KAMA HUMPENDI SAMIA KUTOKANA NA DINI YAKE, SUBIRI AMALIZE MUDA WAKE- RAIS SAMIA
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU
"Mimi toka nimeingia madarakani matamko nane yametolewa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), lakini ukienda chini huko wenyewe wanapingana kwamba matamko yale hayafanyi vizuri kwasababu waliosimama kwenye mstari wa haki wanaona ile ni batili inayofanyika. Kwahiyo niseme kwamba Tanzania yetu ni nchi ya umoja, mshikamano, amani na utulivu na ndio ngao zetu, tusivurugwe ndugu zangu kupitia mirengo ya dini, siasa ama mirengo mingine yoyote ile hata kama aliyepo juu serikalini humtaki.
"Kuna muda, hii ni nchi ya demokrasia, huyo mtu ataongoza mpaka wakati huu, kafanya makosa semeni makosa yake. Kosa la serikali ya awamu ya sita ni kueneza huduma bora za afya kwa Watanzania? Kosa letu kueneza huduma bora za elimu mpaka kule Vijijini? Kosa letu kukuza uchumi wa Tanzania ukakua mpaka kusifiwa duniani?, Kosa letu ni kuifanya Tanzania kuwa salama na ikalike? Kosa letu ni nini?
Kama mtu hampendi anayeongoza tustahimili tu, mioyo yetu imeundwa na stahimili, demokrasia ipo, ataongoza ataondoka. Kama humpendi Samia hakuna sababu ya kuvuruga nchi, kama humpendi kwa alivyo, humpendi kwa dini yake, humpendi kwa alikotoka, hakuna sababu ya kuvuruga nchi, Katiba yetu, sheria zetu zipo hakuna sababu ya kuvuruga nchi.
Niwaombe sana zile sumu mnazopewa huko tumieni akili zenu. Najua hakuna eneo baya la kumpata mtu kama dini."- Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Dar Es salaam leo Jumanne Disemba 02, 2025.

Comments
Post a Comment