DKT. TULIA APIGA KURA UYOLE, AHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Ubunge Jimbo la Uyole kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Tulia Ackson, leo tarehe 29 Oktoba, 2025 amejitokeza kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Tambukareli mkoani Mbeya.
Dkt. Tulia ametoa wito kwa wananchi wa jimbo hilo na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua Viongozi wanaowataka.



.jpg)


Comments
Post a Comment