TUME YA MADINI YAWAALIKA WADAU KUTUMIA MAABARA YA KISASA
Meneja wa Huduma za Maabara ya Tume ya Madini, Mhandisi Mwarabu Mvunilwa amewaalika wadau wa sekta ya madini nchini kutumia maabara ya kisasa ya Tume kwa huduma za uhakika na viwango vya kimataifa. Akizungumza kupitia mahojiano maalum amesema kuwa maabara hiyo, ipo katika Jengo la TIRDO Complex, Msasani – Dar es Salaam, na imekuwa ikihudumia wachimbaji, wafanyabiashara wa madini, wawekezaji pamoja na taasisi mbalimbali kwa huduma za uchambuzi na ushauri wa kitaalamu. Mhandisi Mvunilwa amesema kuwa maabara hiyo ya serikali imewekewa teknolojia ya kisasa ikiwemo mashine za X-Ray Fluorescence (XRF) na fire assay furnaces zinazotoa matokeo ya haraka, sahihi na yenye gharama nafuu. “Tunatoa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa vya ISO 17025. Matokeo yetu yanakubalika ndani na nje ya nchi, hivyo kuwa msingi wa uwazi katika biashara ya madini,” amesema. Huduma zinazotolewa na maabara hiyo ni pamoja na uchambuzi wa madini ya metali kwa kutumia XRF, vipimo vya dhahabu na fedha kwa nji...