Posts

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA MAAFISA DAWATI NGAZI YA MIKOA NA HALMASHAURI

Image
📌 *Lengo ni kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.* 📌 *Mafunzo kuhusisha mikoa 26 na Halmashauri zake.* Wizara ya Nishati imeanza kutoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia kwa Maafisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia ngazi ya mikoa na halmashauri kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na kuwawezesha Maafisa Dawati kutambua majukumu yao katika utekelezaji wa mkakati.. Akifungua mafunzo hayo, wilayani Kibaha mkoani Pwani, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Hadija Mruma ameipongeza Wizara ya Nishati kwa jitihada mbalimbali inazochukua kwa vitendo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini mojawapo ikiwa ni kuhakikisha elimu na vifaa vya nishati safi ya kupikia vinafika hadi ngazi za Mikoa, Halmashauri na Vijiji. Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachi wanatumia nishati safi ya kup...

WANABUKOMBE SITAWAANGUSHA, NINA DENI KUBWA KWENU - DKT. BITEKO

Image
Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapunduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko amewashukuru wana Bukombe kwa heshima waliyompa kipindi chote Cha kampeni Katika wilaya ya Bukombe. Dkt. Biteko ametoa shukurani hizo Oktoba 27, 2025 wakati wa kuhitimisha kampeni Katika Uwanja wa Igulwa, Wilayani Bukombe, Mkoani Geita. "Nataka niwaambie wana Bukombe huwa mnanipa deni kubwa sana moyoni mwangu hamjui tu, huwa hamjui huwa najiona mmenipa stahili nisiyostahili kwa sababu kama binadamu nina mapungufu yangu mengi lakini mnanipa heshima"- amesema Biteko. Dkt. Biteko amewashukuru pia vijana wa hamasa na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali. "Nitafanya kila linalowezekana vijana wa hamasa wasiishie Kwenye kampeni ni vijana wetu lazima tuwakomboe. Nataka niwaambie kila wakati tukiwaita mnakuja mnanipa deni na heshima kubwa sana" Aidha Dkt. Biteko amewakumbusha wana Bukombe Kuwa leo ilikuwa siku ya kuhitimisha kampeni katika jimbo la Bukombe na tarehe 29 wajiyoke...

NGORONGORO DELIVERS LIFELINE TO KAKESIO WARD WITH NEW WATER PROJECT

Image
Residents of Kakesio Ward, located in the Ngorongoro Division of Ngorongoro District, Arusha Region, are set to benefit from a new water project aimed at providing clean water for both livestock and domestic use. The Government, through the Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA), has drilled a 110-metre-deep borehole expected to produce up to 80,000 litres of water per day. This initiative is part of the government’s continued efforts to improve the wellbeing of communities living within the Ngorongoro Conservation Area. Similar projects have already been completed in the Mount Matiti area, serving residents of Endulen and Laetoli Wards. A similar project will soon be implemented in Olbalbal Ward to help address persistent water shortages for livestock and human needs throughout the year.

JAMBO BAYA LISIKUMBATIWE- MUFTI ZUBEIR

Image
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesisitiza umuhimu wa kutanguliza amani na maslahi ya wengi mbele katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu na hata baada ya zoezi hilo kukamilika, akisisitiza umuhimu wa kutokumbatia jambo baya hasa kwa kutazama mifano dhahiri ya yale yanayoendelea katika Mataifa ya jirani na yale yenye ukosefu wa amani. Mufti Zubeir amesisitiza hayo leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 wakati wa Kongamano na Viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali Jijini Dar Es Salaam akirejea mfano wa hadithi za Haruni katika enzi za Musa katika Maandiko ya dini na namna ambavyo Mungu alimuangamiza Mtu huyo mara baada ya kukaidi maagizo na maonyo ya watu wake wakaribu waliokuwa wakimtaka kutenda wema na kuacha kuichafua nchi yake kutokana na tabia zake. "Mwenyenzi Mungu anasema ana wivu zaidi kuliko sisi, wivu wa Mungu hataki kuona kiumbe chake kinadhulumiwa, watu wanaharibu amani ama watu wanaharibu nchi. Ipo ibada ya Hijja kwenye nguzo za uislamu, kila mmoja huwa...

TUKISEMA UKWELI WANATUITA MACHAWA- SHEIKH KISHKI

Image
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Al- Hikma Islamic Foundation Sheikh Nurdin Kishki amesema wajibu wa viongozi wa dini kote nchini ni kusimamia Amani na mshikamano wa jamii pamoja na kuonya wananchi wasikubali kutumika kwa maslahi binafsi ya watu wanaotaka kuvuruga mshikamano na amani ya Tanzania. Sheikh Kishki ameyasema haya Leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 kwenye kongamano la viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali lililofanyika jijini Dar es Salaam, Ajenda kuu ikiwa ni kuilinda na kuitunza amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025. Kishki amezungumzia pia tabia iliyozuka nchini kwa baadhi ya watu wanaowakebehi na kuwasema Viongozi wanaosema mema ya nchi na kuelekeza kuhusu amani na mshikamano wa Watanzania kwa madai kuwa wanafanya hivyo kutokana na kuwa wanalipwa fedha na Mamlaka. "Siku hizi ukisimama kulitetea Taifa lako unaambiwa chawa umepewa bahasha na mimi nauliza ninyi mliosimama mstari wa mbele kutaka kutoboa jahazi la MV Tanzania, kut...

CWT YAWAHAKIKISHIA WATANZANIA USHIRIKI WA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025

Image
Chama cha waalimu nchini Tanzania CWT kimewataka waalimu kote nchini kuendelea na msimamo wao wa kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba, 2025 kwenda kupiga kura kwani ndiyo msimamo wa Chama ambao ulikwisha tolewa na Msemaji wa Chama hicho ambaye ni Rais wa Chama Cha waalimu nchini Tanzania Bw. Suleiman Ikomba. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Joseph Misalaba kwenda kwa Makatibu wa CWT, Mikoa na Wilaya imesisitiza waalimu pia na umma kwa ujumla kuwa Mabalozi wazuri wa Upendo, amani, umoja na mshikamano kwaajili ya maendeleo thabiti ya Tanzania kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye, wakiishukuru pia serikali kwa kuendelea kutatua kero za waalimu kwa kushirikiana na CWT. Taarifa ya Katibu Mkuu wa CWT imekuja baada ya kuzuka kwa uvumi mitandaoni zikieleza kuwa Chama Cha Waalimu kimesusia uchaguzi Mkuu wa Keshokutwa Jumatano, ambapo Mwalimu Misalaba amekanusha taarifa hizo na akitaka Watanzania wazipuuzie. "Chama Cha Waalimu Tanzania kinapenda kukanusha kwa nguvu zote...