Posts

Showing posts from June, 2026

MADIWANI WA MPANDA NA NSIMBO WAIPONGEZA SERIKALI KWA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA JULIUS NYERERE

Image
Na Mwandishi wetu, Rufiji - Pwani Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Mpanda na Nsimbo mkoani Katavi, wakiongozana na baadhi ya wabunge na viongozi wengine, wamepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Kituo cha Kufua Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kujionea kwa karibu uendeshaji wa kituo hicho na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya nishati nchini. Viongozi hao walitembelea kituo hicho tarehe 20 Juni 2026 kwa lengo la kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali, kufahamu namna kituo kinavyoendeshwa pamoja na kupata uelewa wa mchango wake katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini. Ziara hiyo ilihusisha madiwani 22 pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Katavi. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda, Charles Philipo, aliishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazoendelea kufanya katika kuimarisha sekta ya nishati na kuipongeza TANESCO kwa kuwapatia viongozi hao fursa ya kujionea kituo hicho. “Tunais...

WANANCHI MSIHOFU KUTUMIA NISHATI YA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI -MD TWANGE

Image
Na Mwandishi wetu  📌Asema TANESCO inajenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima 📌Aeleza mpango wa kusambaza majiko sanifu ya umeme takribani Mil 1 📌Awapongeza Wafanyakazi kwa ubunifu na jitihada za kuwahudumia wateja kwa ufanisi. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, amewaondoa hofu wananchi kuhusu matumizi ya nishati ya umeme katika vyombo vya usafiri, akisema kuwa TANESCO imejipanga kujenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima. Mkurugenzi huyo amesema hayo Juni 19, 2026, alipotembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali, mkoani Dodoma. Amesema shirika linatambua kuwa mahitaji ya umeme yanaendelea kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi, hivyo jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kwa ubora na uhakika kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. “TANESCO inafanya kazi kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati s...

MSUVA AUNGA MKONO MPANGO WA MAFUNZO WA JAB KUELEKEA AFCON 2027

Image
Na Mwandishi Wetu Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simon Msuva, amepongeza mpango wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) wa kuandaa mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), akisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha mchango wa sekta ya habari katika kuitangaza Tanzania, kukuza vipaji vya wanamichezo na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo zitakazotokana na mashindano hayo. Msuva ametoa pongezi hizo leo, tarehe 19 Juni 2026, alipotembelea Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari zilizopo Posta Mpya, Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula. Amesema Waandishi wa Habari wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo nchini kwa kutangaza vipaji vya wanamichezo, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi. “Mimi nawaombea waweze kutengeneza elimu ...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

MAJIBU YA TANESCO KUHUSU CHANGAMOTO ZA WATEJA ZILIZOWASILISHWA KUPITIA JUKWAA LA JAMII FORUMS

Image