Posts

POLISI YAJIIMARISHA KULINDA RAIA MSIMU HUU WA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, (DCP) David Misime, amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wakati na baada ya sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, wito ukitolewa kwa kila mwananchi kutambua na kuheshimu thamani na umuhimu wa amani na usalama kwa kila mmoja. Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Disemba 22, 2025 na Jeshi la polisi imewataka pia wale wote watakaokuwa wakisafiri kutoka eneo moja kwenda jingine kuzingatia sheria za usalama barabarani kama sehemu ya kuepuka ajali za barabarani, wakikumbusha kuhusu kaulimbiu ya wiki ya nenda kwa usalama isemayo "endesha salama, familia inakusubiri." "Maisha yetu na shughuli zetu wakati wa hizi sikukuu yanahitaji mazingira ya amani ili kila mmoha aweze kushiriki kwenye ibada za kumshukuru Mungu, kukaa na familia na marafiki bila ya bugudha yeyote ile hivyo tuilinde amani kwa ushirikiano na kwa nguvu zetu zote." Imesema t...

SERIKALI KUJENGA MTAMBO WA KUCHENJUA DHAHABU MWAKITOLYO SHINYANGA

Image
■ Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan ▪️Zaidi ya tani 100 - 120 kuchenjuliwa kwa siku ■ Makundi ya vijana na wanawake kupatiwa leseni kupitia programu ya MBT ■ Leseni zisizoendelezwa kufutwa kwa mujibu wa sheria ■ Aelekeza Wachimbaji kufuata kanuni za usalama za uchimbaji kuepuka madhara *Mwakitolyo, Shinyanga* Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwasimamia wachimbaji wadogo, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ipo mbioni kuanza ujenzi wa mtambo wa kuchenjua madini ya dhahabu mkoani Shinyanga. Hayo yameelezwa leo tarehe 22 Desemba, 2025 na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde alipofanya ziara ya kikazi na kuzungumza na wachimbaji katika eneo la Mwakitolyo lililopo Shinyanga Vijijini. Waziri Mavunde ametangaza habari hizo njema kuwa, tayari Shirika la STAMICO limeanza utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais na kwamba eneo limeshapatikana katika Kijiji cha Mawemelu na ujenzi utaanza hivi karibuni. "M...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

DKT MIGIRO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI KUTOKA CHINA

Image
  Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Jumatatu, Desemba 22, 2025, amefanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao, wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), pamoja na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China.

WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA PILI WA JUKWAA LA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI ZA AFRIKA NA URUSI ULIOFANYIKA TAREHE 19 NA 20 DISEMBA, 2025, JIJINI CAIRO, MISRI

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Urusi uliofanyika tarehe 19 na 20 Disemba, 2025, jijini Cairo, Misri. Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika, Jumuiya za Kikanda za Afrika pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi.  Mkutano huo uliofanyika chini ya Wenyeviti Wawili, Mheshimiwa Dkt. Badr Abdelatty, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri na Mhe. Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi, umetoa nafasi ya nchi za Afrika na Urusi kujadiliana na kukubaliana masuala muhimu yanayogusa maslahi ya pamoja katika nchi zao na katika Umoja wa Mataifa, na Mashirika yake. Mawaziri wa Afrika na Urusi wamesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa na Mashirika yaliyo chini yake, ikiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanyiwa marekebisho ili k...

KAMPUNI PLATIUM CREDIT YATOA MKOPO WA GARI KWA WATANZANIA,RUHUZA AFUNGUKA.

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  KATIKA kuhakikisha wanawainua kiuchumi watumishi wa Umma,wafanyabiashara na Wafanyakazi wa sekta binafsi,Kampuni ya utoaji mikopo ya Platinum credit limited imetanga huduma ya mikopo wa magari kwa riba nafuu. Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Maendeleo ya Biashara,Allan Ruhuza wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 wameamua kuwawezesha watanzania kuweza kumiliki gari. "Sisi Platinum Credit tutagharamia hadi asilimia 65 ya thamani ya Gari yako kwa vigezo rafiki huku mteja atatoa asilimia 35 atatoa mteja "Amesema Ruhuza, Ruhuza ameitaja Mikopo hiyo iliyotamulishwa ni pamoja Logbook Finance Loan(Mikopo yakutumia kadi ya Gari),Civil servants loans(mkopo maalum kwa watumishi wa umma.) Na SMEs Loans(Mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wakati). Hata hivyo,Ruhuza,amesema Mikopo hiyo imebuniwa kwa utaratibu rahisi,upatikanaji wa haraka na masharti rafiki kwa wateja. "Kupit...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image