Posts

Showing posts from September, 2025

DK.MWINYI AAHIDI KUJENGA MASOKO MAPYA 5 ZANZIBAR

Image
Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kujenga masoko makubwa mapya matano ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira bora zaidi. Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mwanakwerekwe leo tarehe 29, Septemba 2025 katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi, Dkt. Mwinyi alisema masoko hayo mapya yatakayojengwa katika maeneo ya Kinyasini, Mwera, Kibandamaiti, Kisauni na Kwahajitumbo yataleta suluhisho la kudumu kwa changamoto za wafanyabiashara. Ameeleza kuwa kukamilika kwa masoko hayo kutapunguza msongamano unaotokana na uhaba wa nafasi, pamoja na kupunguza kodi kubwa zinazowakabili wafanyabiashara hivi sasa. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kumchagua tena yeye pamoja na wagombea wa CCM katika ngazi za ubunge, uwakilishi na udiwani, ili kutimiza dhamira ya ujenzi wa masoko hayo chini ya ...

REA YAUZA MAJIKO 1,500 KWA BEI YA RUZUKU KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Image
๐Ÿ“ŒREA yapongezwa kwa kuuza majiko kwa bei ya ruzuku na kutoa elimu ya miradi ya wakala ๐Ÿ“Geita Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yamehitimishwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambayo yalifunguliwa Septemba 18 na kufikia kilele tarehe 28 Septemba, 2025 Wakala umeshiriki maonesho hayo kwa kutoa elimu ya nishati safi ya kupikia, kutoa elimu ya miradi inayotekelezwa na wakala wa nishati vijijini pamoja na fursa zinazopatikana kwa wakala kama vile vituo vidogo vya mafuta. Sambamba na hayo Wakala unahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuuza kwa ruzuku mitungi ya gesi ya kilo 6 ambayo inauzwa kwa bei ya 50% ambayo ni kiasi cha shilingi 17,500 ambapo jumla ya mitungi 5,00 imeuzwa kwa ruzuku kwenye maonesho. Pamoja na hayo, Wakala unafadhili uuzwaji wa majiko banifu yanayotumia mkaa mbadala pamoja na mkaa wa kawaida, majiko hayo yameuzwa kwa bei ya ruzuku ya 85% ambayo ni shilingi 6,195 ambapo bei yake ya kawaid...

DK MWINYI MUKINIPA RIDHAA YA KUONGOZA TENA NITAWAWEZESHA MITAJI WAFANYABIASHARA

Image
Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema endapo akipata ridhaa ya kuiongoza tena Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano atawawezesha mitaji wafanyabiashara. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Mwanakwerekwe lilopo wilaya ya Magharibi ‘B’ mkoa wa Mjini Magharibi. Amesema serikali ya awamu ya nane imetoa sh.bilioni 96 kwa wafanyabiashara mbalimbali ikiwa ni mitaji ya biashara zao. “Tunatambua kuwa wapo wafanyabiashara waliokuwa bado hawajapata mitaji hiyo lakini kipindi kijacho tunaongeza fungu hilo ili waweze kupata wengi zaidi,” amesema  Pia, Dk.amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo atajenga masoko mengi Zaidi ikiwemo soko la Kibanda maiti,Kisauni,Fuoni,Kwahaji Tumbo na Mwera ili wafanyabiashara waweze kufanyabiashara na kwamba ataendelea kumaliza changamoto zinazowakabili.

UTENDAJI KAZI WA WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE WAIMARIKA

Image
๐Ÿ“Œ *Wapanda kutoka asilimia 95 hadi 96.16 katika kipindi cha robo mwaka* ๐Ÿ“Œ *Mhandisi Mramba asema ongezeko hilo linaakisi utoaji wa huduma kwa wananchi* ๐Ÿ“Œ *Apongeza Taasisi kuendelea kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.* ๐Ÿ“Œ *Asisitiza mitandao ya kijamii kutumika ipasavyo utoaji elimu Nishati Safi ya kupikia.* Imeelezwa kuwa, utendaji kazi wa Wizara ya Nishati kupitia Taasisi inazosisimamia umezidi kuimarika na kufikia asilimia 96.16 katika kipindi cha robo nne ya mwaka 2024/2025. Hayo yamefahamika wakati wa kikao cha Tano cha Tathmini ya utendaji kazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa robo nne ya mwaka 2024/2025 kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba. Tathmini hiyo ya utendaji kazi iliyofanywa na Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini katika Wizara ya Nishati imeonesha kuwa katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2024/2025 utendaji kazi wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati umeimarika kwa zaidi ya asilimi...

MATHIAS CANAL AONGOZA UPATIKANAJI MIL 85 UJENZI WA KANISA KIOMBOI-IRAMBA

Image
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya WAZOHURU MEDIA Ndg Mathias Canal amewaongoza Viongozi wa dini, Wadau wa maendeleo na Waumini kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania-KKKT Usharika wa St George Kiomboi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida. Katika harambee hiyo iliyofanyika leo tarehe 28 Septemba 2025 katika eneo la Ujenzi wa Kanisa Mtaa wa Lulumba, Mgeni huyo rasmi amesimamia upatikanaji wa fedha taslimu Tsh 79,407,000 ambapo ahadi ni Shilingi Milioni 4,010,000 na jumla ya fedha zote zilizopatikana ni Shilingi Milioni 85,017,000. Mgeni rasmi Ndg Mathias Canal pamoja na marafiki zake waliomuunga mkono amechangia jumla ya Tsh milioni 3,835,000 na mifuko 10 ya Saruji. Akizungumza katika harambee hiyo Mathias amesema kuwa Kanisa ni nguzo muhimu ya maisha ya kiroho, kijamii na hata kiuchumi. Kupitia kanisa waumini wanajifunza misingi ya upendo, mshikamano, uadilifu na ujenzi imara wa taifa.  "Ujenzi wa kanisa si kwa ajili ya kizazi cha leo pekee,...

REA KIVUTIO KIKUBWA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU

Image
*๐Ÿ“ŒBanda la REA limepamba Maonesho ya Madini Geita* *๐Ÿ“ŒMajiko ya gesi ya kupikia nayo yanatolewa kwa bei ya ruzuku Geita* ๐Ÿ“Geita Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.  Katika maonesho ya madini, REA inauza majiko banifu kwa gharama ya shilingi 6,200 tu ambapo kabla ya ruzuku kutolewa na Serikali majiko hayo yaliuzwa kwa gharama ya shilingi 41,300. Majiko banifu yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa (carbon monoxide) hivyo kusaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa. Katika mkoa wa Geita kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.

DKT. BITEKO AMPA POLE RAIS MWINYI, ASHIRIKI MAZISHI YA KAKA YAKE

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameungana na mamia ya waombolezaji kutoa pole kwa familia ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha kaka yake Abass Mwinyi ambaye pia alikuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Fuoni kilichotokea Zanzibar, Unguja usiku wa kuamkia Septemba 25, 2025. Dkt. Biteko ameshiriki mazishi hayo Septemba 26, 2025 Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar. Ambapo ameungana na viongozi mbalimbali akiwemo Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Stephen Wasira, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla . Aidha, baada ya mazishi baadhi viongozi walipata fursa ya kutoa heshima katika kaburi la Hayati Ali Hassan mwinyi lililopo Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar. Awali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alifika msiba...

MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY YAKUSANYA ZAIDI YA TANI 5 ZA DHAHABU KWA NIABA YA BOT

Image
๐Ÿ“Mwanza Kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery (MPMR) kilichopo jijini Mwanza, kimefanikiwa kukusanya zaidi ya tani tano za dhahabu kwa niaba ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Hayo yamesemwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Nyaisara Mgaya, alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka nchini Malawi uliotembelea mkoani humo kwa lengo la kujifunza kuhusu usimamizi na uendeshaji wa biashara ya madini, hususan mfumo wa masoko unaotumika nchini Tanzania. Mhandisi Mgaya amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha hadi kilo 960 za dhahabu kwa siku, ingawa kwa sasa kinatumia mashine zenye uwezo wa kusafisha kilo 480 kwa siku, kutokana na upatikanaji wa malighafi. Katika kikao hicho, kiongozi wa ujumbe kutoka Malawi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo ya Biashara za Vikundi nchini humo, Zizwan Khonje, amemshukuru Afisa Madini wa Mkoa wa Mwanza kwa elimu waliyoipata kuhusu mfumo wa biashara na masoko ya madini hapa nchini. “Tanzani...

DK MWINYI APOKEA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea mkono wa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Abbas Ali Mwinyi, kilichotokea jana tarehe 25 Septemba 2025. Katika kuonesha mshikamano wa kitaifa kwa familia ya marehemu Abbas Mwinyi, viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, walifika kutoa mkono wa pole nyumbani kwa familia Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi B. Miongoni mwa walioungana na Rais Samia ni Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Mashaka Biteko, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro, pamoja na viongozi wengine mbalimbali. Marehemu atasaliwa Masjid Jamia Zinjibar, Mazizini baada ya Sala ya Ijumaa, na kuzikwa Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja,...

DKT. MWINYI AWATAKA WAZANZIBARI KUDUMISHA UMOJA, AAHIDI MAENDELEO MAKUBWA

Image
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Wazanzibari kuepuka siasa za kikanda, kidini, ubaguzi na mifarakano, akisisitiza kuwa mshikamano na amani ni nguzo kuu za maendeleo. Akizungumza leo tarehe 24 Septemba 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Makombeni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Dkt. Mwinyi alisema CCM itaendelea kudumisha amani, maridhiano na mshikamano ili Serikali iendelee kutekeleza mipango ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi wote. Ameeleza kuwa kasi ya maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita itaongezeka zaidi kupitia miradi mikubwa ya maendeleo. ๐Ÿ‘‰ Sekta ya Afya: Serikali itahakikisha hospitali zote nchini zinatoa huduma za kibingwa, ikiwemo Hospitali ya Abdalla Mzee kupatiwa mashine ya MRI. ๐Ÿ‘‰ Miundombinu: Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Pemba na barabara ya Chakechake–Mkoani utaiwezesha P...

HEMED SULEIMAN ABDULLA: DK.MWINYI AMETEKELEZA MIRADI MUHIMU KWA MAENDELEO YA MKOANI PEMBA

Image
‎ ‎Mgombea nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo la Kiwani kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hemed Suleiman Abdulla, amempongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa kazi kubwa na za kutukuka alizozifanya katika maeneo mbalimbali ya maendeleo, akisisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar wanapaswa kumshukuru na kumpigia kura kwa kishindo ifikapo Oktoba 29. ‎ ‎Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Makombeni, wilaya ya Mkoani, mkoa wa Kusini Pemba, Hemed alisema kuwa miradi mingi muhimu ya maendeleo imefanywa chini ya uongozi wa Dk. Mwinyi, hususan katika wilaya ya Mkoani, ambapo alisema anaendelea kushuhudia mafanikio makubwa yanayotokana na uongozi huo. ‎ ‎"Mambo matatu ni muhimu ambayo ni lazima niyaeleze. Kila nikipita kwenye miradi hii, wananchi wananishukuru kwa kazi kubwa anayoifanya Dk. Mwinyi. Pia, wamekuwa wakimuombea dua na baadhi yao walikuwa wananiingiza salamu maalum za kumfikishia Dk. Mwinyi," alisema Hemed, akionyesha furaha na shukran...

PROF. MBARAWA ASEMA WANANCHI WA MKOANI WANA SABABU KUBWA YA KUMSAPOTI DK. HUSSEIN MWINYI KWA URAIS WA ZANZIBAR ‎

Image
‎ ‎Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba - Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkoani kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Prof. Makame Mbarawa, ametoa sababu za msingi za kwa nini wakazi wa wilaya hiyo wanapaswa kumchagua Dkt. Hussein Ali Mwinyi kama Rais wa Zanzibar katika uchaguzi unaotarajiwa. ‎ ‎Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Makombeni, Wilaya ya Mkoani, Prof. Mbarawa alisema kuwa Dkt. Mwinyi amekuwa na mchango mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo, hasa katika sekta ya miundombinu, ambayo imekuwa na changamoto kubwa kwa miaka mingi. ‎ ‎Bandari ya Mkoani Yapata Mwelekeo Mpya ‎ ‎Prof. Mbarawa alitaja moja ya mafanikio makubwa ya Rais Dkt. Mwinyi kuwa ni uboreshaji wa Bandari ya Mkoani, ambayo imekuwa na umuhimu mkubwa kwa uchumi wa wilaya hiyo na mkoa mzima wa Kusini Pemba. Alisema kabla ya Dkt. Mwinyi kuchukua hatua ya kuboresha bandari hiyo, meli za mizigo hazikuwa zikifika mara kwa mara, hali iliyosababisha matatizo kwa wafanyabiashara na wananch...

TANZANIA YANG’ARA UWEKEZAJI KATIKA ELIMU KWA RASILIMALI ZA NDANI

Image
๐Ÿ“Œ Dkt. Biteko asema tafiti zaonesha elimu bora huchangia asilimia 20-30 ya ukuaji wa uchumi ๐Ÿ“Œ Walimu milioni 17 wa shule za msingi na sekondari wahitajika Afrika ifikapo 2030 ๐Ÿ“Œ Bajeti ya elimu yaongezeka kwa trilioni 1.44 tangu mwaka 2020/21 Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua katika matumizi ya rasilimali za ndani na kuwekeza katika sekta ya elimu kwa maendeleo endelevu. Amesema hayo Septemba 24, 2025 jijini Dar es salaam wakati akifungua Kongamano la Tano la Kimataifa la Elimu Bora lililoongozwa na kauli mbiu inayosema “Kuimarisha mifumo na uwekezaji: Kusonga mbele katika Uhamasishaji wa Rasilimali za Ndani kwa ajili ya Elimu Jumuishi, Bora na Endelevu Barani Afrika”. Dkt. Biteko ametaja hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwa ni pamoja na kutunga na kuboresha Sera, Sheria na miongozo mbalimbali ya elimu, kuongeza kiwango cha bajeti ya elimu kutoka sh...

SERIKALI YAONDOA VAT KWA VITUO VYA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG)

Image
๐Ÿ“Œ *Lengo ni kuongeza uwanda wa matumizi ya CNG katika vyombo vya moto nchini* ๐Ÿ“Œ *Mhandisi Mramba azindua kituo cha Gesi Asilia iliyoshindiliwa ( CNG) cha PUMA Energy* ๐Ÿ“Œ *Asema vifaa vya kuwekea mifumo ya gesi kwenye vyombo vya moto pia imeondolewa* ๐Ÿ“Œ *Apongeza PUMA Energy kwa kuiunga mkono Serikali katika ujenzi wa vituo vya CNG* Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amesema Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa vituo vyote vya Gesi iliyoshindiliwa (CNG) nchini ili kuhamasisha matumizi ya gesi asilia kwenye vyombo vya moto kupitia uwepo wa vituo vingi vya kutoa huduma hiyo kwa wananchi.  Amesema kuwa Serikali pia imeondoa kodi kwenye vifaa vya kuwekea mifumo hiyo ya gesi kwenye vyombo vya moto kama vile magari na bajaji ikiwa ni hatua pia ya kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto. Mhandisi Mramba ameeleza hayo leo Septemba 24, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua kituo cha Gesi Asilia iliyoshindiliwa (CNG) c...

DKT. ABBAS AFUNGUA KIKAO KAZI CHA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, amefungua rasmi kikao kazi cha kuandaa Mpango Mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2026/2027 hadi 2030/2031, akisisitiza umuhimu wa kuwa na malengo na mwelekeo thabiti ili kuiwezesha wizara hiyo kufanikisha malengo yake kwa ufanisi. Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho kilichowakutanisha Wakuu wa Idara, Vitengo pamoja na Maafisa Bajeti wa wizara hiyo, leo Septemba 23, 2025, jijini Dodoma, Dkt. Abbas amesema kuwa kazi ya kuandaa mpango huo ni ya msingi kwa maendeleo ya wizara kwa kuwa utasaidia kuchambua mahitaji ya muda mrefu na maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kuongeza ufanisi wa utendaji. “Tunapozungumzia Mkakati (Strategic Plan), tunamaanisha mpango kazi wa muda mrefu. Nina imani mkakati huu utaweza kuchambua mahitaji ya muda mrefu ya Wizara ili tufanikishe malengo yetu,” amesema Dkt. Abbas. Aidha, amewataka viongozi hao kuainisha fursa zilizopo katika sekta ya maliasili na utalii, akieleza kuwa...

NISHATI SAFI INATEKELEZWA KWA VITENDO GEITA

Image
*๐Ÿ“ŒChereko yatajwa na wananchi Banda la REA* *๐Ÿ“ŒMajiko ya gesi na majiko banifu yanauzwa kwa bei ya ruzuku* Wananchi wakiwa katika banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kununua majiko ya gesi na majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

TUME YA MADINI YAVUNJA REKODI YA UPIMAJI SAMPULI KWA MWAKA 2024/2025

Image
Maabara ya Tume ya Madini imevuka lengo la upimaji sampuli za madini kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2024/2025, baada ya kupima jumla ya sampuli 7684 dhidi ya lengo la 6,800.  Hili ni ongezeko linaloashiria ufanisi mkubwa wa maabara katika kutoa huduma kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini. Akizungumza katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita, Mkemia kutoka maabara hiyo, David Lyandala amesema maabara inaendelea kutoa huduma za kitaalam za uchunguzi wa madini ili kubaini ubora na kiasi kilichomo.  Huduma hizo zinajumuisha uchunguzi wa dhahabu, makinikia, kaboni, kimiminika chenye dhahabu, mbale za udongo na miamba kwa kutumia (Fire Assay), pamoja na uchunguzi wa metali kama shaba, chuma, nikeli, manganizi, galena na zinki kwa kutumia mashine za kisasa za X-Ray Fluorescence (XRF). Aidha, maabara hupima madini ya kinywe (graphite), unyevunyevu wa udongo na miamba, pamoja na upotevu wa uzito kwa kuchoma (Loss in Ignition).  Lyandala...