SERIKALI YASISITIZA KUJENGA MAZINGIRA YAFAAYO KWA WAFANYABIASHARA NA WALAJI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA AI-KATAMBI



‎Na Madina Mohammed 

‎Serikali imesema kuwa itahakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira wezeshi ya biashara, kupata faida, na kuchangia katika ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.

‎Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Patribas Katambi, alipomuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Judith Kapinga, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

‎Kauli mbiu ya mwaka huu, “Akili Mnemba (AI) katika Kudumisha Ushindani wa Haki na Kulinda Walaji”, inalingana na dhana ya kimataifa ya Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy, ikisisitiza kuwa teknolojia ya AI ni zana muhimu katika kudumisha ushindani wa haki, kulinda maslahi ya walaji, na kuongeza uwazi katika masoko.

‎“Serikali imejipanga kuwa daraja, si ukuta, kuhakikisha sera zinazolinda walaji na wafanyabiashara zinatekelezwa ipasavyo, hususan katika matumizi ya TEHAMA na AI,” alisema Mh. Katambai, akiweka mkazo katika uwekaji wa mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na walaji.

‎Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Hadija Ngasongwa, alisema maadhimisho yalianza kwa shughuli za kijamii, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao, umuhimu wa uwazi katika masoko, na namna ya kuepuka vitendo vinavyokandamiza ushindani.

‎Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT), Jaji Rose Ebrahim, amewataka wananchi na wafanyabiashara kutoa taarifa za vitendo viovu visivyo vya haki katika soko, huku Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani, Dkt. Aggrey Mlimuka, akisisitiza uhusiano kati ya AI na ulinzi wa walaji, akibainisha kuwa teknolojia inasaidia kuhakikisha uwazi na ufanisi katika biashara.



Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI