Posts

SIMBACHAWENE AWATAKA VIJANA NA WANAHARAKATI KUTAFUTA NJIA SAHIHI YA KUDAI HAKI

Image
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amewataka Vijana na Wanaharakati kutafuta njia sahihi ya kudai haki ikiwemo mazungumzo mezani akiwaasa kuwa vita na vurugu avijawahi kusaidia bali upelekea kupotea kwa amani huku akitolea mfano wa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo takribani ni zaidi ya miaka thelathini wanaitafuta amani ambayo imepotea. Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Pili unaohusisha Pande Tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani UNHCR ambapo pia walitumia mkutano huo kusaini nyaraka zinazoelezea Mpango wa Urejeshwaji wa Wakimbizi Elfu Themanini na Sita na Mia Mbili Hamsini na Sita waliopo hapa nchini ambapo pia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Shabani Bihango na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani nchini Tanzania,Barbara Dotse waliishukuru Tanzania kwa kuhifadhi wakimbizi hao kwa muda unaozidi miaka thelathini.

TUFUATE TARATIBU ILI KUDUMISHA AMANI YETU- MALECHA

Image
Khalid Malecha, Mkazi wa Kitonga Jijini Dar Es Salaam, ameeleza kuwa maelfu ya wananchi waliathirika moja kwa moja na ghasia na matukio ya uvunjifu wa amani uliojitokeza Oktoba 29, 2025, akihamasisha Jamii kuienzi amani ya Tanzania na kufuata taratibu rasmi za maandamano. Malecha amebainisha hayo leo Alhamisi Disemba 04, 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, akionesha pia kusikitishwa na waliofanya vurugu hizo kukosa sababu za msingi za kufanya hivyo. "Tuangalie zaidi amani tuliyo nayo katika nchi yetu kwasababu tuna mengi tunayotaka kuyafanya kwente maisha yetu hususani Vijana wenzangu ikiwemo malengo tuliyonayo kwani fursa zipo nyingi ambazo Rais wetu ametuwekea." Amesema Bw. Malecha. Malecha amezungumzia pia matarajio yake katika Wizara mpya ya maendeleo ya Vijana, akisema anaamini kupitia Wizara hiyo Vijana watazifahamu fursa nyingi zaidi za kiuchumi na ajira, suala ambalo litawatoa Vijana katika hatua moja kuelekea nyingine katika ukuaji wa uchumi.

TUTUMIE NJIA YA MAJADILIANO KUONDOA TOFAUTI ZA KIJAMII

Image
Abdulkarim Mohamed, Mkazi wa Dar Es Salaam amesema kufanya vurugu kama sehemu ya kushinikiza serikali kutoa haki ama huduma fulani kwa jamii hakuna faida yoyote na badala yake vurugu zimekuwa sababu ya anguko la kiuchumi na kukwama kwa shughuli za kijamii na kiuchumi. Mohamed amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uzoefu na athari ya kiuchumi na kijamii aliyoipata wakati wa vurugu na matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akilaani wale wote walioratibu na kushiriki katika matukio hayo ya uvunjifu wa amani. "Kwa mimi binafsi siliungi Mkono, sisi Tanzania tumezoea kuwa ni nchi ya amani na hao waliopanga jambo hili mapema kulingana na kauli zao hatukuamini kama jambo lile lingetokea na bado mpaka sasa tuna mashaka ikiwa kweli walikuwa ni Watanzania waliofanya matukio haya." Amesema Bw. Mohamed. Kadhalika Bw. Mohamed amehimiza pia kufuatwa kwa taratibu rasmi zinazokubalika kisheria na kijamii ikiwa baadhi ya ...

ELIMU YA MBOLEA YAONGEZA TIJA KILIMO CHA PAMBA SIMIYU*

Image
Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Godwin Vedastus akitoa elimu ya mbolea kwa wakulima wa kijijichi Bukangilija kilichopo Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu leo tarehe 3 Desemba,2025. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Kilimo, Idara ya Maendeleo ya Mazao Samson Poneja walipotembelea ofisini kwake kueleza uwepo wao mkoani humo kutekeleza kampeni ya Mali Shambani tarehe 3 Desemba, 2025 Wakulima wa kijiji cha Hinduki kilichopo Halmshauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani wa Simiyu wakifuatilia mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea tarehe 3 Desemba, 2025 ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Mali Shambani yenye lengo la kutoa elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo, kuhamasisha wakulima kupima afya ya udongo na kujisajili kwenye mfumo wa pembejeo za kilimo ili kunufaika na ruzuku ya mbolea na mbegu inayotolewa na Serikali. Diwani wa Kata ya Sukuma Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Mary Sagana Misangu...

TWIGA STARS YAKABIDHIWA TSH MILIONI 50

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amekabidhi Shilingi Milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kama pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufuzu mara mbili mfululizo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Desemba 3, 2025 jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Serikali kutambua juhudi na nidhamu ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi katika safari yao ya kufuzu michuano hiyo mikubwa barani Afrika, inayotarajiwa kufanyika Morocco mwaka 2026.

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

KINACHOHAMASISHWA DISEMBA 09 SI MAANDAMANO YA AMANI- POLISI

Image
Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na usalama limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu yanayoendelea kwenye Mitandao ya Kijamii na kwenye makundi sogozi wakihamasisha wanayoyaita maandamano ya amani yasiyo na kikomo ya Disemba 09, 2025. Polisi pia imeeleza katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari leo Jumatano Disemba 03, 2025 kuwa linaendelea kuzuia uhalifu sambamba na kuwakamata wale wanaofanya makosa mbalimbali ikiwemo ya Kimtandao kwa wale wanaoendesha makundi mbalimbali katika Mitandao ya kijamii ya kuhamasisha uhalifu na kuwachukulia hatua kulingana na sheria za nchi. Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime katika taarifa hiyo amelaani pia kile kinachoelezwa katika makundi hayo ya mitandao ya Kijamii ikiwemo wito wa kutoshika silaha katika maandamano hayo ikiwa mwandamanaji hakupitia mafunzo na badala yake waaachie silaha wenye mafunzo. "Kupitia Mitandao na Klabu mbalimbali za Mtandaoni wanahamasishana pia kusiwe na shughuli nying...