CREDIT YATOA MKOPO WA GARI KWA WATANZANIA,RUHUZA AFUNGUKA.
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU
KATIKA kuhakikisha wanawainua kiuchumi watumishi wa Umma,wafanyabiashara na Wafanyakazi wa sekta binafsi,Kampuni ya utoaji mikopo ya Platinum credit limited imetanga huduma ya mikopo wa magari kwa riba nafuu.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Maendeleo ya Biashara,Allan Ruhuza wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 wameamua kuwawezesha watanzania kuweza kumiliki gari.
"Sisi Platinum Credit tutagharamia hadi asilimia 65 ya thamani ya Gari yako kwa vigezo rafiki huku mteja atatoa asilimia 35 atatoa mteja "Amesema Ruhuza,
Ruhuza ameitaja Mikopo hiyo iliyotamulishwa ni pamoja Logbook Finance Loan(Mikopo yakutumia kadi ya Gari),Civil servants loans(mkopo maalum kwa watumishi wa umma.) Na SMEs Loans(Mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wakati).
Hata hivyo,Ruhuza,amesema Mikopo hiyo imebuniwa kwa utaratibu rahisi,upatikanaji wa haraka na masharti rafiki kwa wateja.
"Kupitia juhudi hizi,Platinum Credit Tanzania inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuwa mshirika wa maendeleo kwa watanzania kwa kutoa suluhisho rahisi,Jumuishi na endelevu za kifedha zitakazochochea ustawi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla."

Comments
Post a Comment