WACHIMBAJI WADOGO DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA, AFYA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MIGODINI
_Mafunzo yanalenga kukuza uchimbaji salama, endelevu na wenye tija katika sekta ya madini ya shaba_ *Dodoma, Juni 27 2025* Wachimbaji wadogo kutoka migodi ya shaba iliyopo katika Mkoa wa Dodoma wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu usalama mahali pa kazi, afya, utunzaji wa mazingira na usimamizi wa shughuli za uchimbaji. Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uchimbaji salama na endelevu nchini. Mafunzo hayo yamewahusisha wachimbaji kutoka Mgodi wa Shengde uliopo Nala, Mgodi wa Hussein Pilly uliopo Tambi (Wilaya ya Mpwapwa) na Mgodi wa Canada uliopo Chamkoroma (Wilaya ya Kongwa) ambapo yamewezeshwa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Tume ya Madini. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhandisi Chacha Megewa kutoka Tume ya Madini ameeleza kuwa ni muhimu kwa wachimbaji kufanya kazi katika mazingira salama kwa kutumia vifaa kinga kama kofia ngumu, reflekta, buti, gloves na barakoa (maski). "Ulipuaji wa baruti ni mojawapo ya shughuli...