DK MWINYI MUKINIPA RIDHAA YA KUONGOZA TENA NITAWAWEZESHA MITAJI WAFANYABIASHARA
Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema endapo akipata ridhaa ya kuiongoza tena Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano atawawezesha mitaji wafanyabiashara.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Mwanakwerekwe lilopo wilaya ya Magharibi ‘B’ mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema serikali ya awamu ya nane imetoa sh.bilioni 96 kwa wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni mitaji ya biashara zao.
“Tunatambua kuwa wapo wafanyabiashara waliokuwa bado hawajapata mitaji hiyo lakini kipindi kijacho tunaongeza fungu hilo ili waweze kupata wengi zaidi,” amesema
Pia, Dk.amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo atajenga masoko mengi Zaidi ikiwemo soko la Kibanda maiti,Kisauni,Fuoni,Kwahaji Tumbo na Mwera ili wafanyabiashara waweze kufanyabiashara na kwamba ataendelea kumaliza changamoto zinazowakabili.










Comments
Post a Comment