Posts

UKOSEFU WA AMANI HUSABABISHA UGUMU WA MAISHA- SONGORO

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Lucas Hamis Songoro, Mkazi wa Ilala Dar Es Salaam amesema Tanzania haikuwahi kuzoea maandamano, fujo na matukio ya uvunjifu wa amani, akitahadharisha athari za Machafuko na ukosefu wa amani kwa maendeleo na ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla. "Ni vizuri tukatulia, tukapambana na maisha yetu kwasababu maandamano ya Oktoba 29, 2025 yalitukosesha amani na maisha yakawa magumu hasa katika utafutaji kutokana na kushinda tu nyumbani, kiufupi ni kwamba maisha yalikuwa magumu sana." Amesema Songoro. Songoro anayejihusisha na biashara ya usafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda, amehimiza pia kutumia vyombo rasmi vya kudai haki na usimamizi wa haki zao ikiwemo Wizara mpya ya Maendeleo ya Vijana iliyoundwa, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ya maridhiano na kusema suala hilo litumike vyema kupata suluhu ya changamoto zinazowakabili wananchi hususani Vijana. Songoro anaungana na maelfu ya wananchi wengine w...

HATUA KUBWA ZA MAENDELEO ZIMEPIGWA, VIJANA WAPUNGUZE MIHEMKO- JAPHARI

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Amir Japhari, Fundi Magari anayefanya shughuli zake za ufundi Mkoani Dar Es Salaam, amesisitiza kuwa machafuko na matukio ya uvunjifu wa amani nchini hayawezi kuwa mbinu ya upatikanaji wa haki kwa baadhi ya watu, akihimiza kila Mtanzania kuilinda amani badala ya kukimbilia kufanya fujo zisizokuwa na faida yoyote. Japhari akizungumza na Chombo chetu cha habari mapema leo Jumanne Novemba 25, 2025, amemshukuru Rais Samia pia kwa kusikia kilio cha Vijana na kuunda wizara ya maendeleo ya Vijana pamoja na kuteua Mawaziri wengi Vijana, akiamini kuwa Viongozi hao wanafahamu na wana uwezo mkubwa wa kushughulikia changamoto za Vijana nchini. "Amani ni kitu muhimu sana katika Taifa hili, Vijana wengi wanafikiri Taifa hakuna linachowafanyia lakini ukiangalia kuna Mataifa mengi yameingia kwenye machafuko wakiamini kuwa ndio chanzo cha kupata haki zao leo wamefika sehemu wanatamani amani na imekuwa ngumu kuirejesha. ... Leo ukiangalia katika nchi yetu, tulipotoka n...

KILICHOTOKEA OKTOBA 29 NI UHALIFU NA UHARAMIA- DKT. MSENGI

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Mkuu wa Mkoa mstaafu Dkt. Ibrahim Msengi kwaniaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam ameeleza kusikitishwa na uvunjifu wa amani uliotokea siku na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiwataka wale wanaodai haki kutekeleza wajibu wao kwanza, huku pia akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya uchunguzi kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025. Dkt. Msengi amebainisha hayo leo Jumatatu Novemba 24, 2025 Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mkoani humo akisema kilichotokea siku hiyi haikuwa maandamano bali ni uhalifu ulioandamana na ugaidi na kila aina ya uharamia nchini. "Nishukuru kuwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ameshaunda Tume ambayo tunaiamini na ninaamini italeta majibu mazuri na hatua zitachukuliwa. Suala la usalama kwenye Ilani yetu ni suala la msingi na kama hakuna amani na usalama hakuna maendeleo." "Lakini nikumbushe tu kwamba katika mamb...

NAIBU WAZIRI MAKAMBA ASISITIZA UWEPO WA MAGHALA YA KUHIFADHIA MAFUTA NCHINI.

Image
📌ataka kuwepo njia ya haraka ya usafirishaji wa Mafuta  📌asisitiza uwezekano wa kupunguza gharama za ununuzi wa vifaa vya mifumo ya umeme majumbani (wiring) 📌asisitiza uwepo wa Fursa kwa makundi ya Vijana ili kuwajengea uwezo. Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati Mhe. Salome Makamba ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuimarisha njia bora na ya haraka ya usafirishaji wa Mafuta nchini ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa mafuta. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Makamba alipofanya kikao kazi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Jijini Dodoma. Mhe. Makamba amesisitiza uwepo wa maghala ya kutosha ya kuhifadhia mafuta Nchini ili Wananchi waepukane na changamoto ya ukosefu wa Mafuta na kupongeza jitihada za kukabiliana na changamoto hii ambayo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuidhibiti. Sambamba na hilo Mhe. Makamba ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuangalia namna bora ya...

WAZIRI KAPINGA AIPONGEZA TUME YA USHINDANI (FCC) KWA KAZI YA KUDHIBITI BIASHARA NA KULINDA WALAJI ‎

Image
‎Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM JAMII HURU  ‎ Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amekiri juhudi kubwa zinazofanywa na Tume ya Ushindani (FCC) katika kudhibiti masoko, kulinda walaji, na kuhakikisha bidhaa feki hazingii sokoni. Waziri Kapinga alitoa pongezi hizo leo alipotembelea ofisi za FCC zilizopo jijini Dar es Salaam, akielezea namna tume hiyo inavyofanya kazi muhimu katika kuimarisha ushindani na ufanisi katika sekta ya biashara. ‎ ‎Akizungumza kwenye kikao hicho, Waziri Kapinga alisema kuwa moja ya majukumu makubwa ya FCC ni kuhakikisha kwamba usimamizi wa biashara unakuwa imara, na kwamba ni lazima kuhakikisha bidhaa zinazozunguka katika soko ni bora, salama na zinazokidhi viwango vinavyohitajika. Aliongeza kuwa tume hiyo pia inatoa elimu kwa watanzania kuhusu haki zao kama walaji na jinsi ya kutambua bidhaa feki. ‎ ‎“Watanzania wanatufahamu vizuri, na wao ndio walaji wetu. Kwa hiyo, tunapoongea kuhusu masuala ya biashara, tunapaswa kufikiria namna ya kutimiza ...

DAR CITY YAFUNZU MICHUANO YA MPIRA YA KIKAPU KUCHEZA FAINALI

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU   Timu ya mpira wa Kikapu ya Dar City leo imeandika historia mpya baada ya kufanikiwa kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufuzu kucheza fainali za BAL 2026 (Basketball African League). Dar City wamefuzu hatua hiyo baada ya ushindi wa vikapu 92-77 dhidi ya Club Ferroviario ya Msumbiji, Dar City wamemaliza nafasi ya tatu katika hatua ya Elite 16.

SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA USALAMA DISEMBA 9 UTAKUWEPO - GERSON MSIGWA

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msemaji wake mkuu Gerson Msigwa imesema kuwa inatambua uwepo wa fununu kuhusu Maandamano yanayotajwa kufanyika Disemba 9.2025  Msigwa amesema hayo leo Novemba 23.2025 Jijini Dar es salaam alipokuwa katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari  Aidha amesisitiza kuwa Serikali imejapanga kama ilivyokawaida siku zote kuhakikisha siku hiyo pia usalama utakuwepo pia endapo vitatokea viashiria vya Vurugu mbalimbali ipo kuwalinda Watanzania na mali zao