Posts

JAB YAONYA WAAJIRI KATIKA VYOMBO VYA HABARI KUZINGATIA SHERIA KUEPUKA MIGOGORO YA KISHERIA

Image
Na Mwandishi Wetu  Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewasisitiza waajiri kwenye vyombo vya habari nchini kuzingatia kikamilifu masharti ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, hususan wanapoajiri au kuwasainisha mikataba watumishi wa kada ya habari, ili kuepuka migogoro ya kisheria inayoweza kujitokeza baadaye. Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, tarehe 20-21 Januari, 2026 wakati wa ziara ya kikazi ya Bodi katika mikoa ya Dodoma na Iringa, ilipotembelea vyombo kadhaa vya habari kwa lengo la kukagua kiwango cha uzingatiaji wa Sheria hiyo kwa watumishi wanaojihusisha na shughuli za kihabari, wakiwemo wahariri, waandishi wa habari, watangazaji, wapiga picha waandaaji na waandishi wa kujitegemea. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Wakili Kipangula amesema Bodi imebaini uwepo wa waandishi wenye sifa stahiki kwa mujibu wa Sheria kwenye vyombo hivyo, lakini bado hawajajisajili katika Mfumo wa TAI-HABARI ili kuomba ithibati na vitam...

VIONGOZI WA CHADEMA MBEYA WASHIKILIWA WAKIHAMASISHA MIKUSANYIKO BATILI

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Mbeya Bw. Masaga Pius Kaloli na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mbeya Elisha Chonya kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya mikusanyiko isiyokuwa halali. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa Januari 21, 2026 saa tisa alasiri katika Kijiji na Kata ya Inyala baada ya Polisi kupata taarifa za uwepo wa Viongozi hao katika eneo hilo wakifanya maandalizi na wakiwahamasisha watu kukusanyika ili kufanya Mkutano bila bila kufuata taratibu za kisheria zilizopo. "Pamoja na kukiuka kwa makusudi taratibu hizo za kisheria, ikimbukwe kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimezuiliwa na Mahakama kufanya shughuli zozote za kisiasa." Amesema Kamanda Kuzaga. Taarifa hiyo ya Polisi Mkoa wa Mbeya imeendelea kueleza kuwa upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wat...

POLISI WAKANUSHA TAARIFA YA CHADEMA "HATUJAKAMATA MTU YEYOTE NKASI"

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa leo Jumatano Januari 21, 2026 limekanusha taarifa zisizo sahihi zilizosambazwa mitandaoni zikidai kuwa Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamevamiwa, kukamatwa na kutawanywa kwa nguvu na Jeshi la Polisi wakati wakipanda Miti Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa. Kupitia taarifa yake kwa Vyombo vya habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa amesema taarifa hizo za CHADEMA hazina ukweli wowote na zina lengo la kupotosha na kuzua taharuki zisizo na msingi kwani katika Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla hakuna tukio la matumizi ya mabavu ama la wafuasi wa Chama hicho kukamatwa na Jeshi la Polisi. "Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa linaendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao na tunaendelea kusisitiza wananchi kupuuza taarifa zinazoandaliwa na kusambazwa kwa lengo la kupotosha, kuchonganisha, kujenga chuki baina ya wananchi na Taasisi mbalimbali." Imesema taarifa hiyo ya Polisi. Jana kupitia Mitand...

MAKAMPUNI 300 KUUNGANISHWA NA MFUMO WA "IDRAS" TRA IMESEMA

Image
Na Magrethy Katengu MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema zaidi ya makampuni 300 yataunganishwa na mfumo wa mfumo wa kisasa wa usimamizi wa kodi za ndani ujulikanao kama “Integrated Domestic Revenue Administration System (IDRAS)” na kutatua kero mbalimbali za huduma za kikodi. Hayo yalielezwa jana na Kamishna wa Kodi za Ndani, Alfredy Mregi wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa walipakodi wa ndani yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) Dar es Salaam. Pia Kamishna huyo alisema kwamba kwakuanzia mnamo Februari 9, 2026 makampuni ama taasisi 60 zitaanza kuingizwa katika mfumo huo ambao unatajwa kurahisisha shughuli za kikodi baina ya TRA na wadau wa kodi za ndani hususani wafanya biashara wadogo wakati na wakubwa. “Niseme tu kwamba mfumo huu umekuja wakati muafaka kwa ajili ya kutatua kero na changamo za muda mrefu kwa wafanyabiashara wetu wa ndani hivyo utasaidia kupunguza gharama ambazo zilikuwa zikitumika kwa mlipa kodi kuja ofisini na w...

BANDARI ZETU ZINA UWEZO WA KUHUDUMIA MELI KUBWA NA ZA KISASA- MSIGWA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Serikali imeonesha kuridhishwa na ufanisi mkubwa pamoja na kurejea kuaminika kwa bandari ya Dar Es Salaam, akisema kwasasa Meli kubwa zimekuwa zikisimama katika bandari hiyo baada ya uwekezaji wa kuongeza Kina cha bandari hiyo, suala lenye kuwezesha Tanzania kuweza kupokea Meli zenye hadi ukubwa wa Mita 305. Kulingana na Msemaji Mkuu wa serikali Bw. Gerson Msigwa amesema mafanikio hayo makubwa yanatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na hivyo kuweza kupunguza gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara wenye mizigo mikubwa ama mingi, suala ambalo lililazimu hapo awali kusafirishwa kwa awamu kutokana na Bandari kukosa uwezo wa kuhudumia meli kubwa. "Nipo hapa na nyuma yangu mnaona kuna meli ya Galaxy S yenye uwezo wa kubeba magari zaidi ya 6,000 kuna nyingine pia hapa imeleta ngano ikiwa na uwezo wa kubeba tani 60,000 kwa wakati mmoja. Huko nyuma meli hizi zisingeweza kuja hapa kwani gati zetu zilikuwa fupi kuweza kuhimili ukubwa wa meli hizi." ...

MIZIGO YA TANI MILIONI 12 IMEPITISHWA BANDARINI KUHUDUMIA NCHI JIRANI KWA MWAKA 2024/25- MSIGWA

Image
Bandari za Tanzania zikiongozwa na Bandari kuu ya Dar Es Salaam zimetajwa kuendelea kuwa kiungo muhimu kwa kuhudumia baadhi ya Mataifa yenye kuizunguka Tanzania na yasiyokuwa na bandari, suala linalodhihirisha umuhimu na upekee wa Tanzania katika utoaji wa huduma za usafiri na usafirishaji kwa nchi hizo. Kulingana na Msemaji Mkuu wa serikali Bw. Gerson Msigwa, mbele ya waandishi wa habari leo Jumanne Januari 20, 2026 Jijini Dar Es Salaam amesema bandari hizo zimekuwa zikihudumia nchi za Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia na Uganda. "Pamoja na mizigo inayokuja kwaajili ya Tanzania, Bandari zetu zinahudumia nchi majirani ambapo kwa mwaka 2024/25, tuliihudumia DRC shehena ya mizigo ya tani 5, 995, 295, Tumehudumia Zambia shehena ya tani 3, 510, 706, Burundi tani 425, 774, Rwanda Tani 1,724, 370, Malawi shehena ya tani 675,000, Uganda 185, 625 na Zimbabwe tumewahudumia shehena ya tani 61,306." Amesisitiza Bw. Gerson Msigwa. Kulingana na Msigwa Banda...

UBIA WA DP WORLD NA ADANI GROUP WAKUZA PATO LA TAIFA NA UFANISI BANDARINI

Image
Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema uwekezaji katika bandari ya Dar Es Salaam kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wabia wa Kimataifa DP World na Adani Group umeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa shehena zinazohudumiwa Bandarini hapo kutokana na kuongezeka kwa ufanisi na kuaminika kwa bandari hiyo. Msigwa amebainisha hayo leo Jumanne Januari 20, 2026 wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Bandari hiyo na kuangazia uwekezaji uliofanywa chini ya serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. "Shehena zinazohudumiwa kwenye Bandari yetu ya Dar Es Salaam zimefikia tani Milioni 27. 7 kwa mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 17 kulinganisha na mwaka uliopita. Muda wa meli kuhudumiwa umepungua pia kutoka siku 30 au wakati mwingine 46 hadi kufikia siku 6." Amesema Msigwa. Aidha katika mwaka huu, Msemaji huyo wa serikali amebainisha kuwa kuanzia Julai hadi Disemba 2025, tayari Bandari ...