Posts

POLISI NJOMBE WAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI KUCHOMWA MOTO NA KUPORWA SILAHA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari limekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa katika Mitandao ya Kijamii nchini zikiambatana na picha mjongeo (Video), zikieleza uwepo wa Askari Polisi wa Mkoa huo aliyechomwa moto na kisha kuporwa silaha Mkoani humo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Banga, Januari 28, 2026 amesema kuwa katika Mkoa wa Njombe hakuna tukio kama hilo, akionya dhidi ya wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji. "Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla." Amesema Kamanda Banga. Polisi pia imesema inaendelea kumfuatilia mtu ama watu waliochukua na kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo a...

MWANACHAMA WA CHADEMA ARUSHA MATATANI KWA KUIBA 'FEDHA ZA LISSU'

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumkamata Bw. Fredrick Mbwambo, Mwanachama wa Chadema na Mkazi wa Arusha kwa tuhuma za wizi wa fedha ambazo alikuwa amezikusanya kutoka kwa wananchi waliokuwa wamechanga kwaajili ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu kupitia Kampeni yao ya "Funga mwaka na Tundu Lissu". Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo leo Jumatano Januari 28, 2026 Jijini Arusha mbele ya wanahabari, amesema ukamataji wa mtuhumiwa huyo umefanyika baada ya Polisi kupokea malalamiko kutoka kwa Bw. Alute Mughwai, aliyeeleza kubaini wizi wa fedha zilizokuwa zimechangwa. "Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishwa kwenye namba mbili za simu, moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ikiwa ni ya kampuni ya simu ya nchi jirani." Amesema Kamanda Masej...

RADA ZA HALI YA HEWA NI MUHIMU KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NCHINI.

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliandaa warsha ya mafunzo ya Rada za Hali ya Hewa na matumizi ya taarifa zinazotokana na Rada, tarehe 26-27 Januari 2026, Dodoma. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiufundi katika matumizi ya teknolojia Rada, hususan katika uchambuzi, tafsiri na matumizi ya taarifa ili kuboresha utoaji wa utabiri zikiwemo tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa wakati na kwa usahihi zaidi.           Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema “Kama mnavyofahamu, kwa sasa dunia inashuhudia ongezeko kubwa la matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotokana na kuchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, ikiwemo mvua kubwa, mafuriko, vipindi virefu vya ukame, pamoja na matukio ya vimbunga na upepo mkali. ...

RAIS SAMIA ANAAHIDI NA KUTEKELEZA "NI MFANO SAHIHI KWETU WASICHANA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa na Wanawake na Mabinti wa Kitanzania kama Kiongozi wa mfano na mwanamke mwenye athari chanya kiasi cha kutoweza kupimika kwa wanawake na mabinti wa Tanzania, Wakimsifu na kumpongeza kwa ujasiri na umahiri wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Kauli hiyo imebainishwa na Bi. Asina Sancho, Kijana na Mjasiriamali wa Kitanzania, akisema Rais Samia amewapa sababu mabinti wengi ya kuamini kuwa wanaweza kufikia malengo yao na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kupambania ndoto zao. "Mama Samia ametutia nguvu sisi mabinti kuamini kuwa tunaweza kusimama na kutimiza ndoto zetu, hata katika nyakati za majaribio, Mama Samia ametupa nguvu ya kuamini hakuna linaloshindikana. Katika imani pia Mhe. Rais amesemwa katika namna nyingi mbaya na bado amekuwa na imani na kuwasamehe waliomkosea licha ya wao waliomkosea kutotaka msamaha." Amesema Bi. Sancho...

NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES IWAFIKIE WATANZANIA WOTE - BALOZI KINGU

Image
*πŸ“ŒUzalishaji wa Rafiki briquettes uende sambamba na uzalishaji wa majiko banifu* *πŸ“ŒSTAMICO waahidi kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati safi nchini* πŸ“Kisarawe - Pwani Watanzania wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi ya kupikia (mkaa mbadala wa Rafiki briquettes) unaozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).  Rai hiyo imetolewa leo Januari 24, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Balozi Jacob Kingu akiwa ameambatana na Wajumbe wa REB na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walipotembelea kiwanda cha Nishati safi ya Rafiki Briquettes kinachomilikiwa na STAMICO kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani. Balozi Kingu amewataka STAMICO kuongeza kasi ya uzalishaji wa mkaa wa Rafiki briquettes ili watanzani wote nchini waweze kutumia nishati safi ya kupikia na salama.  “Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wa...

KANISA LA ACK WAIRIMA LASHAMBULIWA KWA MABOMU, GACHAGUA ANUSURIKA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Makabiliano makubwa yameshuhudiwa katika Kanisa la ACK Wairima, Kaunti ya Nyeri alikokuwa anahudhuria ibada ya leo Jumapili Januari 25, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya Mhe.Rigathi Gachagua Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, Polisi waliokuwa wamefunika nyuso zao wametupa mabomu ya kutoa machozi na kurusha risasi za moto katika kanisa hilo, watu kadhaa wakijeruhiwa huku Gagachua na ujumbe wake wakofanikiwa kutoroka. Hii si mara ya kwanza kwa Naibu huyo wa Rais wa zamani kushambuliwa kanisani ambapo Wiki mbili zilizopita shambulio kama hilo lilitokea nje ya kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) huko Kiamworia, Gatundu Kusini ambapo mafuriko yalitokea baada ya makundi hasimu ya vijana waliokuwa na virungu kuhusika katika vurugu nje ya Kanisa hilo. Kwenye chapisho lake kwenye Mtandao wa X Gagachua amedai kuwa yeye na washirika wake walinaswa ndani ya Kanisa hilo baada ya shambulio hilo kutokana na kile alichokiita Jaribio la m...

𝗠π—ͺπ—˜π—‘π—¬π—˜π—žπ—œπ—§π—œ π—žπ—”π—ͺπ—”π—œπ——π—”: π—‘π—œπ— π—£π—’π—‘π—šπ—˜π—­π—˜ π—₯π—”π—œπ—¦ π——π—žπ—§. π—¦π—”π— π—œπ—” π—žπ—¨π—˜π—‘π——π—˜π—Ÿπ—˜π—” π—žπ—¨π—Ÿπ—˜π—§π—” π— π—”π—˜π—‘π——π—˜π—Ÿπ—˜π—’

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta maendeleo hususani ahadi alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika siku 100 za kwanza za uongozi wake. Ndugu Kawaida akizungumza na maelfu ya wanafunzi wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu mkoani Dodoma leo tarehe 24 Januari 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete. Ametaja baadhi ya yaliyotekelezwa ikiwemo Bima ya Afya kwa wote na ajira kwa vijana zikiwemo za udaktari.