Posts

RADA ZA HALI YA HEWA NI MUHIMU KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NCHINI.

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliandaa warsha ya mafunzo ya Rada za Hali ya Hewa na matumizi ya taarifa zinazotokana na Rada, tarehe 26-27 Januari 2026, Dodoma. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiufundi katika matumizi ya teknolojia Rada, hususan katika uchambuzi, tafsiri na matumizi ya taarifa ili kuboresha utoaji wa utabiri zikiwemo tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa wakati na kwa usahihi zaidi.           Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema “Kama mnavyofahamu, kwa sasa dunia inashuhudia ongezeko kubwa la matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotokana na kuchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, ikiwemo mvua kubwa, mafuriko, vipindi virefu vya ukame, pamoja na matukio ya vimbunga na upepo mkali. ...

RAIS SAMIA ANAAHIDI NA KUTEKELEZA "NI MFANO SAHIHI KWETU WASICHANA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa na Wanawake na Mabinti wa Kitanzania kama Kiongozi wa mfano na mwanamke mwenye athari chanya kiasi cha kutoweza kupimika kwa wanawake na mabinti wa Tanzania, Wakimsifu na kumpongeza kwa ujasiri na umahiri wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Kauli hiyo imebainishwa na Bi. Asina Sancho, Kijana na Mjasiriamali wa Kitanzania, akisema Rais Samia amewapa sababu mabinti wengi ya kuamini kuwa wanaweza kufikia malengo yao na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kupambania ndoto zao. "Mama Samia ametutia nguvu sisi mabinti kuamini kuwa tunaweza kusimama na kutimiza ndoto zetu, hata katika nyakati za majaribio, Mama Samia ametupa nguvu ya kuamini hakuna linaloshindikana. Katika imani pia Mhe. Rais amesemwa katika namna nyingi mbaya na bado amekuwa na imani na kuwasamehe waliomkosea licha ya wao waliomkosea kutotaka msamaha." Amesema Bi. Sancho...

NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES IWAFIKIE WATANZANIA WOTE - BALOZI KINGU

Image
*πŸ“ŒUzalishaji wa Rafiki briquettes uende sambamba na uzalishaji wa majiko banifu* *πŸ“ŒSTAMICO waahidi kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati safi nchini* πŸ“Kisarawe - Pwani Watanzania wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi ya kupikia (mkaa mbadala wa Rafiki briquettes) unaozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).  Rai hiyo imetolewa leo Januari 24, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Balozi Jacob Kingu akiwa ameambatana na Wajumbe wa REB na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walipotembelea kiwanda cha Nishati safi ya Rafiki Briquettes kinachomilikiwa na STAMICO kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani. Balozi Kingu amewataka STAMICO kuongeza kasi ya uzalishaji wa mkaa wa Rafiki briquettes ili watanzani wote nchini waweze kutumia nishati safi ya kupikia na salama.  “Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wa...

KANISA LA ACK WAIRIMA LASHAMBULIWA KWA MABOMU, GACHAGUA ANUSURIKA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Makabiliano makubwa yameshuhudiwa katika Kanisa la ACK Wairima, Kaunti ya Nyeri alikokuwa anahudhuria ibada ya leo Jumapili Januari 25, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya Mhe.Rigathi Gachagua Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, Polisi waliokuwa wamefunika nyuso zao wametupa mabomu ya kutoa machozi na kurusha risasi za moto katika kanisa hilo, watu kadhaa wakijeruhiwa huku Gagachua na ujumbe wake wakofanikiwa kutoroka. Hii si mara ya kwanza kwa Naibu huyo wa Rais wa zamani kushambuliwa kanisani ambapo Wiki mbili zilizopita shambulio kama hilo lilitokea nje ya kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) huko Kiamworia, Gatundu Kusini ambapo mafuriko yalitokea baada ya makundi hasimu ya vijana waliokuwa na virungu kuhusika katika vurugu nje ya Kanisa hilo. Kwenye chapisho lake kwenye Mtandao wa X Gagachua amedai kuwa yeye na washirika wake walinaswa ndani ya Kanisa hilo baada ya shambulio hilo kutokana na kile alichokiita Jaribio la m...

𝗠π—ͺπ—˜π—‘π—¬π—˜π—žπ—œπ—§π—œ π—žπ—”π—ͺπ—”π—œπ——π—”: π—‘π—œπ— π—£π—’π—‘π—šπ—˜π—­π—˜ π—₯π—”π—œπ—¦ π——π—žπ—§. π—¦π—”π— π—œπ—” π—žπ—¨π—˜π—‘π——π—˜π—Ÿπ—˜π—” π—žπ—¨π—Ÿπ—˜π—§π—” π— π—”π—˜π—‘π——π—˜π—Ÿπ—˜π—’

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta maendeleo hususani ahadi alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika siku 100 za kwanza za uongozi wake. Ndugu Kawaida akizungumza na maelfu ya wanafunzi wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu mkoani Dodoma leo tarehe 24 Januari 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete. Ametaja baadhi ya yaliyotekelezwa ikiwemo Bima ya Afya kwa wote na ajira kwa vijana zikiwemo za udaktari.

DKT SAMIA: TANZANIA ITAVUKA NA KUSONGA MBELE

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba amesema Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha nchi inakuwa moja na inasonga mbele, baada ya kupita katika changamoto. Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, mtendaji mkuu huyo wa Serikali, amesisitiza tayari kuna utashi wa kisiasa wa kujenga umoja nchini na kwamba jukumu hilo amekabidhiwa yeye. Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo jijini Arusha leo, Jumamosi Januari 24, 2026 alipotoa salamu za Serikali kwa Rais Dkt Samia, aliyemwakilisha katika maziko ya Gavana wa kwanza wa Tanzania, Edwin Mtei. “Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha kwamba nchi inakuwa moja na tunasonga mbele na mimi niwahakikishie tutavuka na tutasonga mbele na heshima ya Tanzania ya mara zote tutakuwa nayo,” amesema. Amesema Rais Dkt Samia angependa kushiriki maziko hayo, lakini wingi wa majukumu umemfanya amtume yeye kumwakilisha na kwamba yaliyozungumzwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini ameyachukua.

MBOWE ATAKA UPINZANI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, KUJENGA UMOJA WA KITAIFA* ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Mwenyekiti wa mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho na vyama vingine vya upinzani kushirikiana na Serikali kuleta umoja wa kitaifa. ‎ ‎Katika kulitekeleza hilo, Mbowe amevitaka vyama vya upinzani kuweka utaratibu wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa katika njia moja ya kuliunganisha Taifa. ‎ ‎Kauli hiyo ya Mbowe inakuja wakati ambao Rais Dkt Samia ameshafanya juhudi mbalimbali zinazolenga kuleta maridhiano ili kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa. ‎ ‎Mbowe ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Januari 24, 2026 alipotoa salamu kwa niaba ya familia ya Mzee wakati wa maziko ya Gavana wa kwanza wa Tanzania, Edwin Mtei yanayofanyika mkoani Arusha. ‎ ‎“Tafuteni namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili katika utaratibu wa kuliunganisha Taifa, kusiwe na taifa la vipande vipande vya vyama vya siasa,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa  ‎ ‎“Tunataka Taifa moja lenye misingi ya maendeleo, lenye upendo, l...