Posts

Showing posts from October, 2025

DKT. MWINYI APIGA KURA MJINI MAGHARIBI

Image
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika zoezi la upigaji wa kura katika Kituo cha kupigia Kura cha Kariakoo kilichopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi leo Jumatano Oktoba 29, 2025.

WAPIGA KURA WA MWANZA WAJITOKEZA KUPIGA KURA KWA WINGI ILEMELA MWANZA

Image
 Wapiga Kura wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupiga kura katika Kata ya Kirumba, Ilemela Mwanza.

RC MAKALLA AONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUPIGA KURA

Image
 *_Asema hali ya usalama mkoa Arusha ni Shwari na Salama_*     *_Awahimiza wananchi wenye sifa kujitokeza kutumia haki yao ya Kikatiba_*  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla mapema asubuhi ya leo Oktoba 29,2025 amewaongoza wananchi wa mkoa wa Arusha kupiga kura kwa kutimiza wajibu wake na kutumia haki yake ya Kikatiba ya kuchagua viongozikatiba ya kkuchagua viongozi. CPA Makalla mara baada ya kukamilisha zoezi la upigaji kura kwenye Kituo chake cha AICC Hospitali Jijini Arusha, ameendelea kuwahakikishia wananchi wote kuwa hali ya usalama iko shwari na kuwataka wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kutimiza haki yako ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Aidha, CPA Makalla ametumia muda huo kuwahamasisha wananchi wa Arusha wenye sifa kujitokeza kupiga kura huku akiwathibitishia wananchi wote kuwa, Tume imeweka utaratibu mzuri kwa kuwa na vituo vingi, ambavyo vinawezesha mpiga kura kutotumi...

DKT. TULIA APIGA KURA UYOLE, AHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI

Image
  Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Ubunge Jimbo la Uyole kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Tulia Ackson, leo tarehe 29 Oktoba, 2025 amejitokeza kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Tambukareli mkoani Mbeya. Dkt. Tulia ametoa wito kwa wananchi wa jimbo hilo na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua Viongozi wanaowataka.

DKT. TULIA ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI KWENYE UCHAGUZI

Image
Spika wa Bunge ambaye pia ni mgombea wa Jimbo la Uyole, Dkt. Tulia Ackson, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu, akisisitiza umuhimu wa kutumia haki yao ya kidomokrasia kuchagua viongozi wanaowataka. Dkt. Tulia alitoa wito huo mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Tambukareli, ambako aliwasihi wananchi wasikae majumbani bali washiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa taifa. Amesema uchaguzi ni fursa ya wananchi kuamua mustakabali wa nchi yao kupitia kura, hivyo ni wajibu wa kila mwenye sifa kuhakikisha anatumia haki hiyo kwa utulivu na uwajibikaji. Aidha, amewapongeza watendaji wa tume ya uchaguzi kwa maandalizi mazuri na kuhimiza kuendelea kudumisha amani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi.

ZOEZI LA KUPIGA KURA LAENDELEA UBUNGO KWA UTULIVU

Image
  Zoezi la kupiga kura linaendelea kwa utulivu katika kituo cha Buyuni, kilichopo Changanyikeni, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, likianza mapema saa 1.00 asubuhi. Wananchi wameendelea kujitokeza kwa utaratibu kutekeleza haki yao ya kikatiba katika mazingira ya amani na usalama. Maafisa wa tume ya uchaguzi wanaendelea kusimamia mchakato huo kwa weledi, wakitoa huduma kwa wapiga kura kwa namna inayoonesha maandalizi mazuri ya uchaguzi huu. Wananchi wametakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani, wakizingatia maelekezo yanayotolewa na wasimamizi wa vituo, ili zoezi hilo muhimu kwa demokrasia ya nchi liwe na mafanikio makubwa.

TAASISI ZA MADINI ZAELEZA MAFANIKIO ROBO YA KWANZA 2025/26

Image
*Tume ya Madini Yakusanya Bilioni 315.4 Robo ya Kwanza* *Kilo 2,356.413 za Dhahabu Zasafishwa Kiwanda cha Mwanza Metals Refinery* *Ununuzi wa Helkopta ya Utafiti unaendelea* *Viwanda vya Kuzalisha Mkaa wa Rafiki Briquettes Mbioni Dodoma, Tabora* *TGC Yaanzisha duka la bidhaa za mapambo ya Vito, AICC-Arusha* *Dodoma* Menejimenti ya Wizara ya Madini Oktoba 27, 2025 ilikutana na Wakuu wa Taasisi zake katika kikao kilicholenga kupokea taarifa ya ufuatiliaji na tathmini kwa majukumu yaliyotekelezwa na taasisi hizo katika kipindi cha Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2025/26.  Taasisi zilizo chini ya Wizara ni pamoja na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini, Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) cha jijini Arusha.  Katika taarifa iliyowasilishwa na Tume ya Madini, ilielezwa kwamba, katika kipindi robo ya kwanza, ta...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

ASKOFU MWANKUGA AWASIHI WATANZANIA KUJITOKEZA KUPIGA KURA KESHO NA KUTILIA MKAZO AMANI NA MAENDELEO

Image
Baba Askofu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki Askofu Lawi Mwankuga amesisitiza umuhimu wa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura hapo Kesho Jumatano Oktoba 29, 2025 na kutanguliza wajibu wa kulinda amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa Uchaguzi ni tukio la wakati mmoja na maisha ni lazima yaendelee. Baba Askofu Mwankuga ametoa wito huo leo Jumanne Oktoba 28, 2025 Jijini Dar Es Salaam punde baada ya Vyama vya siasa kuhitimisha Kampeni zao, tayari kwa uchaguzi Mkuu, akisisitiza pia wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali kuyaishi yale yatakayoleta maendeleo kwa Watanzania sambamba na kutanguliza mbele maslahi yao pale watakapoibuka na ushindi wa kura za wananchi katika uchaguzi huo. Baba Askofu amesisitiza pia umuhimu wa kuchagua kiongozi mwenye dhamira ya dhati katika kuwaletea watanzania maendeleo katika nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali Chama anachotokea Mgombea wa nafasi hizo zinazowaniwa hapo kesho. Amewashukuru pia na ...

UCHAGUZI MKUU WA 2025 NI HALALI” – MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Image
Na Mwandishi wetu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ni halali kwakuwa umefuata misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za Uchaguzi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo katika Mkutano na Vyombo vya Habari uliofanyika Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 28 Oktoba, 2025. Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Johari amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa, ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  “Ibara ya 5(1) ya Katiba yetu inatoa haki kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura katika uchaguzi unaofanyw...

JESHI LA POLISI LATOA TAHADHARI DHIDI YA TAARIFA ZA UONGO,UCHOCHEZI LAHIMIZA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Image
Dodoma Jeshi la Polisi nchini limesema hali ya usalama inaendelea kuwa shwari kote nchini kuelekea siku ya kupiga kura hapo kesho, Oktoba 29, 2025, na kwamba hakuna tishio lolote la kiusalama lililobainika hadi sasa.  Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dodoma DCP David Misime amesema jeshi limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote wanatekeleza haki yao ya kupiga kura katika mazingira ya amani, utulivu na usalama wa kutosha. Ameeleza kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, kumekuwa na juhudi za baadhi ya watu wachache wanaojaribu kuvuruga amani kwa njia za kidijitali baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa vitendo, jambo ambalo jeshi limeanza kulifuatilia kwa karibu. “Baada ya kuona wameshindwa kuvuruga amani ya nchi, watu hao wameunda kikundi cha vijana wanaotengeneza picha, video na taarifa mbalimbali bandia kuhusu matukio yanayodaiwa kutokea nchini, kisha kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii ili kuonesha kana kwamba ni halisi,” amesema msemaji huyo. Aidha, Jeshi...

USALAMA UMEIMARISHWA NCHI NZIMA, TUJITOKEZE KUPIGA KURA BILA HOFU — BASHUNGWA

Image
πŸ“Œ Bashungwa atoa onyo kali kwa watakaovuruga uchaguzi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, amewahakikishia Watanzania wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa nchi nzima, hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki kupiga kura kuwachagua Rais, Wabunge na Madiwani bila hofu yoyote kesho, tarehe 29 Oktoba 2025. Bashungwa ameyasema hayo leo, tarehe 28 Oktoba 2025, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaifa, ikiwa ni siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. “Kesho, Oktoba 29, hakutakuwa na shida yoyote. Vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, vipo timamu nchi nzima. Usalama umeimarishwa, kwa hiyo Watanzania tuende tukapige kura bila kuwa na wasiwasi wowote. Na yeyote atakayethubutu kuvuruga amani, atakutana na kisiki,” amesisitiza Bashungwa. Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa vijana kujitokeza kushiriki kikamilifu ka...

ASKOFU KAEMELA AHIMIZA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA KULINDA AMANI YA TANZANIA

Image
Askofu Jacob William Kaemela wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania, ametoa wito wa matumizi sahihi ya mitandao ya Kijamii na kujiepusha na uhalifu wa kimitandao pamoja na uvunjifu wa amani na sheria zilizopo nchini Tanzania. Askofu Kaemelea ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijiji Dar Es Salaam, pembezoni mwa Kongamano la Viongozi wa Dini waliokutana Dar Es Salaam kujadili kuhusu amani kuelekea uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akihimiza pia kujiridhisha na kila habari inayochapishwa kwenye mitandao ya Kijamii ili kujitenga na habari za upotoshaji zinazoweza kumuwema mtu matatani kulingana na sheria na miongozo ya Mitandao hiyo. "Watu wana chaguo, unaweza kuchagua kuwa mtu mwema ukatumia vizuri mitandao ya kijamii lakini ujue tu kuwa ukitumia mitandao ya kijamii kwa nia ovu wewe utakuwa muhalifu kama muhalifu mwingine yoyote yule. Muhimu tuhimize amani, kuacha uhalifu na mitandao isitumike kama sehemu ya kufanya uhalifu." Amesi...

UTENDAJI KAZI PURA WAMKOSHA NAIBU KATIBU MKUU TUGHE TAIFA

Image
Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa , Ndg. Amani Msuya ameeleza kuvutiwa na kiwango cha utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa mwaka 2024/25 kufuatia Mamlaka hiyo kutekeleza majukumu yake kwa zaidi ya asilimia 94.  Msuya ameeleza hayo Oktoba 27, 2025 Mkoani Morogoro wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi PURA kilichofanyika kwa lengo la kujadili, pamoja na mambo mengine, taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25. “Nimevutiwa sana kusikia kuwa, kwa mujibu wa mrejesho wa tathmini ya utekekelezaji wa mjukumu iliyofanywa kupitia Mfumo wa Tathmini ya Utendaji kazi (PEPMIS), PURA ilitekeleza majukumu yake kwa asilimia 94.46 kwa mwaka wa fedha 2024/25” “Kwa kiwango hiki cha utendaji kazi, ni dhahiri kuwa PURA inatekeleza majukumu yake ipasavyo na kwa hakika ni jambo linalostahili pongezi” alisema Msuya.  Msuya pia alitumia fursa hiyo kuwaasa watumishi wa PURA kutobweteka na kiwango cha tathmini cha mwaka wa fedha u...