Posts

WAZIRI NYANSAHO APONGEZA JKT NA JWTZ KWA KUIMARISHA ULINZI, ASEMA VINACHANGIA AJIRA NA MAENDELEO

Image
‎ ‎Na Madina Mohamed  ‎ ‎Dar es Salaam – Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amevipongeza viongozi na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa juhudi wanazozifanya katika kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi. ‎ ‎Dkt. Nyansaho ametoa pongezi hizo Julai 6, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), akisema utendaji wa vyombo hivyo umeendelea kuwa msingi wa kudumisha amani na utulivu unaowapa wananchi fursa ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. ‎ ‎Amesema mazingira ya amani na usalama yanayolindwa na JKT na JWTZ yana mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kwani wananchi wanaendelea kufanya shughuli za kiuchumi bila hofu. ‎ ‎Waziri huyo alieleza kuwa mbali na jukumu la ulinzi, JKT imeendelea kutekeleza shughuli za uzalishaji mali pamoja na kutoa mafunzo kwa v...

MADIWANI WA MPANDA NA NSIMBO WAIPONGEZA SERIKALI KWA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA JULIUS NYERERE

Image
Na Mwandishi wetu, Rufiji - Pwani Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Mpanda na Nsimbo mkoani Katavi, wakiongozana na baadhi ya wabunge na viongozi wengine, wamepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Kituo cha Kufua Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kujionea kwa karibu uendeshaji wa kituo hicho na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya nishati nchini. Viongozi hao walitembelea kituo hicho tarehe 20 Juni 2026 kwa lengo la kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali, kufahamu namna kituo kinavyoendeshwa pamoja na kupata uelewa wa mchango wake katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini. Ziara hiyo ilihusisha madiwani 22 pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Katavi. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda, Charles Philipo, aliishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazoendelea kufanya katika kuimarisha sekta ya nishati na kuipongeza TANESCO kwa kuwapatia viongozi hao fursa ya kujionea kituo hicho. “Tunais...

WANANCHI MSIHOFU KUTUMIA NISHATI YA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI -MD TWANGE

Image
Na Mwandishi wetu  📌Asema TANESCO inajenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima 📌Aeleza mpango wa kusambaza majiko sanifu ya umeme takribani Mil 1 📌Awapongeza Wafanyakazi kwa ubunifu na jitihada za kuwahudumia wateja kwa ufanisi. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, amewaondoa hofu wananchi kuhusu matumizi ya nishati ya umeme katika vyombo vya usafiri, akisema kuwa TANESCO imejipanga kujenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima. Mkurugenzi huyo amesema hayo Juni 19, 2026, alipotembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali, mkoani Dodoma. Amesema shirika linatambua kuwa mahitaji ya umeme yanaendelea kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi, hivyo jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kwa ubora na uhakika kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. “TANESCO inafanya kazi kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati s...

MSUVA AUNGA MKONO MPANGO WA MAFUNZO WA JAB KUELEKEA AFCON 2027

Image
Na Mwandishi Wetu Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simon Msuva, amepongeza mpango wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) wa kuandaa mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), akisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha mchango wa sekta ya habari katika kuitangaza Tanzania, kukuza vipaji vya wanamichezo na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo zitakazotokana na mashindano hayo. Msuva ametoa pongezi hizo leo, tarehe 19 Juni 2026, alipotembelea Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari zilizopo Posta Mpya, Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula. Amesema Waandishi wa Habari wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo nchini kwa kutangaza vipaji vya wanamichezo, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi. “Mimi nawaombea waweze kutengeneza elimu ...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

MAJIBU YA TANESCO KUHUSU CHANGAMOTO ZA WATEJA ZILIZOWASILISHWA KUPITIA JUKWAA LA JAMII FORUMS

Image

UBORESHAJI WA HUDUMA ZA WATEJA: MBUNGE BAGAMOYO AKABIDHI MAGARI KWA TANESCO

Image
Lengo ni kupunguza muda wa kushughulikia hitilafu na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wateja* Asema TANESCO imeimarika, imetoka katika kutengeneza hasara* 📍Bagamoyo, Pwani Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. Subira Mgalu leo Machi 03, 2026 amekabidhi magari mapya kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa lengo la kuimarisha huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika kuwahudumia Wateja wilayani Bagamoyo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ofisi ya TANESCO Bagamoyo, Mhe. Mgalu amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kwa wakati, kwa ubora na kwa uhakika zaidi. “Magari haya yatawezesha mafundi na wahandisi wa TANESCO kuwafikia wananchi kwa haraka pale panapotokea hitilafu au changamoto za umeme. Tunataka kuona muda wa kushughulikia matatizo unapungua na huduma inaboreshwa,” amesema Mhe. Mgalu. Amesisitiza kuwa, hivi sasa TANESCO imeimarika katika utoaji ...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SALOME MAKAMBA AKUTANA NA MKURUGENZI WA Go PLANT EMMANUEL LIKIDA KWA LENGO LA KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MAANDALIZO YA MIJADALA

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amekutana na Mkurugenzi wa Go Plant Tanzania Bw. Emmanuel Likida kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana katika maandalizi ya Mjadala (Debate) wa Clean Cooking Solutions utakaowahusisha wanafunzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma.  Katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadili umuhimu wa kuwajengea vijana uelewa wa mapema kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, athari za matumizi ya nishati zisizo safi kwa afya na mazingira, pamoja na fursa zilizopo katika ubunifu na ujasiriamali wa suluhisho za upishi safi. Mjadala huo unatarajiwa kuwa jukwaa la kielimu na kimkakati la kukuza uelewa, kuchochea fikra bunifu, na kuibua mabalozi vijana wa Nishati Safi katika jamii. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 03,2026 katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.

GEN'Z WAJIFUNZE AMANI ILIVYOSAIDIA USTAWI NA MAENDELEO YA NCHI- MANG'ATI

Image
  Vijana wa Kata ya Pugu, Wilayani Ilala Mkoani Dar Es Salaam wamehimizwa kusoma na kuijua Historia ya Tanzania na hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa nchini, msingi ukitajwa kuwa amani, utulivu na usalama unaoshuhudiwa kote nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Frank Mang'ati, Diwani wa Kata ya Pugu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa maendeleo na ustawi wa wananchi, akibainisha pia wajibu wake mkubwa katika kuhakikisha amani inaendelea kutawala katika eneo lake la kiungozi. "Mimi kama kama Kiongozi nawajibika kuhakikisha amani inakuwepo Pugu na huwezi kuongoza vyema kama amani hiyo hakuna. Amani ndio tunu ya Taifa letu na tunapaswa kuijali na kuienzi kwani amani na Utanzania wetu ndio inayotuunganisha." Amesisitiza Mhe. Mang'ati. "Sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, tunao wajibu wa kuhakikisha nchi yetu inastawi na kushamiri katika amani. Wito wangu kwa Vijana almaarufu kama GenZ, Tujifunze tujue Taifa letu lilipotoka...

CRC YADAIWA BILIONI 4.7 NA TRA,MALI ZAKE ZIKISUBIRI KUPIGWA MNADA KUFIDIA DENI LA BENKI LA BILIONI 26.

Image
Na. Mwandishi wetu, Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA inaidai zaidi ya shilingi bilioni 4.7 kama malimbikizo ya kodi kampuni ya Continental Reliable Clearling (CRC), fedha ambazo kampuni hiyo imezichepusha kwa matumizi binafsi badala ya kulipa kodi ya Watanzania  Hii inaibuka ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kampuni hiyo ya CRC kugonga mwamba kuitumia Mahakama Kuu ya Tanzania kama kichaka cha kukwepa kulipa madeni, kwa mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya kampuni hiyo iliyoyapeleka dhidi ya benki za Equity Kenya na Tanzania na kuiagiza kampuni hiyo kulipa madeni waliyokopa na kuacha ujanja ujanja. Kufuatia uamuzi huo, tangazo la mnada wa mali za kampuni hiyo lililotolewa katika magazeti ya Mwananchi na The Citizen ya tarehe 19 mwezi wa pili kupitia kampuni ya udalali ya Adili Auction Mart Limited, lilithibitisha kuwa mali za CRC zinakwenda kuuzwa ili kufidia deni la benki linalofikia Shilingi bilioni 26. Hata hivyo, wakati harakati za mnada huo wa njia ya zabuni uliopangwa k...

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO LA MWENYEKITI WA CCM ALIYEKUTWA AMEKUFA

Image
Kupitia mitandao ya kijamii kunasambazwa picha mjongeo akionekana mtu mmoja mwanaume ambaye anajinasibu kuhusika katika tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Itumbi aitwaye Elia Richard Sambala, miaka 53, mkazi wa Itumbi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Ukweli ni kwamba, Februari 11,2026 saa 7 mchana katika Kijiji cha Itumbi, Elia Richard Sambala, alikutwa shambani kwake akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye makali kichwani na watu wasiojulikana na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa matibabu. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, kupitia Askari wa kuchunguza matukio ya mauaji, walianza msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kuhusiana na tukio hilo na ufuatiliaji zaidi kwa wengine waliohusika unaendelea. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa masilahi wa eneo la uchimbaji madini ya dhahabu ambapo mmoja wa wanafamilia hao alikodisha kwa wawekezaji raia wa Chin...

JESHI LA POLISI KUENDELEA KUWEKA JITIHADA ZA KUNUNUA MBWA WAPYA WA KISASA WENYE UWEZO WA KUBAINI,KUZUIA NA KUMDHOOFISHA MHALIFU.

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuweka jitihada mbalimbali za kununua mbwa wapya wa kisasa na wenye uwezo ili kuboresha muonekano wa mbwa wa Polisi mwenye umbo lenye kumdhoofisha mhalifu. IGP Wambura, ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Kikosi cha Mbwa na farasi wa Mikoa na Wataalam Waongoza Mbwa na Farasi kikao kilichofanyika jijini Dar es salaam Februari 9,2026 huku akiweka msisitizo kwenye eneo la utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwatumia Wanyama kazi katika kudhibiti uhalifu kwenye maeneo yao. Akizungumza na Watendaji hao IGP Wambura, amebainisha kuwa, Kikosi hicho kina umuhimu mkubwa kiusalama kwa kuwa Doria za mipakani na maeneo mengine muhimu hulazimika kutumia mbwa na farasi kwani ni rahisi kupenya kwenye maeneo ambayo gari haliwezi kupita kwa urahisi. Amesema, Jeshi la Polisi lina Mbwa na Farasi wanaofanya kazi katika bandari, viwanja vya ndege na mipakani kwa lengo la kuzuia biashara...

UPENDO NA MAELEWANO VYATAJWA KUWA MSINGI WA AMANI NCHINI

Image
Adam Seleman, Mkazi wa Msongora Jijini Dar Es Salaam amesema tafsiri halisi ya amani ni pamoja na kuelewana na kupendana miongoni mwa Watanzania, akihimiza upendo na maelewano kama msingi wa kudumisha amani na utulivu nchini. Bw. Selemani amebainisha hayo leo Jumamosi Februari 07, 2026 wakati akizungumza na mwandishi wetu wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa ustawi na maendeleo, akisema familia, Jamii na Nchi yoyote inahitaji amani na utulivu ili kuweza kutimiza majukumu na wajibu walionao. "Maana halisi ya amani ni ile hali ya mtu kuwa na uhuru wa kufanya jambo ambalo linaruhusiwa Kikatiba na pia amani tafsiri yake ni upendo, tukipendana ndio amani yenyewe kuanzia ndani ya nyumba. Nawaomba sana tuendelee kushikamana na kudumisha hiki tulichonacho kwani sisi nchi yetu ni kisiwa cha amani." Amesema Bw. Selemani.

AMANI INATUPA UHURU WA KUJIENDELEZA KIUCHUMI- NIACHIENI

Image
Uwepo wa amani katika Taifa kumetajwa kama miongoni mwa rasilimali muhimu zinazohitajika ili kufanikisha malengo na mipango ya mtu mmoja mmoja, Familia, Jamii na Taifa kwa ujumla, Wito ukitolewa kwa Watanzania kuilinda na kudumisha amani. Kauli hiyo imetolewa na Bw. Ramadhan Mohamed Niachieni, Mkazi wa Mtaa wa Mkera, Kata ya Msongora Jijini Dar Es Salaam, akisisitiza kuwa amani ndiyo yenye kuleta maendeleo nchini hivyo kila mmoja anawajibika kuilinda kwa ustawi na maendeleo yetu binafsi. "Amani ina tija sana katika nchi yetu ikiwemo maendeleo ya kila hali kutokana na uhuru wa kufanya shughuli zetu za kiuchumi. Naomba sana tuilinde ili tusiharibikiwe kama wengine na ili tupate fursa ya kuijenga nchi yetu." Amesema Bw. Niachieni. Mwananchi huyo anaungana na maelfu ya wananchi wengine ambao wamekuwa wakisisitiza kuhusu ulinzi wa amani na kuwakataa wote wenye kuhatarisha amani nchini, wakirejea athari za kiuchumi na kijamii zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktob...

WITO WATOLEWA, JITIHADA ZA PAMOJA UDHIBITI WA SILAHA HARAMU NCHINI

Image
Kamati ya udhibiti na usimamizi wa silaha imetakiwa kujikita katika utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya silaha haramu ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya silaha haramu. Kauli hiyo imetolewa wakati wa ufungaji wa kikao cha kwanza cha mafunzo cha kamati ya udhibiti na usimamizi wa silaha, kilichofanyika kwa siku tatu Jijini Dar Es Salaam, wajumbe wakikubaliana kuwa ikiwa elimu itatolewa na jamii ikaelewa madhara ya kusambaa kwa silaha haramu, nchi itakuwa salama. Mapema akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, IGP Camillus Wambura amesema wajumbe wa kamati hiyo ni watu makini na wameonesha kuwa watakuwa msaada mkubwa katika kutekeleza majukumu yao kutokana na kuwa wabobezi katika nyanja tofauti kutoka Serikalini na sekta binafsi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini na Mrajisi Mkuu wa Silaha DCI Ramadhan Kingai alisema wataendelea kuchukua hatua kali kwa wamiliki wa silaha ambao wamekuwa wakikiuka taratibu z...

POLISI NJOMBE WAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI KUCHOMWA MOTO NA KUPORWA SILAHA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari limekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa katika Mitandao ya Kijamii nchini zikiambatana na picha mjongeo (Video), zikieleza uwepo wa Askari Polisi wa Mkoa huo aliyechomwa moto na kisha kuporwa silaha Mkoani humo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Banga, Januari 28, 2026 amesema kuwa katika Mkoa wa Njombe hakuna tukio kama hilo, akionya dhidi ya wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji. "Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla." Amesema Kamanda Banga. Polisi pia imesema inaendelea kumfuatilia mtu ama watu waliochukua na kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo a...

MWANACHAMA WA CHADEMA ARUSHA MATATANI KWA KUIBA 'FEDHA ZA LISSU'

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumkamata Bw. Fredrick Mbwambo, Mwanachama wa Chadema na Mkazi wa Arusha kwa tuhuma za wizi wa fedha ambazo alikuwa amezikusanya kutoka kwa wananchi waliokuwa wamechanga kwaajili ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu kupitia Kampeni yao ya "Funga mwaka na Tundu Lissu". Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo leo Jumatano Januari 28, 2026 Jijini Arusha mbele ya wanahabari, amesema ukamataji wa mtuhumiwa huyo umefanyika baada ya Polisi kupokea malalamiko kutoka kwa Bw. Alute Mughwai, aliyeeleza kubaini wizi wa fedha zilizokuwa zimechangwa. "Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishwa kwenye namba mbili za simu, moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ikiwa ni ya kampuni ya simu ya nchi jirani." Amesema Kamanda Masej...

RADA ZA HALI YA HEWA NI MUHIMU KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NCHINI.

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliandaa warsha ya mafunzo ya Rada za Hali ya Hewa na matumizi ya taarifa zinazotokana na Rada, tarehe 26-27 Januari 2026, Dodoma. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiufundi katika matumizi ya teknolojia Rada, hususan katika uchambuzi, tafsiri na matumizi ya taarifa ili kuboresha utoaji wa utabiri zikiwemo tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa wakati na kwa usahihi zaidi.           Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema “Kama mnavyofahamu, kwa sasa dunia inashuhudia ongezeko kubwa la matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotokana na kuchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, ikiwemo mvua kubwa, mafuriko, vipindi virefu vya ukame, pamoja na matukio ya vimbunga na upepo mkali. ...

RAIS SAMIA ANAAHIDI NA KUTEKELEZA "NI MFANO SAHIHI KWETU WASICHANA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa na Wanawake na Mabinti wa Kitanzania kama Kiongozi wa mfano na mwanamke mwenye athari chanya kiasi cha kutoweza kupimika kwa wanawake na mabinti wa Tanzania, Wakimsifu na kumpongeza kwa ujasiri na umahiri wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Kauli hiyo imebainishwa na Bi. Asina Sancho, Kijana na Mjasiriamali wa Kitanzania, akisema Rais Samia amewapa sababu mabinti wengi ya kuamini kuwa wanaweza kufikia malengo yao na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kupambania ndoto zao. "Mama Samia ametutia nguvu sisi mabinti kuamini kuwa tunaweza kusimama na kutimiza ndoto zetu, hata katika nyakati za majaribio, Mama Samia ametupa nguvu ya kuamini hakuna linaloshindikana. Katika imani pia Mhe. Rais amesemwa katika namna nyingi mbaya na bado amekuwa na imani na kuwasamehe waliomkosea licha ya wao waliomkosea kutotaka msamaha." Amesema Bi. Sancho...

NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES IWAFIKIE WATANZANIA WOTE - BALOZI KINGU

Image
*📌Uzalishaji wa Rafiki briquettes uende sambamba na uzalishaji wa majiko banifu* *📌STAMICO waahidi kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati safi nchini* 📍Kisarawe - Pwani Watanzania wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi ya kupikia (mkaa mbadala wa Rafiki briquettes) unaozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).  Rai hiyo imetolewa leo Januari 24, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Balozi Jacob Kingu akiwa ameambatana na Wajumbe wa REB na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walipotembelea kiwanda cha Nishati safi ya Rafiki Briquettes kinachomilikiwa na STAMICO kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani. Balozi Kingu amewataka STAMICO kuongeza kasi ya uzalishaji wa mkaa wa Rafiki briquettes ili watanzani wote nchini waweze kutumia nishati safi ya kupikia na salama.  “Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wa...