DKT MWINYI AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI WA PEMBA NA UNGUJA KUWA NA UWIANIO SAWA WA MAENDELEO



Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

 Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wananchi wa Pemba kuwa Serikali itaendelea kuweka uwiano sawa katika miradi ya maendeleo kwa Unguja na Pemba. 

Akizungumza leo Septemba, 24 2025 na wafanyabiashara na wajasiriamali wa Soko la Chakechake wa Mkoa wa Kusini Pemba Dk. Mwinyi amesema miradi mbalimbali imekuwa ikitekeleza kwa usawa ikiwemo Sekta za miundombinu, elimu, afya na nyenginezo. 


Amesema Serikali itaendelea kulinda na kuimarisha soko la asili la Chakechake ili libakie na uasili wake huku ikipanga kujenga soko jipya la kisasa.


"Suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa Serikali ijayo itaongeza mara dufu fedha za uwezeshaji ili kuhakikisha kila mjasiriamali anapata mkopo bila kuachwa nyuma," amesema Dk. Mwinyi. 


Ameeleza kuwa Serikali itafanyia kazi kwa kina suala la msururu wa kodi na kuweka utaratibu wa kodi nafuu kwa wafanyabiashara.

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI