KASI NDOGO YA UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA CHALINZE- DODOMA YAMKASIRISHA DKT. BITEKO
π *Asikitishwa mradi huo aliouzindua Novemba 2024 kuwa nyuma kwa asilimia Saba* π *Asema Rais Samia alitoa agizo mradi usichezewe kutokana na umuhimu wake katika mikoa mbalimbali ikiwemo ya Magharibi* π *Asema sababu zilizotolewa na mkandarasi (TBEA) za kusuasua kwa mradi hazikubaliki* π *Atoa maagizo kwa Mkandarasi kuwasilisha mpango kazi mpya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati ili kufidia muda uliopotezwa* π;*Aagiza TANESCO kutumia mapato ya ndani kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekagua mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Zuzu Dodoma na kueleza kutoridhishwa kwake na utekelezaji wa mradi huo ambao ulipaswa kuwa umefikia asilimia 31 lakini kwa sasa umefikia asilimia 24 tangu kuzinduliwa kwake Novemba mwaka 2024. Hali ya kusuasua kwa mradi imebainika wakati Dkt. Biteko akikagua mradi huo katika Kijiji cha Manchali wilayani Chamwino mkoani Dodoma tarehe 2...