Posts

Showing posts from January, 2026

POLISI NJOMBE WAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI KUCHOMWA MOTO NA KUPORWA SILAHA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari limekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa katika Mitandao ya Kijamii nchini zikiambatana na picha mjongeo (Video), zikieleza uwepo wa Askari Polisi wa Mkoa huo aliyechomwa moto na kisha kuporwa silaha Mkoani humo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Banga, Januari 28, 2026 amesema kuwa katika Mkoa wa Njombe hakuna tukio kama hilo, akionya dhidi ya wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji. "Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla." Amesema Kamanda Banga. Polisi pia imesema inaendelea kumfuatilia mtu ama watu waliochukua na kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo a...

MWANACHAMA WA CHADEMA ARUSHA MATATANI KWA KUIBA 'FEDHA ZA LISSU'

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumkamata Bw. Fredrick Mbwambo, Mwanachama wa Chadema na Mkazi wa Arusha kwa tuhuma za wizi wa fedha ambazo alikuwa amezikusanya kutoka kwa wananchi waliokuwa wamechanga kwaajili ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu kupitia Kampeni yao ya "Funga mwaka na Tundu Lissu". Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo leo Jumatano Januari 28, 2026 Jijini Arusha mbele ya wanahabari, amesema ukamataji wa mtuhumiwa huyo umefanyika baada ya Polisi kupokea malalamiko kutoka kwa Bw. Alute Mughwai, aliyeeleza kubaini wizi wa fedha zilizokuwa zimechangwa. "Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishwa kwenye namba mbili za simu, moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ikiwa ni ya kampuni ya simu ya nchi jirani." Amesema Kamanda Masej...

RADA ZA HALI YA HEWA NI MUHIMU KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NCHINI.

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliandaa warsha ya mafunzo ya Rada za Hali ya Hewa na matumizi ya taarifa zinazotokana na Rada, tarehe 26-27 Januari 2026, Dodoma. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiufundi katika matumizi ya teknolojia Rada, hususan katika uchambuzi, tafsiri na matumizi ya taarifa ili kuboresha utoaji wa utabiri zikiwemo tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa wakati na kwa usahihi zaidi.           Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema “Kama mnavyofahamu, kwa sasa dunia inashuhudia ongezeko kubwa la matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotokana na kuchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, ikiwemo mvua kubwa, mafuriko, vipindi virefu vya ukame, pamoja na matukio ya vimbunga na upepo mkali. ...

RAIS SAMIA ANAAHIDI NA KUTEKELEZA "NI MFANO SAHIHI KWETU WASICHANA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa na Wanawake na Mabinti wa Kitanzania kama Kiongozi wa mfano na mwanamke mwenye athari chanya kiasi cha kutoweza kupimika kwa wanawake na mabinti wa Tanzania, Wakimsifu na kumpongeza kwa ujasiri na umahiri wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Kauli hiyo imebainishwa na Bi. Asina Sancho, Kijana na Mjasiriamali wa Kitanzania, akisema Rais Samia amewapa sababu mabinti wengi ya kuamini kuwa wanaweza kufikia malengo yao na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kupambania ndoto zao. "Mama Samia ametutia nguvu sisi mabinti kuamini kuwa tunaweza kusimama na kutimiza ndoto zetu, hata katika nyakati za majaribio, Mama Samia ametupa nguvu ya kuamini hakuna linaloshindikana. Katika imani pia Mhe. Rais amesemwa katika namna nyingi mbaya na bado amekuwa na imani na kuwasamehe waliomkosea licha ya wao waliomkosea kutotaka msamaha." Amesema Bi. Sancho...

NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES IWAFIKIE WATANZANIA WOTE - BALOZI KINGU

Image
*📌Uzalishaji wa Rafiki briquettes uende sambamba na uzalishaji wa majiko banifu* *📌STAMICO waahidi kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati safi nchini* 📍Kisarawe - Pwani Watanzania wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi ya kupikia (mkaa mbadala wa Rafiki briquettes) unaozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).  Rai hiyo imetolewa leo Januari 24, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Balozi Jacob Kingu akiwa ameambatana na Wajumbe wa REB na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walipotembelea kiwanda cha Nishati safi ya Rafiki Briquettes kinachomilikiwa na STAMICO kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani. Balozi Kingu amewataka STAMICO kuongeza kasi ya uzalishaji wa mkaa wa Rafiki briquettes ili watanzani wote nchini waweze kutumia nishati safi ya kupikia na salama.  “Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wa...

KANISA LA ACK WAIRIMA LASHAMBULIWA KWA MABOMU, GACHAGUA ANUSURIKA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Makabiliano makubwa yameshuhudiwa katika Kanisa la ACK Wairima, Kaunti ya Nyeri alikokuwa anahudhuria ibada ya leo Jumapili Januari 25, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya Mhe.Rigathi Gachagua Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, Polisi waliokuwa wamefunika nyuso zao wametupa mabomu ya kutoa machozi na kurusha risasi za moto katika kanisa hilo, watu kadhaa wakijeruhiwa huku Gagachua na ujumbe wake wakofanikiwa kutoroka. Hii si mara ya kwanza kwa Naibu huyo wa Rais wa zamani kushambuliwa kanisani ambapo Wiki mbili zilizopita shambulio kama hilo lilitokea nje ya kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) huko Kiamworia, Gatundu Kusini ambapo mafuriko yalitokea baada ya makundi hasimu ya vijana waliokuwa na virungu kuhusika katika vurugu nje ya Kanisa hilo. Kwenye chapisho lake kwenye Mtandao wa X Gagachua amedai kuwa yeye na washirika wake walinaswa ndani ya Kanisa hilo baada ya shambulio hilo kutokana na kile alichokiita Jaribio la m...

𝗠𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘𝗞𝗜𝗧𝗜 𝗞𝗔𝗪𝗔𝗜𝗗𝗔: 𝗡𝗜𝗠𝗣𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗘 𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗨𝗟𝗘𝗧𝗔 𝗠𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗢

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta maendeleo hususani ahadi alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika siku 100 za kwanza za uongozi wake. Ndugu Kawaida akizungumza na maelfu ya wanafunzi wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu mkoani Dodoma leo tarehe 24 Januari 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete. Ametaja baadhi ya yaliyotekelezwa ikiwemo Bima ya Afya kwa wote na ajira kwa vijana zikiwemo za udaktari.

DKT SAMIA: TANZANIA ITAVUKA NA KUSONGA MBELE

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba amesema Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha nchi inakuwa moja na inasonga mbele, baada ya kupita katika changamoto. Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, mtendaji mkuu huyo wa Serikali, amesisitiza tayari kuna utashi wa kisiasa wa kujenga umoja nchini na kwamba jukumu hilo amekabidhiwa yeye. Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo jijini Arusha leo, Jumamosi Januari 24, 2026 alipotoa salamu za Serikali kwa Rais Dkt Samia, aliyemwakilisha katika maziko ya Gavana wa kwanza wa Tanzania, Edwin Mtei. “Serikali haitakuwa kikwazo cha kuhakikisha kwamba nchi inakuwa moja na tunasonga mbele na mimi niwahakikishie tutavuka na tutasonga mbele na heshima ya Tanzania ya mara zote tutakuwa nayo,” amesema. Amesema Rais Dkt Samia angependa kushiriki maziko hayo, lakini wingi wa majukumu umemfanya amtume yeye kumwakilisha na kwamba yaliyozungumzwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini ameyachukua.

MBOWE ATAKA UPINZANI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, KUJENGA UMOJA WA KITAIFA* ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Mwenyekiti wa mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewataka viongozi wa chama hicho na vyama vingine vya upinzani kushirikiana na Serikali kuleta umoja wa kitaifa. ‎ ‎Katika kulitekeleza hilo, Mbowe amevitaka vyama vya upinzani kuweka utaratibu wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa katika njia moja ya kuliunganisha Taifa. ‎ ‎Kauli hiyo ya Mbowe inakuja wakati ambao Rais Dkt Samia ameshafanya juhudi mbalimbali zinazolenga kuleta maridhiano ili kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa. ‎ ‎Mbowe ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Januari 24, 2026 alipotoa salamu kwa niaba ya familia ya Mzee wakati wa maziko ya Gavana wa kwanza wa Tanzania, Edwin Mtei yanayofanyika mkoani Arusha. ‎ ‎“Tafuteni namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili katika utaratibu wa kuliunganisha Taifa, kusiwe na taifa la vipande vipande vya vyama vya siasa,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa  ‎ ‎“Tunataka Taifa moja lenye misingi ya maendeleo, lenye upendo, l...

DKT. SAMIA AAGIZA HAYA KUMUENZI MTEI

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara ya njia nne ya Tengeru hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kumuenzi Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Edwin Mtei. ‎ ‎Katika hatua hiyo ya kumuenzi Mtei, mkuu huyo wa nchi ameagiza hadi Februari 20, mwaka huu maeneo yote korofi yarekebishwe kuwaondolea wananchi shida na kuleta maendeleo kama alivyotaka marehemu Mtei. ‎ ‎Maelekezo hayo yametolewa na Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Rais Dkt Samia, jijini Arusha leo, Jumamosi Januari 24, 2026 wakati wa salamu za mwisho kwa Gavana wa kwanza wa Tanzania, Mtei. ‎ ‎Ameitaka Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kukamilisha kazi hiyo kwa haraka kama alama kwa Mtei aliyeitumikia nchi kwa uadilifu, heshima na kiu ya maendeleo. ‎ ‎Pia, ameagiza katika Shamba la Mringa Estate ambako mchakato ulielekeza baadhi ya wananchi wanufaike ni muhimu wahusika wote wanaostahili wa...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

WADAU WAJENGEWA UELEWA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA ZINAZOTOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Image
Dodoma Wadau kutoka sekta mbalimbali wamejengewa uelewa wa huduma za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia warsha ya siku mbili iliyofanyika katika Hoteli ya Best Western, Dodoma. Warsha hiyo ilifunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, tarehe 22 Januari ambapo alisema warsha hiyo inalenga kuimarisha matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta zote za kiuchumi na kijamii, na hivyo kuongeza ufanisi na tija katika shughuli hizo. Katika warsha hiyo, wataalamu wa TMA waliwasilisha na kutoa ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na TMA, ikiwemo utabiri wa kila siku na tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa. Wataalamu walianisha pia matakwa ya kisheria kwa WADAU kutumia na kuzingatia taarifa za hali ya hewa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo katika sekta ya Ujenzi, usafir...

WATENDAJI WA UCHAGUZI PERAMIHO WATAKIWA KUVISHIRIKISHA VYAMA VYA SIASA

Image
 Na. Mwandishi WETU, Iringa Watendaji wa uchaguzi wametakiwa kuvishirikisha kwa ukaribu vyama vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi katika maeneo yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe. Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Kata ya Shiwinga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Februari, 2026. “Wakati wote wa mchakato wa uchaguzi huu, ni vema mkavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yenu kuhusu masuala ya kiu...

DK. HOMERA AWEKA MSINGI WA MOTISHA KWA WATUMISHI NAMTUMBO*

Image
- Ataf­siri maono ya Rais Samia kwa vitendo akitoa magodoro 222 - asema motisha ni nguzo ya huduma bora kwa wananchi Na. Mwandishi wetu, NAMTUMBO.  Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Dkt. Juma Zuberi Homera, ameendelea kutafsiri kwa vitendo maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ya kuwajengea motisha na mazingira bora ya kazi watumishi wapya, baada ya kukabidhi magodoro 222 kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, hatua inayolenga kuinua morali na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi. Magodoro hayo yamegawanywa kwa mpangilio mahsusi ambapo 202 kwa watumishi walioajiriwa tayari, 13 kwa watumishi wanaotarajiwa kuajiriwa, na 7 kama akiba.  Makabidhiano yamefanyika tarehe 23 Januari 2026 katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Akizungumza mbele ya viongozi wa Serikali na Chama, Dkt. Homera amesema motisha kwa watumishi si hisani bali ni mkakati wa maendeleo, akisisitiza kuwa ajira mpya na usta...

UZINDUZI WA MELI YA MV NEW MWANZA NI UTEKELEZAJI WA MAONO YA RAIS SAMIA- MWIGULU

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuzinduliwa kwa Meli mpya ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Kusini leo Ijumaa Januari 23, 2026 ni dhihirisho la kuendelea kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kunakofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyoahidi kwa wananchi. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amebainisha hayo muda mfupo baada ya kuzindua meli hiyo, akieleza kuwa kuzinduliwa kwa usafiri huo ni tukio lenye kuonesha pia uwezo wa nchi katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo. "Tukio hili tunalolifanya leo la uzinduzi wa meli hii kubwa ni tukio linaloonesha uwezo wetu katika kutekeleza miradi ya maendeleo, linaelezea uwezo wa Kiongozi wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza maono makubwa yanayoweza kuwaletea Watanzania maendeleo." Amesisitiza Dkt. Mwigulu. Meli hiyo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu imejengwa na Mkandarasi kutoka Korea aitwaye Gas Entec Ship-building kwa kushirikiana na TASHICO, ikitengene...

AMANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO NA USTAWI WETU, TUILINDE- MWIGULU

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kudumisha amani ya Tanzania, akisema amani ndio msingi wa maendeleo na ustawi wa jamii. ‎ ‎Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 23, 2026 wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa Meli mpya na ya kisasa ya MV New Mwanza, kwenye Bandari ya Kusini, akisema hata maendeleo binafsi ya kila mwananchi yanategemea utulivu na amani. ‎ ‎"Yote tunayoyasema hayawezi kutekelezeka kama hakuna amani, hata shughuli zako wewe mmoja mmoja huwezi kuzitekeleza kama hakuna amani katika eneo lako. Mnufaika namba moja wa amani ni wewe mwenyewe." Amesema Mhe. Waziri Mkuu. ‎ ‎Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amesisitiza pia umuhimu wa kulinda umoja, utaifa na undugu tuliourithi kutoka kwa watangulizi waliokuwepo, akisema kote duniani amani imekuwa msingi wa mafanikio na ustawi wa wananchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

RAIS SAMIA NI MSIKIVU, ANASHUGHULIKIA MAHITAJI YETU- KIRUMBA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Vijana nchini Tanzania wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa za maendeleo zinazoendelea kupigwa kote nchini, pamoja na serikali yake kuwa sikivu katika kusikiliza na kufanyia kazi changamoto za wananchi hususani katika huduma za kijamii nchini. ‎ ‎Akizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Ijumaa Januari 23, 2026, Bw. Denis Kirumba mkazi wa Tabata, Dar Es Salaam ameeleza matokeo chanya ya kuundwa kwa wizara ya maendeleo ya Vijana, akisema Wizara hiyo imemsaidia kutambua fursa mbalimbali za Vijana pamoja na kupata elimu ya namna ya kuweza kuwa mnufaika wake. ‎ ‎"Tunamshukuru sana Rais kwa kuunda Wizara hii ya Vijana kwani inasikiliza kero zetu, inatupa fursa mbalimbali na pia inatuelekeza kuhusu Mikopo na namna ya kuwa wajasiriamali."amesema Bw. Kirumba. ‎ ‎Kirumba pia ameeleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara za lami katika Mitaa mbalimbali, utatuzi wa kero za maji katika maeneo mengi nch...

WAJASIRIAMALI TARIME WAMSHUKURU RAIS SAMIA UJENZI WA SOKO LA KISASA ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Wajasiriamali wa Soko kuu la Tarime Mkoani Mara lililogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 9.6 kutoka serikali kuu, wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa soko hilo, wakisema kwasasa wanafanya biashara zao katika mazingira salama, sahihi na tulivu, tofauti na ilivyokuwa hapo awali, suala linalowawezesha kupata faida zaidi katika Biashara zao. ‎ ‎Akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali wengine leo Ijumaa Januari 23, 2026, Mjasiriamali Rebecca William amesema hakuwahi kutegemea kuwa Tarime wangepata soko kubwa na la kisasa kama hilo, akimuombea kheri na maisha marefu Rais Samia ili aweze kuwapelekea miradi mingine mingi zaidi ya maendeleo katika Wilaya yao. ‎ ‎"Nimefanya kazi kwenye soko hili kwa miaka minne, leo tunampongeza Rais Samia kwa kutujengea soko hili la kisasa na la Kimataifa, Mungu amlinde sana maana sisi Wakurya hatukuwahi kuota kuwa na soko kama hili lakini leo tumepata. Mama Samia hongera sana, Mungu akubariki." Amese...

‎MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA VIJIJINI MATATANI KWA UCHOCHEZI ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetangaza kumkamata na kumshikilia Bi. Getruda Japhet Lengesela, Mkazi wa Nsalala- Mbalizi na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Wilaya ya Mbeya Vijijini. ‎ ‎Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Ijumaa Januari 23, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Benjamin Kuzaga imesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana Januari 22, 2026 saa tatu usiku eneo la Nsalala, Mji mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwa ni pamoja na uchochezi. ‎ ‎Kulingana na Polisi, upelelezi unakamilishwa na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake mara baada ya upelelezi kukamilika

RAIA WA NAIGERIA MIAKA 28 KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

Image
  Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Mahakama Kuu ya Uhujumu Uchumi, Divisheni ya Makosa ya Rushwa, imemhukumu kifungo cha miaka 28 jela mshtakiwa David Kanayo Chukwu, raia wa Nigeria, ambaye ni mshtakiwa wa kwanza kati ya watatu, baada ya kukiri kosa la kushiriki katika kusafirisha kilogramu 268.50 za dawa za kulevya aina ya heroin. Akisoma hukumu hiyo tarehe 22 Januari, 2026, Mheshimiwa Hakimu Otaru Joachimu alisema kuwa mahakama imezingatia miaka 5 na miezi 9 aliyokaa gerezani mshtakiwa huyo tangu alipokamatwa. Hivyo basi, atatumikia kifungo cha miaka 22 na miezi mitatu iliyobaki ili kukamilisha adhabu yake. Aidha, mahakama hiyo imemuondolea mashtaka Alistair Amon Mbele, ambaye ni mshtakiwa wa tatu, baada ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha hatia dhidi yake katika shauri namba DCEA/IR/06/2020 ECO 36/2020 linalowahusu David Kanayo Chukwu (raia wa Nigeria), Isso Lomward Lupembe (Mtanzania), na Alistair Amon Mbele (Mtanzania). Kwa upande wa mshtakiwa wa pili, Isso Lomward Lupembe, ke...

‎WATUHUMIWA WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA ‎

Image
  Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  WATUHUMIWA wawili, Amasha Iddi Mrisho (40), mkazi wa Buza, Dar es Salaam na Seleman Juma Ally (32), raia wa Msumbiji, Januari 22, 2026, wamefikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke kujibu tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya skanka. Akisoma maelezo ya awali ya shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Lukosi, Mwendesha Mashtaka wa Serikali Wakili Nicas Kihembe akisaidiana na Erick alidai kuwa washtakiwa hao walikamatwa tarehe 08 Desemba 2025 katika mtaa wa Wailes, Temeke, Dar es Salaam, na maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, wakati wa operesheni hiyo, DCEA ilikamata pakiti 20 za Bangi aina ya skanka zenye uzito wa jumla wa kilogramu 20.03, ambazo zilikuwa zimefichwa ndani ya balo la mitumba, kisha kufichwa katika basi aina ya Scania la kampuni ya King Masai Tours, lenye namba za usajili wa Msumbiji A...

TUTACHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA TAARIFA BINAFSI ZA WATU KINYEMELA- PDPC ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎Tume ya taarifa ya ulinzi wa Taarifa binafsi Tanzania PDPC imetangaza kuanza mara moja kwa ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria kwa Taasisi za umma na za binafsi, zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi. ‎ ‎Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 22, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt. Emmanuel Mkilia amesema zoezi hilo linafanyika mara baada ya muda wa hiari kuisha kulingana na tangazo la Tume hiyo lililoweka ukomo wa Aprili 8, 2026 kwa Taasisi husika kukamilisha usajili wao. ‎ ‎"Ukaguzi huu utahusisha kubaini Taasisi za umma na za binafsi zinazokusanya, kuhifadhi kuchakata na kusafirisha taarifa binafsi nje ya nchi bila kuzingatia matakwa ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44 na kanuni zake na PDPC tutachukua hatua kali za kisheria dhidi ya yeyote, taasisi ama kampuni itakayokiuka sheria hii ikiwa ni pamoja na faini, kifungo, fidia kwa waathirika ama vyote kwa pamoja." Amesema Dkt. Mkilia. ‎ ‎Aidha PDPC imesema ...

TUNATAKA KAZI ZA SERIKALI ZIFANYIKE MAKAO MAKUU YA NCHI-DKT. MWIGULU.* ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  ‎_Asisitiza Taasisi za Serikali zinapaswa kufahamu kwamba makao makuu ya nchi ni Dodoma_ ‎  ‎WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inataka kazi zote zifanyike makao makuu ya nchi ili kusogeza huduma karibu na Wananchi. ‎  ‎Amesema hayo leo Alhamisi (Januari 22, 2026) alipotembelea Ofisi za Wizara ya Maji na Wizara ya Madini zilizopo mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma. ‎  ‎“Ninawapongeza sana, mmehamia Makao Makuu, taasisi zote za Serikali zinapaswa kutambua kwamba makao makuu ya nchi ni Dodoma, na huduma zote zinapaswa kutolewa hapa, hii sio kambi na wala hatutakuwa na Makao Makuu mbili zilizo sambamba”. ‎  ‎Pia, Mheshimiwa Mwigulu ameziagiza Taasisi zote ambazo zimeshakamilisha ujenzi wa majengo katika makao makuu kuyatoa majengo hayo kwa Taasisi ambazo haziwajibiki kuhamia Dodoma lakini bado zimepanga. ‎  ‎“Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwelekeze Katibu Mkuu atengeneze timu ifanye tathmi...

WAZIRI NDEJEMBI AFUNGUA KIKAO CHA 55 CHA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI WA TANESCO DODOMA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  📌 Amshukuru Mhe.Rais Dkt Samia kwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi 📌 Asisitiza usimamizi bora wa masuala ya haki za wafanyakazi na utoaji wa elimu kwa umma na kuboresha utoaji wa huduma za umeme nchini. Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua rasmi Kikao cha 55 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kinachofanyika mkoani Dodoma. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Waziri Ndejembi amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia kwa kuboresha maslahi na stahiki za wafanyakazi wa TANESCO, huku akisisitiza usimamizi madhubuti wa masuala ya haki za wafanyakazi na kuimarisha ushirikiano mahali pa kazi, pamoja na kuendeleza utoaji wa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu huduma ya umeme.  "Natambua mmekutana hapa kujadili kwa kina mambo yanayowahusu wafanyakazi naomba mhakikishe mnazungumza yote na kukubaliana ili kuendelea kuboresha utendaji wa shirika na maslahi ya wa...

ILALA TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA "AMETULETEA MAENDELEO"- MAMBO

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Wananchi wa Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam wameeleza kufurahishwa na kazi kubwa inayotekelezwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa katika Ujenzi wa mundombinu ya barabara za ndani, Vyumba vya madarasa katika shule za msingi na Sekondari pamoja na ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya na maji Wilayani humo. Kwa kuitaja, wananchi hao wameeleza kuhusu ujenzi wa barabara za ndani kupitia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa DMDP, ikiwemo barabara ya Nyeburu- Miti mirefu pamoja na barabara ya Kigezi- Njianne kuelekea Majohe, wakisema awali ilikuwa ni ngumu kuona barabara za ndani zikijengwa kwa kiwango cha lami nchini. Bw. Othman Hassan Mambo, Mkazi wa Nyeburu, ameitaja miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari ikiwemo katika shule za Msingi Nyeburu na Kaliani pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kigezi. "Mama Samia hakuishia hapo kwenye elimu pia ameipandisha hadhi shule ya Sekondari Nyeburu, na sas...

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ILIVYOTAMBA NA HISTORIA YA FARU JOHN NA FARU FAUSTA MBELE YA KAMATI YA BUNGE.

Image
Na Mwandishi wetu, Dodoma. Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) wiki hii ameendelea kuongoza menejimenti ya wizara hiyo mbele ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuelezea kazi,majukumu ,muundo na changamoto za wizara hiyo na taasisi zake. Katika mawasilisho mbalimbali yaliyofanyika mbele ya kamati hiyo kutoka kwa taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiongozwa na Kamishna wa uhifadhi Bw. Abdulrazaq Badru iliwasilisha taarifa yake ikiwa na mafanikio makubwa katika uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii. Katika kikao hicho Ngorongoro iliwakumbusha waheshimiwa wabunge kuhusiana na historia isiyofutika ya faru wakubwa wawili ambao waliishi katika hifadhi hiyo kwa mda mrefu zaidi. Faru hao ni Fausta aliyezaliwa mwaka 1965 na kufa mwaka 2019 na faru John aliyezaliwa mwaka 1978 na kufa mwaka 2016. Ngorongoro imewaweka kwenye historia faru hao ili kuwaonesha watanzania umuhimu wa kuhifadhi faru ambapo idadi yake ndani ya hifa...

WANANCHI WA UKONGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUDUMISHA AMANI NA USALAMA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Wananchi wa Ukonga Mkoani Dar Es Salaam wametoa pongezi na Shukrani kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha amani, utulivu na usalama katika Jimbo lao la Ukonga, suala ambalo limewezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea. Kwaniaba ya wananchi wengine wa Jimbo hilo wakati akizungumza na Chombo chetu cha habari, Bw. Salum Issa Salum, Mkazi wa Kata ya Buyuni ameeleza kuwa licha ya kupitia baadhi ya changamoto mwishoni mwa mwaka jana, hali kwasasa ni shwari na hatua za maendeleo zimeendelea kushuhudiwa katika Kata hiyo na maeneo mengine kote Tanzania. "Nisemee zaidi katika miundombinu, Mama amesikia kilio chetu na sasa barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa DMDP kutoka hapa kwetu kwenda Kivule." Amesema Bw. Salum. Katika maelezo yake, Mwananchi huyo amemuombea uhai zaidi na afya njema Rais Samia, akisisitiza pia umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu ka...

WIZARA YA MALIASILI YAENDELEA KUWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TAASISI ZAKE KWA KAMATI YA BUNGE

Image
📍 Kamati yaipongeza TAWA kwa ubunifu uliopelekea ongezeko la watalii, mapato Na Beatus Maganja, Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mzanva (Mb) imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa ubunifu wake katika sekta ya uhifadhi na utalii, ubunifu uliosababisha ongezeko kubwa la watalii na mapato ya Serikali. Pongezi hizo zimetolewa baada ya Kamati kupokea wasilisho la utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo. Taarifa ya TAWA iliwasilishwa leo Januari 21, 2026 jijini Dodoma na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mlage Yussuf Kabange kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), katika mwendelezo wa Wizara hiyo kuwasilisha taarifa za taasisi zake kwa Kamati ya Bunge. Katika wasilisho hilo, Kamishna Kabange aliieleza Kamati kuwa TAWA inasimamia eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 133,286.36, linalojumuisha Mapori ya Akiba 28, Mapori Tengefu 23, Maeneo ya Malikale 2...