MBETO AWATAKA WAAFRIKA WALIOKO NJE KUTUMIA FURSA NA KUWEKEZA TANZANIA



Na Mwandishi wetu,zanzibar


Chama Cha Mapinduzi kimewashauri Watanzania wanaoishi Marekani katika Nchi za Falme za Kiarabu na Ulaya kufuata taratibu za kisheria ili kuwekeza miradi ya kiuchumi na Biashara Zanzibar


CCM kimeeleza tayari Serikali zake zimeandaa mazingira wezeshi yanayotoa nafasi kwa Watanzania na wageni wenye mitaji ya kuwekeza katika visiwa vya Pemba na Unguja. 


Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo alipotembelewa na raia toka Canada na Marekani wenye asili ya Afrika. 


Mbeto akizungumza na wageni hao ofisini kwake , alitoa wito kwa Watanzania walioko nje na ambao wameshapata uraia wa nchi nyingine,wajitahidi kuwekeza miradi katika Nchi zao za Asili.


Alisema kwa Watanzania waliopata uraia wa Mataifa mengine ,wenye mitaji na mipango ya kufanya biashara , wasione woga badala yake ,waje kuja kuwekeza Zanzibar ambako kuna miundombinu ya uhakika. 


"Watanzania na Waafrika waliopata Uraia Canada, Marekani,Falme za Kiarabu au Ulaya wawekeze Zanzibar .Waje Tanzania zipo fursa nyingi .Kuna umeme ,majisafi, barabara, Usafiri wa Anga na Majini kwa saa 24 " Alisema Mbeto.


Katibu huyo Mwenezi alieleza baada ya Waafrika wengi kuishi ughaibuni ,bila shaka sasa wamepata elimu ya kutosha, uzoefu na mbinu aidha za bisahara au za kuanzisha kampuni kubwa . 


"Kuna Waafrika wanaoishi ugenini kwa miaka mingi wakifanya kazi zilizowapatia fedha na Mitaji. Njia pekee waje kuwekeza Tanzania ambako kuna Amani na utulivu "Alisisitiza 


Hata hivyo raia hao wa kigeni wenye asili ya Afrika , wamemhakikishia Katibu Mwenezi huyo na kuahidi kufikisha ujumbe kwa wenzao na kuwataka wachangamkie fursa hizo .

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI