TAMWA YALAANI UDHALILISHAJI WA WANAWAKE WANASIASA MITANDAONI




Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM JAMII HURU 

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimelaani vikali mashambulizi ya kijinsia yanayowakumba wanawake wanasiasa katika mitandao ya kijamii, kikieleza kuwa ni kikwazo kikubwa kwa jitihada za kuendeleza usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.



Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa mwaka (AGM) wa chama hicho, muasisi wa TAMWA, Halima Sharifu, amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali za kijinsia, bado ushiriki mdogo wa wanawake katika siasa ni changamoto kubwa inayoathiri ustawi wa taifa.



Sharifu ameongeza kuwa mitandao ya kijamii, licha ya kufungua fursa kwa wanawake kushiriki mijadala ya kisiasa na kujitangaza, imegeuka kuwa jukwaa la mashambulizi ya kisaikolojia na lugha za matusi, dhihaka, na kejeli zenye misingi ya kijinsia.



TAMWA imeeleza kusikitishwa na ongezeko la vitendo hivyo vinavyoathiri motisha ya wanawake kushiriki siasa, huku ikisisitiza kuwa jamii inapaswa kushirikiana kuwalinda wanawake dhidi ya unyanyasaji wa aina hiyo.



Pamoja na changamoto hizi, TAMWA imesema inajivunia hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa kwanza mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi wa wanawake wenye uwezo katika nafasi za juu za uongozi umetajwa kama mfano wa kuigwa.



Naye Mkurugenzi mkuu WA TAMWA DKT Rose Reuben amesema Kwa takribani miongo Minne,Tamwa imekuwa Chombo Muhimu katika kupaza Sauti dhidi ya ukatili WA kijinsia,kuhamasisha uundwaji WA sera na Sheria Zenye mlengo WA usawa WA kijinsia,na kuwajengea uwezo na kuwezesha maelfu ya wanahabari kufahamu Kwa kina masuala ya usawa WA kijinsia Pamoja na wanawake katika siasa na uongozi.
















Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI