TUSHEHEREKEE MWAKA MPYA PASIPO KULETA TAHARUKI YOYOTE:RC CHALAMILA
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert John Chalamila, amewasihi wananchi pindi wanaposheherekea sikukuu za mwaka mpya pasipo kuleta taharuki yoyote na pia ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kusherehekea Mwaka Mpya kwa njia zisizozua taharuki kwa wengine. Akizungumza na waandishi wa habari Leo 31,2025 Mkuu wa mkoa Albert Chalamila amesema kuwa tabia ya kupiga fataki kiholela na kuchoma matairi wakati wa shamrashamra za Mwaka Mpya inaweza kuleta usumbufu, hofu na hata kuathiri usalama wa wananchi, hasa ikizingatiwa hali ya kiusalama ambayo jiji hilo limepitia miaka ya nyuma. Amesisitiza kuwa kwa yeyote anayehitaji kulipua fataki ni lazima kupata kibali maalumu kutoka kwa Jeshi la Polisi, huku akibainisha kuwa maofisa wa usalama watakuwepo eneo la tukio kuongoza utaratibu na kuhakikisha kunafuatwa sheria na taratibu. “Ni muhimu kuwaheshimu majirani na kuwapasha taarifa mapema endapo utalipua fataki ili kuepusha hofu au taharuki isiyo ya la...