BODI YA TMA YAFANYA ZIARA YA KIKAZI RADA YA HALI YA HEWA BANGULO, PUGU NA KITUO CHA HALI YA HEWA JNIA
Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya ziara ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Mamlaka katika kituo cha Rada ya Hali ya Hewa, Bangulo, Pugu na Ofisi za TMA zilizopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 23 Julai 2025. Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari na Makamu Mwenyekiti, Dkt. Emmanuel Mpeta.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Jaji Mshibe alisema lengo la ziara ni kukagua na kutathmini usimamzi na utendaji kazi wa miundombinu ya TMA na kutathmini utekelezaji wa Maagizo na Maelekezo ya Bodi katika kuboresha huduma na pia kutambua changamoto zilizopo, na kuona Taasisi ilipo na inapoelekea. “Bodi imekuwa ikitoa maelekezo hivyo leo ilikuwa ni siku maalum kuangalia utekelezaji wake”.Alisema Jaji Mshibe. Alisisitiza kuwa TMA ya sasa imepiga hatua kubwa katika uboreshaji wa miundombinu ya utoaji huduma. Aidha, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka kwa...