HEMED SULEIMAN ABDULLA: DK.MWINYI AMETEKELEZA MIRADI MUHIMU KWA MAENDELEO YA MKOANI PEMBA



‎Mgombea nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Kiwani kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hemed Suleiman Abdulla, amempongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa kazi kubwa na za kutukuka alizozifanya katika maeneo mbalimbali ya maendeleo, akisisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar wanapaswa kumshukuru na kumpigia kura kwa kishindo ifikapo Oktoba 29.

‎Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Makombeni, wilaya ya Mkoani, mkoa wa Kusini Pemba, Hemed alisema kuwa miradi mingi muhimu ya maendeleo imefanywa chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi, hususan katika wilaya ya Mkoani, ambapo alisema anaendelea kushuhudia mafanikio makubwa yanayotokana na uongozi huo.

‎"Mambo matatu ni muhimu ambayo ni lazima niyaeleze. Kila nikipita kwenye miradi hii, wananchi wananishukuru kwa kazi kubwa anayoifanya Dk. Mwinyi. Pia, wamekuwa wakimuombea dua na baadhi yao walikuwa wananiingiza salamu maalum za kumfikishia Dk. Mwinyi," alisema Hemed, akionyesha furaha na shukrani za wananchi kwa Rais Mwinyi.

‎Hemed alisisitiza kwamba, kazi za Rais Dk. Mwinyi zinaonyesha ni kiongozi mwenye maono ya kweli na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi. Alisema kuwa heshima inayotolewa kwa Dk. Mwinyi kutokana na kazi yake ni lazima iendelee kwa kumpigia kura za ndiyo kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

‎"Kwa heshima na imani waliyo nayo wananchi, ni muhimu kumtia moyo Rais wetu kwa kumchagua tena kwa wingi ili aendelee kutekeleza miradi hii ya maendeleo kwa manufaa ya vizazi vijavyo," aliongeza Hemed.

‎Kwa upande wake, wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo walionyesha kuridhika na miradi ya maendeleo inayoendelea chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi na walijitolea kutoa ahadi za kumuunga mkono kwa kura katika uchaguzi ujao.

Comments

Popular posts from this blog

IDD AZZAN AJA KIVINGINE TENA JIMBO LA KINONDONI

WANAOSEMEKANA KUWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*

DOLA MILIONI 2 ZA KIMAREKANI Kununufaisha WAKULIMA NCHINI