Posts

Showing posts from August, 2025

CAG AFURAHISHWA NA MAKUMBUSHO YA NGORONGORO LENGAI UNESCO GEOPARK.

Image
Na Mwandishi Wetu, Karatu. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Charles Kichere, amefanya ziara maalum kwenye jengo la Makumbusho ya Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu kwenye Eneo la Makumbusho hayo.  CAG Kichere ambaye aliongozana na mwenyeji wake, Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Bw. Abdul-Razaq Badru na menejimenti yake, amejionea na kujifunza urithi wa kitamaduni unaoelezea upekee wa vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, shughuli za utamaduni, urithi na historia za makabila mbalimbali. Akiwa ndani ya Jengo hilo, CAG Kichere alipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhifadhi Mkuu Dr. Agnes Gidna ambaye ni Mtaalam wa Urithi wa Utamaduni NCAA, ambapo alionekana kufurahishwa na namna NCAA ilivyowekeza kwenye Makumbusho hiyo ambayo itatumika kama kivutio cha utalii pamoja na kujifunza kwa wadau mbalimbali. Hifadhi ya jiolojia ya Ngorongoro Lengai unatokana na urithi wa kijiolojia, kiikolojia na kiutamaduni unaojumuisha Mlima Lengai wen...

SHIMIWI NI MAHALA PA KAZI – Bi ZIANA MLAWA

Image
πŸ“Œ *Asema Wizara ya Nishati ipambane irudi na ushindi* πŸ“Œ *Asema Wizara ya Nishati iwe mfano kwa Wizara zingine* Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Bi. Ziana Mlawa leo amesema kushiriki michezo mbali mbali inasaidia katika kujenga afya ya mwili na akili hivyo mtumishi anapopata nafasi ya kushiriki michezo yeyote aitumie ipasavyo pia husaidia hali itakayowajengea uwezo kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi. Bi. Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Nishati watakao shiriki michezo ya SHIMIWI itakayofanyika jijini Mwanza kwanzia tarehe 1 Septemba 2025 " Pamoja na kushiriki michezo ambapo ni mbali na eneo la kazi mkumbuke mkiwa huko ni eneo la kazi nidhamu na uadilifu uwe kipau mbele mdaa wote muwapo kwenye michezo hiyo." Amesisitiza Bi. Mlawa Ameongeza kuwa watumishi hao wajitahidi wapate ushindi ambapo kwa ushindi huo Wizara itapata heshima njee na ndani ya Wizara

RAIS SAMIA AMEWASHA UMEME VIJIJI VYOTE ARUSHA

Image
*πŸ“ŒVitongoji 936 vimefikiwa na huduma ya umeme Arusha* *πŸ“ŒREA yaahidi kufikisha umeme kwa wakati ili kukuza uchumi wa wananchi* πŸ“Arusha Imeelezwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), amewezesha kuwasha umeme vijiji vyote 368 sawa na asilimia 100 na sasa utekelezaji unaendelea kwa kasi ya kupeleka huduma ya umeme kwenye vitongoji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo jijini Arusha.  Hayo yamebaibishwa leo Agosti 28, 2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, wakati wa ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, sambamba na kuzungumza na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ambapo ameweza kushuhudia wananchi wakiunganishiwa huduma ya umeme Wilaya ya Arumeru, Kitongoji cha Kisongo Juu jijini humo.  Ameongeza kuwa, mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji unaendelea vizuri ambapo vitongoji 936 kati ya vitongoji 1,50...

‎MRISHO KAMBA AAHIDI MAGEUZI MAKUBWA SANDALI, AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUANZA KAMPENI ‎

Image
‎Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM JAMII HURU  ‎Dar es Salaam, Agosti 27, 2025 — Mgombea Udiwani wa Kata ya Sandali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mrisho Kamba, amesema yupo tayari kuwatumikia wananchi wa kata hiyo na ameahidi kuleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo iwapo atachaguliwa kuwa diwani. ‎ ‎Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurudisha barua ya uteuzi kutoka ofisi za Kata ya Sandali, Kamba alisema amefarijika sana na imani ambayo chama chake kimemuonesha kwa kumpa ridhaa ya kuwania nafasi hiyo muhimu ya uongozi. ‎ ‎"Nimepokea kwa moyo wa shukrani uteuzi huu kutoka CCM. Ni heshima kubwa na wajibu mzito ambao nipo tayari kuubeba kwa ajili ya maendeleo ya Sandali na ustawi wa wananchi wake," alisema Kamba. ‎ ‎Kamba alieleza kuwa ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha kata ya Sandali inapiga hatua kimaendeleo kupitia mipango ya kimkakati katika sekta za elimu, afya, miundombinu na uwezeshaji wa vijana na wanawake kiuchumi. ‎ ‎Aidha, aliwataka wananchi wa Kata...

REA YAENDELEA KUWAUNGANISHIA UMEME WANANCHI MKOANI MANYARA

Image
*πŸ“ŒBodi ya REA yashuhudia wananchi wakiunganishiwa umeme* *πŸ“ŒVijiji vyote 440 vimeunganishwa na umeme Manyara* *πŸ“ŒWakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA watakiwa kumaliza kazi kwa wakati* *πŸ“ŒElimu umuhimu wa huduma ya umeme kwa wananchi yatolewa* πŸ“Manyara Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeendelea kutekeleza miradi ya nishati kwa kuunganisha wateja umeme katika maeneo ya vijijini ili kuboresha na kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi mkoani Manyara. Hayo yamebaibishwa leo Agosti 27, 2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, wakati wa ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, sambamba na kuzungumza na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ambapo ameweza kushuhudia wananchi wakiunganishiwa huduma ya umeme kijiji cha Chemchem, Kitongoji cha Soraa mkoani Manyara. "Sisi REA tayari tumekamilisha kupeleka umeme kwenye vijiji vyote 440 vya mkoa huu wa Manyara, sasa tuna...

DKT. BITEKO AZINDUA TEKNOLOJIA YA KUONDOA UVIMBE MWILINI BILA UPASUAJI

Image
πŸ“Œ Ni kwa mara ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati πŸ“Œ Aipa kongole Hospitali ya Kairuki kwa kutoa punguzo la asilimia 50 kwa wagonjwa 50 wa kwanza πŸ“Œ Asema Serikali itaendelea kuweka msukumo ushirikiano na Sekta binafsi πŸ“Œ Awaasa Watendaji Wizara ya Afya kutoogopa kujifunza pale Sekta binafsi inapofanya vizuri πŸ“Œ Wagonjwa 300 wanufaika na teknolojia ya utoaji uvimbe bila upasuaji Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameziindua teknolojia ya kuondoa uvimbe mwilini bila upasuaji inayofahamika kama High-Intensity Focused Ultrasound (HIFU) katika Hospitali ya Kairuki ikiwa ni mara ya kwanza kwa huduma hiyo kuzinduliwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati. Akizindua huduma hiyo Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam, Dkt. Biteko amepongeza Watendaji wa hospitali ya Kairuki pamoja na muasisi wake Hubert Kairuki na Mkewe kwa uthubutu wao katika masuala mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma hiyo ya HIFU ambayo...

SERIKALI YASISITIZA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KATIKA UTEKELEZAJI WA ASDP II

Image
NA.MWANDISHI WETU – DODOMA Serikali imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II), hususan katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu. Akizungumza katika kikao kazi cha waratibu wa programu hiyo kilichofanyika leo Agosti 27, 2025 jijini Dodoma, Mratibu wa Taifa wa ASDP II kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Salim Nandonde, alisema sekta binafsi ni nguzo muhimu katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo na mifumo ya chakula nchini. “Uratibu wa ASDP II unaoratibiwa katika ngazi ya taifa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na OR-TAMISEMI katika ngazi za mikoa na halmashauri, unalenga kuhakikisha sekta binafsi inashiriki kikamilifu, hasa kwenye kuongeza thamani katika mazao na mifumo ya chakula ili kuongeza tija na ushindani,” alisema Dkt. Nandonde. Akiainisha maeneo ya utekelezaji wa programu hiyo, Dkt. Nandonde alitaja dh...

MAKONDA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE ARUSHA MJINI

Image
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Arusha Mjini, Paul Christian Makonda rasmi amechukua fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) jijini Arusha. Makonda aliyeambatana na mkewe pia amesindikizwa na watu zaidi ya 150,000 wakiwamo viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya ya Arusha.

DKT. DOTO BITEKO ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOMBE

Image
πŸ“Œ Wanachama zaidi ya 1000 wajitokeza kumdhamini πŸ“Œ Dkt. Biteko ahimiza Kampeni za kistaarabu, mshikamano na upendo πŸ“Œ Awaomba Wana Bukombe kumchagua Dkt. Samia, Biteko na madiwani wa CCM Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukombe, Zedekiah Solomon Osano amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 26, 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bukombe - Mkoani Geita. Makabidhiano hayo ya fomu ni utekelezaji wa ratiba kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka 2025 Aidha, Maelfu ya wana CCM na wapenzi wa chama hicho wamemsindikiza mgombea kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume huru ya Uchaguzi. Katika hali isiyo ya kawaida, zaidi ya wanama 1000 wamejitokeza kumdhamini Dkt. Biteko ikilinganishwa na mahitaji ya wadhamini 25 waliohitajika kisheria. Akizungumza na wanaCCM katika viwanja Ofisi ya CCM Wilaya y...

DKT. BITEKO AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO VIKAO VYA KIMKAKATI VYA WENYEVITI WA BODI NA WAKUU WA TAASISI

Image
πŸ“Œ Awakumbusha kuhusu dhamana waliyobeba ya kubadili maisha ya watanzania kupitia mtaji wa shilingi Trilioni 86 waliopewa πŸ“Œ Afunga Kikao kazi cha Tatu cha Wenyeviti wa Bodi, Wakuu wa Taasisi πŸ“Œ Asema Rais, Dkt. Samia anatambua mchango wa Taasisi za umma; ana matarajio makubwa kutoka kwao πŸ“Œ Awakumbusha kutekeleza Maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais πŸ“Œ Kikao kazi chafanyika kwa mafanikio; chahusisha washiriki zaidi ya 600 Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma nchini kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kimkakati yanayofikiwa katika vikao kazi wanavyofanya kwa kutambua kuwa wamebeba dhamana ya kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mtaji wa shilingi Trilioni 86 ambao Serikali imewekeza kwenye Taasisi na mashirika yake.. Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 26 Agosti 2025 jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi...

WAMACHINGA KAWE KWA USHIRIKIANO NA CAMGAS KUANDAA KONGAMANO LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Image
  Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎ ‎Lengo ni kuunga mkono jitihada za Dkt.Samia kutangaza matumizi ya Nishati safi y kupikia. ‎ ‎ ‎Kikundi Cha Wamachinga"Ngome ya mama Samia"Kawe ,Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na kampuni ya Camgas -Camel Oil Ltd,kimeamdaa kongamano la kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia litakalofanyika Msasani Beach  August, 26 Mwaka huu.  ‎ ‎Kongamano hilo litakua na fursa mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu juu ya matumizi sahihi ya gesi safi ya kupikia ili jamii iweze kuachana na matumizi ya Nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa ambayo imekua ikiathiri afya za watumiaji pamoja Mazingira kwa ujumla. ‎ ‎Taarifa hiyo imetolewa leo August 21,2025,katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam na Mratibu Mkuu wa Kongamano hilo Potipoti Ndanga wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakusema kuwa kufanyika kwa kongamano hilo ni kutokana na utafiti walioufanya kuanzia ngazi ya Serikali ya mtaa,huku kaulimbiu yake ikiwa ni"Gesi safi ni ha...

AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA

Image
πŸ“Œ Dkt.Biteko ashuhudia utiaji saini mikataba itakayowezesha Wilaya zote Kagera kupata umeme wa Gridi πŸ“Œ Awali umeme mwingi ulikuwa ukitoka nchini Uganda hivyo kufanya Mkoa kutokuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha πŸ“Œ Asema Rais.Dkt. Samia alishatoa maagizo ya mradi huo kutekelezwa kwa wakati na kwa usahihi πŸ“Œ Aagiza wananchi 1,014 waliopisha mradi kulipwa fidia kuanzia mwezi Septemba 2025 πŸ“Œ Apongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa ufanisi katika.usimamizi wa miradi Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Ahadi ya Serikali ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera imetekelezwa baada ya Serikali kusaini mikataba ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benako, Ngara hadi Kyaka wilayani Misenyi na kituo cha kupoza umeme cha Benako cha msongo wa kilovoti 220/33, hatua inayotoa uhakika kwa Mkoa huo sasa kupata umeme wa gridi badala ya kutegemea umeme kutoka Uganda kwa kiasi kikubwa. Akizungumza baada ya kushuhu...

TANGA MJINI TUNATIKI KWA DKT. SAMIA - UMMY MWALIMU

Image
Aliyekuwa mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu leo Agosti 25, 2025 amewataka wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Tanga kuacha makundi na kujikita katika kutafuta kura za ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassani ambaye ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mauungano wa Tanzania kupitia CCM pamoja na kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo la Tanga mjini ndugu. Kassim Mbaraka Amali na kukiwezesha Chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Octoba 2025. “Watu wa Tanga tunakila sababu za kumpa kura zote za ndio Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri alizofanya Tanga mjini na Taifa letu, hivyo nawaomba sana wanatanga twendeni tukamlipe hisani Dkt. Samia na kazi yetu iwe ni kutafuta ushindi wa Chama Cha Mapinduzi”

UMMY MWALIMU APOKEA UAMUZI W HALMASHAURI KUU YA CCM

Image
Alhamdulillah ala kulli hal Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu. ALHAMDULILLAH Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk kipindi chote cha Utumishi wangu. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini imani hii daima.  UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM Tanga Mjini.  Ninawaomba wanakimji wen...

MKUTANO WA SABA WA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI KUFANYIKA NOVEMBA, 2026

Image
*Yaelezwa Sababu ni kupisha maandalizi ya Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu* *Dodoma* Wizara ya Madini imetangaza kusogeza mbele Mkutano wa Saba (7) wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliokuwa ufanyike mwezi Novemba 2025 na badala yake mkutano huo utafanyika tarehe 19 hadi 21 Novemba 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar EsSalaam. Taarifa iliyotelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba imeleza sababu za kusogezwa kwa mkutano huo kuwa ni kupisha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa nchini uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2025. ‘’Wizara ya Madini inaomba radhi kwa wadau wote wa ndani na nje ya nchi waliokuwa wanatarajia kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ambao ulipangwa kufanyika Novemba 2025,’’ imeeleza taarifa hiyo. Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini unaofanyika kila mwaka tangu 2019 ukibebwa na kaulimbiu mbalimbali, hutumika kama jukwaa la kujadili...

WAZIRI LUKUVI ATOA MAAGIZO YA RAIS SAMIA AJALI YA MGODI NYANDOLWA

Image
NA. MWANDISHI WETU- SHINYANGA Waziri wa nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa viongozi wa Serikali waliopo maeneo ya ajali ya mgodini kushiriki taratibu zote za mazishi kwa walifariki ajali ya mgodini na kuwakilisha rambirambi zake kwa wahusika huku akisihii kuendelea kuratibu vyema shughuli ya uokoaji inayoendelea. Ameyasema hayo wakati wa kikao na viongozi pamoja na ndugu wa waathirika wa ajali ya mgodini katika eneo la tukio la ajali ya mgodi unaomilikiwa na Kikundi cha Wachapakazi katika machimbo ya Nyandolwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. “Rais Samia kaniagiza kuwafikishia salamu za pole na rambirambi pia kanituma kuleta maagizo kwa viongozi wa serikali waliopo eneo hili kuhakikisha wanahudhuria misiba yote ya watu waliopoteza maisha katika ajali hii na kuwakilisha rambirambi alizotoa katika familia hizo” amesema Lukuvi. Agosti 16, 2025 Mkuu wa wilaya ya...

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MGODI NYANDOLWA

Image
NA.MWANDISHI WETU - NYANDOLWA SHINYANGA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi, amemfikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, salamu za pole kufuatia ajali ya kufukiwa kwa mafundi katika Mgodi wa Dhahabu wa Nyandolwa, iliyotokea tarehe 11 Agosti 2025 katika Mkoa wa Shinyanga. Waziri Lukuvi ameeleza kuwa Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo, na kwa niaba ya Rais Samia, ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika tukio hilo la kusikitisha. Aidha, ameeleza kuwa Serikali itagharamia kikamilifu gharama za mazishi kwa waathirika wa ajali hiyo pamoja na matibabu kwa waliofikwa na tukio hilo. Akizungumza na wanandugu wa marehemu na wale waliokwama mgodini, Mhe. Lukuvi amewatia moyo na kuwahakikishia kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Ametoa wito kwa timu za uokoaji kuongeza juhudi na kasi ya uokoaji ili kuwaokoa mafundi waliokwama kwa har...

DKT. BITEKO ATAKA WATUMISHI WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE KUWA MFANO WA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Image
πŸ“Œ Lengo ni kutekeleza Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo πŸ“ŒMatumizi ya Nishati Safi ya Kupikia yapaa kutoka asilimia 6 hadi 20.3 πŸ“Œ Agawa majiko yanayotumia umeme kidogo kwa Watumishi wa Wizara ya Nishati na REA πŸ“Œ Apongeza REA kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia nchini Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewataka watumishi katika Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini ya wizara hiyo kuwa mfano katika matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ili kuitekeleza kwa vitendo ajenda iliyoasisiswa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kwa afya. Dkt. Biteko ametoa maelekezo hayo tarehe 22 Agosti 2025 jijini Dodoma wakati akigawa majiko yanayotumia umeme kidogo kwa watumishi wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo amewataka Watumishi hao wawe mabalozi katika kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia. " Leo t...

AGIZO LA DKT.BITEKO LA MINADA YOTE NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA LAANZA KUTEKELEZWA

Image
πŸ“Œ Wachoma nyama na Mama Lishe katika mnada wa Msalato Dodoma waanza kuonja matunda ya Nishati Safi ya Kupikia πŸ“Œ Dkt. Biteko asema ni matunda ya Rais, Dkt. Samia ambaye anayefahamu machungu ya kutumia Nishati isiyo safi ya Kupikia πŸ“Œ Atoa maagizo kwa Mkurugenzi Jiji la Dodoma kuweka miundombinu itakayohakikisha majiko ya Nishati Safi ya Kupikia ya Wachoma nyama yanakuwa salama πŸ“Œ Apongeza REA, Wizara ya Nishati kutekeleza agizo alilolitoa: STAMICO yatakiwa kuweka kituo cha kudumu cha mkaa mbadala Mnada wa Msalato πŸ“Œ Kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa kujengwa Dodoma Agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alilolitoa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa minada yote nchini inakuwa na miundombinu itakayowawezesha Wachoma nyama, Mama Lishe na Baba Lishe kutumia nishati Safi ya Kupikia limeanza kufanyiwa kazi ikiwa ni utekelezaji wa ajenda ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wote wanatumia Nish...

SERIKALI YAENDELEA NA JITIHADA ZA UOKOAJI MGODI WA NYANDOLWA

Image
*Dkt. Kilabuko atoa wito kwa timu ya uokoaji kuongeza kasi na juhudi za uokoaji* *Mwenyekiti Tume ya Madini atoa Salamu za pole kwa wahanga na waathirika wa ajali Nyandolwa* Imeelezwa kuwa, jitihada za kuendelea kuokoa maisha baada ya ajali ya mgodi kutokea eneo la Nyandolwa mkoani Shinyanga zinaendelea usiku na mchana ambapo hadi kufikia Leo Agosti 21,2025 mafundi 10 kati ya 25 waliokuwa wamekwama chini ya ardhi wameokolewa, huku wanne wakiwa hai, mmoja kati yao akifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini, na saba wakikutwa wamefariki dunia. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkoani humo ambapo amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa tukio hilo lilitokea takribani siku 10 zilizopita, likisababisha shughuli za uokoaji kuendelea kwa muda mrefu katika mazingira magumu. Amesema ajali hiyo ilitokea baada ya ardhi kutitia ghafla na kusababisha kifusi kuporomoka katika mashimo (maduara) ma...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image