WANUFAIKA WA BIMA WAFIKIA MILIONI 25.9 NCHINI – DKT SAQWARE
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU
IMELEZWA kwamba wanufaika wa huduma za Bima nchini wamefikia milioni 25.9 kutoka mil 14 kwa mwaka 2021, huku malengo yakiwa katika miaka 10 ijayo nusu ya watanzania wawe wanatumia huduma hiyo na asilimia 95 wawe na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa bima katika maisha yao.
Kamishna wa Mamlamka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt Baghayo Saqware, amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika kikao cha mpango kazi kulichoandaliwa na Msajili wa Hazina.
Ongezeko hilo la watumiaji wa huduma za bima limetokana na utoaji wa elimu kwa wananchi hali iliyofanya kutambua umuhimu wake katika maisha yao ya kila siku na linaloidia kukabiliana na majanga na maradhi.
Aidha ameongeza kuwa licha ya kuwepo kwa mafanikio hayo ambayo wanajivunia katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan, wanajipanga kuwashughulikia watoa huduma za afya wanaowapuuza wagonjwa wanaotumia bima na kutoa kipaumbele kwa wanaolipa ‘Cash’.
Amefafanua kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo ambayo imeendelea kujitokeza kwa baadhi ya wahudumu wa hospitali, wameanza kusajili hospitali zinazotoa huduma kwa wagonjwa wenye bima ya afya na kuingilia makubaliano nao ya kuhakikisha wanafaika wa bima wanahudumiwa vizuri na si kubaguliwa.
“Mchakato wa kuwasajili hospitali zinazopokea bima ya afya ukikamilika mhuduma yeyote wa hospitali atakayebainika amefanya kinyume na utaratibu tuliokubaliana na mgonjwa akaleta malalamiko hayo kwetu na tukathibisha, hospitali husika itaondolewa katika mpango huo na hatua nyingine kali zitachukuliwa,” amesema.
Akifafanua zaidi mafanikio ambayo yamepatika katika kipinbdi cha miaka minne ya Rais Dkt Samia, amesema kumekuwa na ongezeko la watoa huduma kutoka 993 mwaka 2021 na kufikia 2,425 wakiwermo watoa huduma mpya ikiwemo afya, kidigital na Bima Mtawanyo kutoka moja na kufikia nne.
Pia amesema katika kipindi hicho kampuni za bima zimeongezeka kutoka 32 mwaka 2021 na kufikia 35 na kutoa wito wito kwa wawekezaji katika sekta hiyo kujitokeza kwa wingi hasa wenye mitaji mikubwa ilki kuleta tija stahiki.
Ameongeza kuwa pia mali na mtaji katika soko la Bima imeongezeka kutoka sh. trillion 1.2 kwa mwaka 2021hadi kufikia trillion 2.3 hilo nalo ni jambo la kujivunia kama taasisi.
“Naamini wawekezaji wengi wanavutiwa kuja kuwekeza hapa nchini hususan wenye mitazji mikubwa kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri na utulivu inayohamisishwa na utungwaji wa sheria rafiki ya Bima ya Afya na kanuni zake,” amesema.
Dkt Saqware amesema katika kipindi hicho pia wamefanikiwa kuanzisha mifumo yua Tehama baada ya maelekezo ya Rais kutolewa ya kutaka taaisi za Serikali zisomane na tayari wameunganisha mifumo kadhaa ikiwemo Benki Kuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (LATRA), Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Ameongeza kuwa mataraji yao ni kuhakikisha mifumo inaunganishwa na taasisi zaidi ya 30 Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa lengo la kurahisisha huduma kwa wananchi popote walipo.
Pia amesema kwa sasa wanampango wa kuanzisha consortium ya kilimo ambayo ina kampuni 15 na consortium ya mafuta na gesi ambapo kuna umoja wa kampuni 22 zitakazoshiriki katika uchumi mafuta na gesi kama sekta.

Comments
Post a Comment