RAIS SAMIA HAJAPUUZA MANENO, USHAURI NA HISIA ZA WANANCHI- CHALAMILA



Na Mwandishi Wetu JAMII HURU 

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Albert John Chalamila amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa imara katika kuunda serikali, bila kupuuza maneno, ushauri na hisia za Watanzania.


Chalamila amebainisha hayo leo Jumanne Disemba 02, 2025 wakati Rais Samia Suluhu Hassan akikutana na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, akimpongeza pia kwa kuunda Wizara mpya ya maendeleo ya Vijana kwa kutambua kuwa Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa la Tanzania.


"Mhe. Rais sisi wana Dar Es Salaam tumekusikiliza siku ukiapishwa, tumesikiliza hotuba yako ya kwanza Bungeni, maelekezo yako yote tumeyatekeleza na tunaendelea kuyatekeleza kwa kuhakikisha tunafanyia kazi kwa kusikiliza makundi yote ya msingi, hisia zao, kwa kusikiliza matatizo yao ili tuyafanyie kazi na kuunda taifa lenye umoja." Amesema Chalamila.


Katika hatua nyingine, Mhe. Chalamila ameeleza kuwa Rais Samia kukutana na Wazee wa Dar Es Salaam ni faraja kubwa kwa watanzania kwa kutambua mchango wa Wazee katika maendeleo ya Tanzania, akiahidi kuchukua na kuyafanyia kazi yote yatakayoelekezwa na Rais Samia.






Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI