Posts

Showing posts from February, 2026

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO LA MWENYEKITI WA CCM ALIYEKUTWA AMEKUFA

Image
Kupitia mitandao ya kijamii kunasambazwa picha mjongeo akionekana mtu mmoja mwanaume ambaye anajinasibu kuhusika katika tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Itumbi aitwaye Elia Richard Sambala, miaka 53, mkazi wa Itumbi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Ukweli ni kwamba, Februari 11,2026 saa 7 mchana katika Kijiji cha Itumbi, Elia Richard Sambala, alikutwa shambani kwake akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye makali kichwani na watu wasiojulikana na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa matibabu. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, kupitia Askari wa kuchunguza matukio ya mauaji, walianza msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kuhusiana na tukio hilo na ufuatiliaji zaidi kwa wengine waliohusika unaendelea. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa masilahi wa eneo la uchimbaji madini ya dhahabu ambapo mmoja wa wanafamilia hao alikodisha kwa wawekezaji raia wa Chin...

JESHI LA POLISI KUENDELEA KUWEKA JITIHADA ZA KUNUNUA MBWA WAPYA WA KISASA WENYE UWEZO WA KUBAINI,KUZUIA NA KUMDHOOFISHA MHALIFU.

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuweka jitihada mbalimbali za kununua mbwa wapya wa kisasa na wenye uwezo ili kuboresha muonekano wa mbwa wa Polisi mwenye umbo lenye kumdhoofisha mhalifu. IGP Wambura, ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Kikosi cha Mbwa na farasi wa Mikoa na Wataalam Waongoza Mbwa na Farasi kikao kilichofanyika jijini Dar es salaam Februari 9,2026 huku akiweka msisitizo kwenye eneo la utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwatumia Wanyama kazi katika kudhibiti uhalifu kwenye maeneo yao. Akizungumza na Watendaji hao IGP Wambura, amebainisha kuwa, Kikosi hicho kina umuhimu mkubwa kiusalama kwa kuwa Doria za mipakani na maeneo mengine muhimu hulazimika kutumia mbwa na farasi kwani ni rahisi kupenya kwenye maeneo ambayo gari haliwezi kupita kwa urahisi. Amesema, Jeshi la Polisi lina Mbwa na Farasi wanaofanya kazi katika bandari, viwanja vya ndege na mipakani kwa lengo la kuzuia biashara...

UPENDO NA MAELEWANO VYATAJWA KUWA MSINGI WA AMANI NCHINI

Image
Adam Seleman, Mkazi wa Msongora Jijini Dar Es Salaam amesema tafsiri halisi ya amani ni pamoja na kuelewana na kupendana miongoni mwa Watanzania, akihimiza upendo na maelewano kama msingi wa kudumisha amani na utulivu nchini. Bw. Selemani amebainisha hayo leo Jumamosi Februari 07, 2026 wakati akizungumza na mwandishi wetu wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa ustawi na maendeleo, akisema familia, Jamii na Nchi yoyote inahitaji amani na utulivu ili kuweza kutimiza majukumu na wajibu walionao. "Maana halisi ya amani ni ile hali ya mtu kuwa na uhuru wa kufanya jambo ambalo linaruhusiwa Kikatiba na pia amani tafsiri yake ni upendo, tukipendana ndio amani yenyewe kuanzia ndani ya nyumba. Nawaomba sana tuendelee kushikamana na kudumisha hiki tulichonacho kwani sisi nchi yetu ni kisiwa cha amani." Amesema Bw. Selemani.

AMANI INATUPA UHURU WA KUJIENDELEZA KIUCHUMI- NIACHIENI

Image
Uwepo wa amani katika Taifa kumetajwa kama miongoni mwa rasilimali muhimu zinazohitajika ili kufanikisha malengo na mipango ya mtu mmoja mmoja, Familia, Jamii na Taifa kwa ujumla, Wito ukitolewa kwa Watanzania kuilinda na kudumisha amani. Kauli hiyo imetolewa na Bw. Ramadhan Mohamed Niachieni, Mkazi wa Mtaa wa Mkera, Kata ya Msongora Jijini Dar Es Salaam, akisisitiza kuwa amani ndiyo yenye kuleta maendeleo nchini hivyo kila mmoja anawajibika kuilinda kwa ustawi na maendeleo yetu binafsi. "Amani ina tija sana katika nchi yetu ikiwemo maendeleo ya kila hali kutokana na uhuru wa kufanya shughuli zetu za kiuchumi. Naomba sana tuilinde ili tusiharibikiwe kama wengine na ili tupate fursa ya kuijenga nchi yetu." Amesema Bw. Niachieni. Mwananchi huyo anaungana na maelfu ya wananchi wengine ambao wamekuwa wakisisitiza kuhusu ulinzi wa amani na kuwakataa wote wenye kuhatarisha amani nchini, wakirejea athari za kiuchumi na kijamii zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktob...

WITO WATOLEWA, JITIHADA ZA PAMOJA UDHIBITI WA SILAHA HARAMU NCHINI

Image
Kamati ya udhibiti na usimamizi wa silaha imetakiwa kujikita katika utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya silaha haramu ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya silaha haramu. Kauli hiyo imetolewa wakati wa ufungaji wa kikao cha kwanza cha mafunzo cha kamati ya udhibiti na usimamizi wa silaha, kilichofanyika kwa siku tatu Jijini Dar Es Salaam, wajumbe wakikubaliana kuwa ikiwa elimu itatolewa na jamii ikaelewa madhara ya kusambaa kwa silaha haramu, nchi itakuwa salama. Mapema akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, IGP Camillus Wambura amesema wajumbe wa kamati hiyo ni watu makini na wameonesha kuwa watakuwa msaada mkubwa katika kutekeleza majukumu yao kutokana na kuwa wabobezi katika nyanja tofauti kutoka Serikalini na sekta binafsi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini na Mrajisi Mkuu wa Silaha DCI Ramadhan Kingai alisema wataendelea kuchukua hatua kali kwa wamiliki wa silaha ambao wamekuwa wakikiuka taratibu z...