UKOSEFU WA AMANI HUSABABISHA UGUMU WA MAISHA- SONGORO




Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

Lucas Hamis Songoro, Mkazi wa Ilala Dar Es Salaam amesema Tanzania haikuwahi kuzoea maandamano, fujo na matukio ya uvunjifu wa amani, akitahadharisha athari za Machafuko na ukosefu wa amani kwa maendeleo na ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.


"Ni vizuri tukatulia, tukapambana na maisha yetu kwasababu maandamano ya Oktoba 29, 2025 yalitukosesha amani na maisha yakawa magumu hasa katika utafutaji kutokana na kushinda tu nyumbani, kiufupi ni kwamba maisha yalikuwa magumu sana." Amesema Songoro.


Songoro anayejihusisha na biashara ya usafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda, amehimiza pia kutumia vyombo rasmi vya kudai haki na usimamizi wa haki zao ikiwemo Wizara mpya ya Maendeleo ya Vijana iliyoundwa, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ya maridhiano na kusema suala hilo litumike vyema kupata suluhu ya changamoto zinazowakabili wananchi hususani Vijana.


Songoro anaungana na maelfu ya wananchi wengine wanaolaani matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakihimiza amani kama jambo muhimu zaidi na kusema pasipo amani haki haiwezi kupatikana kwa wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI