TWCC YAWATAKA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO KUWA NA KAULI NJEMA KWA WATEJA WAO

 


Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM JAMII HURU 

Twcc imeweza kuwapa Mafunzo wajasiriamali mbalimbali na kuwataka pindi wapo Katika biashara zao kuweza kuwazingatia wateja wao hata mteja wanapoulizia biashara kwa kebehi wawe na majibu mazuri ya kuwajibu.


Ameyasema hayo Leo Tarehe 27 Juni 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Twcc Dr Mwajuma Hamza Ambapo Leo wametoa wafunzo hayo kwa washiriki wajasiriamali wadogo wadogo ambao wanaenda kushiriki katika maonesho ya 49 ya sabasaba ambayo yanayofanyika Katika viwanja vya sabasaba yanatarajiwa kuanza kesho Tarehe 28 na kutarajia kufanyika Kwa siku 16 


Amesema Lengo la maonesho hayo ni kuwa wanapofika Katika maonesho wanatakiwa wabedhi sana Katika kuuza biashara zao Ili kupata mafanikio,"na kusema kuwa siku 16 ni nyingi na wanaporudi mtaani wawe wameshapata wateja wapya,Oda na kupata Fursa mbalimbali.


"Kila mwaka huwa tunaandaa Mafunzo haya Kwa makusudi kabisa kuwapa Mafunzo na kuhakikisha wanapata elimu na kujua vitu Gani vinatakiwa upange navyo unapoenda kushiriki maonesho kama sabasaba au maonesho mengine yoyote"Amesema Hamza 


Ameongeza kuwa usijivune kufanya maonesho mengi Kwa mwaka alafu hauna matokeo tunatamani sana kama ukishiriki maonesho Ili mwakani uchukue Banda lako mwenyewe sio kila Siku ushiriki Katika Banda la Twcc 


Pia Hamza amewasisitizia wajasiriamali wadogo kuweza kusajili biashara zao katika taasisi ya brela Ili kuweza kuingia Katika masoko ya ushindani na brand ziweze kukua 


Nae mfanyabiashara mdogo wa bidhaa za asali Rina vise Amesema wamepata uelewa wa jinsi ya kuzungumza na wateja na jinsi ya kutafuta masoko 


"kunasehemu nilikuwa sielewi vizuri namna Gani ya kupalangana kama mwanamke na ujasiri umepelekea kusimama popote na kujiamini"Amesema Vise


Aidha Amebainisha kuwa Lengo ni kujitangaza Zaidi na kupata field back Kwa kile ambacho amekifanya Katika maonesho ya sabasaba












Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI