Posts

Showing posts from November, 2025

MZEE WA UPAKO AWATAKA WATANZANIA KUJIFUNZA KUTOKANA NA TUKIO LA OKTOBA 29, "HALIPASWI KURUDIWA TENA"

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’, ametoa wito kwa Watanzania kujifunza kutokana na tukio la Oktoba 29, akisema limeleta maumivu makubwa kwa taifa na halipaswi kurudiwa tena. Amesema tukio hilo limekuwa uzoefu mpya ambao Watanzania hawakuwahi kuupitia, akiwapa pole wakazi wa Dar es Salaam, Arusha, Songwe na Mwanza ambao amesema wameguswa sana na kilichotokea. Amesema hali hiyo imemkumbusha mazingira ya mwaka 1977/1978 wakati wa vita dhidi ya Idd Amin, akieleza kuwa tukio la Oktoba 29 lilikuwa kama “vita ya wenyewe kwa wenyewe.” Pamoja na kueleza kuwa wapo waumini wake waliopigwa risasi maeneo ya Kimara, amesema hakuna Mtanzania ambaye hajaguswa, hivyo si wakati wa kulaumiana bali kila mtu ajihoji kwa nini nchi imefika hatua hiyo huku akionya kuwa kutokujifunza kutokana na kilichotokea kunaweza kusababisha tukio jingine kubwa zaidi baada ya miaka michache ijayo. Mzee wa Upako amesema ni lazima Watanzania, wakiwemo viongozi wa dini, wazazi, viongozi ...

VIJANA TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA KATIKA UJENZI WA TAIFA- CHILONGOLA

Image
Bw. Joseph John Chilongola, Mkazi wa Dar Es Salaam ameeleza kufurahishwa na Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na jitihada mbalimbali anazozichukua katika kuupata muafaka wa Kitaifa, akiwataka wananchi kujiepusha na mikumbo na hamasa za uvunjifu wa amani zinazotolewa Mitandaoni. Chilongola ameeleza namna ambavyo Rais Samia amekuwa akiongozwa na uzalendo kwa nchi yake, suala ambalo limemfanya kuwekeza zaidi katika maendeleo ya watu ikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya barabara tena kwa kiwango cha lami katika mikoa yote nchini. "Mfano ni hapa Msongola, Kata yetu ilikuwa na shida kubwa sana ya barabara lakini sasa kwa asilimia kubwa, barabara hizo zinaelekea kutunufaisha." Amesisitiza Mwananchi huyo. Chilongola ameeleza pia kuhusu namna ambavyo vijana wamekuwa wakitumika katika matukio ya uvunjifu wa amani, akiwasihi kujiepusha na matukio hayo na kushirikiana na serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa Taifa lao. Amesisitiza pia kumtomkatisha tamaa Rais Samia, akitaja...

TUNAUNGA MKONO MCHAKATO WA MARIDHIANO- ZAINAB

Image
Akinamama wajasiriamali wa Mkoa wa Dar Es Salaam wamesisitiza kuhusu umuhimu wa amani katika jamii na ustawi wa familia, wakiwataka Watanzania kuwa wavumilivu na wenye subira katika kushughulikia changamoto za Kijamii na kisiasa walizonazo. Akizungumza na waandishi wa habari kutokana na athari za matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza siku na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Zainabu Juma, amesema mpaka hivi sasa biashara yake imefungwa kutokana na madeni yaliyotokana na siku tano walizoshindwa kufanya biashara, akisema yupo tayari kuunga mkono mchakato wa maridhiano ili kudumisha amani ya Tanzania. "Tunaomba amani ya nchi yetu, Raia wenzetu tuwe na uvumilivu kwani angalieni sisi wa hali ya chini tulivyoathirika na mpaka leo tuna madeni tumefungiwa biashara zetu na hatujui tunalipaje. Ninapenda nchi yetu iwe na amani ili tuishi kwa amani na niseme tu tupo tayari kwa maridhiano maana tunaoumia ni sisi kuanzia ndugu zetu na familia kwa ujumla." Amesema Bi. Zainab ...

TUTUMIE VYEMA FURSA YA KUUNDWA KWA WIZARA YA VIJANA- CHINONGOLO

Image
Kutokana na kuundwa kwa Wizara ya maendeleo ya Vijana nchini chini ya serikali ya awamu ya sita, Vijana wa Kitanzania wametakiwa kuiona kuwa ni fursa muhimu ya kuwajenga kiuchumi na Kijamii, wakitakiwa kuitumia vyema Wizara hiyo katika kushughulikia changamoto na fursa zinazowakabili Watanzania. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Novemba 30, 2025, Bw. Emmanuel Ephraim Chinongolo, Mkazi wa Ilala Dar Es Salaam amemshukuru pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuunda Wizara hiyo pamoja na kumteua Mhe. Joel Nanauka kuwa Waziri wa Wizara hiyo, akisema anaamini kuwa Wizara hiyo italeta matokeo na tija ya haraka kwa Vijana. "Ninaomba sisi Vijana tuione kama ni fursa na tuweze kujitambua kwani tukiwa wenye kujitambua itatusaidia kujua thamani ya Kijana kwenye Taifa hili na tunapaswa kujua ni wakati upi wa kupambania Taifa katika kudai amani na haki kwa njia sahihi na zisizoathiri amani yetu." Amesema Chinongolo. Aidha amesisitiza pia umuhimu wa kuilinda amani n...

REA IMEFANYA KAZI KUBWA YA KUFIKISHA HUDUMA ZA NISHATI VIJIJINI - WAZIRI NDEJEMBI*

Image
*📌Asisitiza ubunifu katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia* *📌Mradi wa vitongozi 9,000 mbioni kuanza* 📍Dodoma Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kufikisha umeme kwenye vijiji na maeneo ya pembezoni mwa miji iliyopelekea kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo. Pongezi hizo zimetolewa leo Novemba 28, 2025 wakati Mhe. Ndejembi alipokutana na kuzungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya REA kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na vitongojini pamoja na utekelezaji wa Mkakati wa nishati safi ya kupikia katika kikao kilichofanyika Ofisi za Makao Makuu ya REA jijini Dodoma.  "REA imefanya kazi kubwa na nzuri sana hapa nchini hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Kipekee nachukua fursa hii kuipongeza sana Bodi ya REA, Menejimenti na Wafanyakazi kwa ujumla kwa kufanya kazi kubwa ya kupeleka umeme katika vijijini vyote nchini, " Amesema Mhe. Ndeje...

MHE. NDEJEMBI AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA KIGAMBONI UMEME WA UHAKIKA

Image
📌Afanya Ziara katika Kituo cha Dege  📌Aelekeza hatua za haraka kuchukuliwa kunusuru hali ya umeme Kigamboni 📌Umeme wa Megawati 22 kupatikana kwa hatua za haraka  📌Upanuzi wa Kituo cha Dege wafikia asilimia 60 Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya Mkoa wa kitanesco wa Kigamboni na kuagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kuhakikisha hali ya umeme katika Mkoa wa Kigamboni inaboreshwa na kuwapa wakazi wa eneo hilo huduma ya uhakika alipotembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza umeme cha Dege tarehe 29 Novemba, 2025. “Leo tumekuja kuona ni namna gani Shirika letu la TANESCO linaweza kutatua changamoto hii kwa haraka zaidi na wameweka mipango mizuri ya muda mrefu katika kuhakikisha wanawezesha kupatikana kwa umeme wa uhakika kwa kujenga na kukiongezea nguvu Kituo cha Dege kwa kuweka transfoma ya MVA 120”, ameeleza Mhe. Ndejembi.  Ili kukabiliana na changamoto ya huduma ya umeme iliyopo kwa haraka, Shirika limekuja na suluhisho l...

HATUTORUHUSU KUTOKEA TENA KWA VURUGU NCHINI- SIMBACHAWENE

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Boniface Simbachawene ametoa wito kwa wananchi na hususani Vijana wa Tanzania kudumisha amani na kuepuka kupanga, kuratibu ama kushiriki kwenye maandamano, akisema kwamba Tanzania bado inakabiliwa na athari kubwa zilizosababishwa na matukio ya Uvunjifu wa amani ya siku ya uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo wa Oktoba 29, 2025. Waziri Simbachawene amesema hayo usiku wa Ijumaa Novemba 28, 2025 katika burudani ya amani iliyofanyika kwenye Soko la Nyama Choma la Kumbilamoto, Kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam akibainisha kuwa maandamano hayo yalisababisha vifo, uharibifu wa mali za serikali na mali binafsi pamoja na kusimama kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi. Simbachawene ameonya kuwa zipo taarifa za mipango ya maandamano mapya yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2025, akisisitiza kuwa Serikali haitaruhusu kutokea kwa vurugu nyingine na kuwaomba wananchi kutotumika na kuchochewa kurudia makosa yali...

Minister Kijaji Reaffirms Tanzania's Commitment to Tourism During Visit to Ngorongoro Conservation Area

Image
 The Minister for Natural Resources and Tourism, Hon. Dr. Ashatu Kijaji (eighth from left), is pictured with international tourists she met at the Ngorongoro Conservation Area entrance (Loduare Gate) during an inspection tour of tourism activities in the area. Dr. Kijaji was accompanied by the Deputy Minister for Natural Resources and Tourism, Hon. Hamad Chande (sixth from left), the Permanent Secretary of the Ministry, Dr. Hassan Abbasi (left), and the Conservation Commissioner for the Ngorongoro Conservation Area, Mr. Abdul-Razaq Badru (right). During the visit, Minister Kijaji assured the tourists that Tanzania remains a peaceful and welcoming destination and continues to implement the directives of the President as well as the CCM government manifesto in serving Tanzanians. Several ministers have already begun implementing the manifesto following the conclusion of the general elections on October 29, 2025.

KILA MMOJA YUPO HURU, HATUINGILIWI NA MAAMUZI YA BUNGE LA ULAYA- SERIKALI

Image
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu azimio lililopitishwa na Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) Novemba 26, 2025, ambalo lilizungumzia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini na kusababisha Kamisheni ya EU kusubirisha kwa muda utiaji saini wa Programu ya Ushirikiano ya Mwaka 2025 (AAP 2025) yenye thamani ya Euro milioni 156. Serikali imesisitiza kuwa madai hayo hayana uthibitisho wa kuaminika na yametokana na taarifa za upande mmoja ambazo hazikupata fursa ya kupingwa au kupewa ufafanuzi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Novemba 27, 2025, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeeleza kuwa Serikali ya Tanzania inaheshimu uhusiano baina yake na EU, ambao ni wa kihistoria, wenye zaidi ya nusu karne, na umejengwa juu ya misingi ya mazungumzo, kuheshimiana na kutokuingiliana katika masuala ya ndani ya kila upande. Imeendelea kueleza kuwa imesikitishwa na hatua ya Bunge la EU kujadili na kupitisha azimio dhidi ya Tanzania bila kuipa Serikali fursa ya k...

RIDHIWANI KIKWETE: NIKO TAYARI KUHOJIWA KUHUSU TUHUMA ZA LAKE OIL

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesema yuko tayari kuitwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kujibu tuhuma zinazomhusisha na umiliki wa vituo vya mafuta vya Lake Oil. Amesema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo Novemba 26, 2025, akibainisha kuwa ni muhimu taarifa za watumishi wa umma kuwa wazi. Alisisitiza kuwa pale panapojitokeza sintofahamu, viongozi wanapaswa kuhojiwa na taarifa kuwekwa hadharani ili wananchi wapate ukweli. “Malalamiko juu ya viongozi yamekuwa mengi sana; haijulikani lipi ni kweli na lipi si kweli,” amesema. Akitoa mfano, Ridhiwani alisema maandamano yaliyotokea hivi karibuni yalihusisha malalamiko kuhusu maadili ya viongozi, ambapo ilidaiwa kuwa vituo vya mafuta vinavyojulikana kama Lake Oil vinamilikiwa naye. “Kuna mtu mmoja anaitwa Ali Edha; ana vituo vya mafuta vinavyoitwa Lake Oil, lakini vimechomwa kwa madai kuwa ni vya Ridhi...

TBN WATOA UFAFANUZI KUHUSU MKUTANO WA IKULU

Image
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) Unatoa Ufafanuzi Kuhusu Mkutano wa Ikulu Dar es Salaam. Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) unapenda kutoa ufafanuzi rasmi na kuweka mambo wazi kufuatia taarifa zisizo sahihi na zinazoleta utata zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano uliofanyika hivi karibuni Ikulu. TBN inakanusha vikali madai yanayosambazwa na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, wakidai—bila uthibitisho wowote—kuwa wanahabari wa maudhui ya mtandaoni waliitwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la "kupewa maelekezo" kuhusu maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika tarehe 9 Desemba. Kusudi Halisi la Mkutano TBN inathibitisha kuwa madai haya si sahihi na yamekuwa yakipotoshwa. Kusudi la kweli na la moja kwa moja la wito wa Ikulu lilikuwa hili: Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Bakari Machumu, alifanya mkutano wa utambulisho rasmi na wadau muhimu wa sekta ya habari, akianza na wanahabari wa maudhui ya mtandaoni. M...

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU BAKARI MACHUMU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WA MTANDAONI

Image
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba, 2025. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kupokea maoni yao, ikiwa ni mfululizo wa mikutano na wadau wa Tasnia ya Habari kwa ajili ya kuboresha masuala mbalimbali ya Mawasiliano baina ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na Vyombo vya Habari, tarehe 27 Novemba, 2025. Viongozi mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja cha Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, Wanablogu mbalimbali pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025. Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali wakizungumza katika Kik...

WANANCHI WAOMBA USAFIRI WA MWENDOKASI KUREJESHWA HARAKA

Image
  Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam wanaoishi kwenye maeneo ambayo Usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu kama Mwendokasi, yalitatizika na matukio ya Uvunjifu wa amani ya Oktoba 29, 2025, wameiomba serikali kurejesha huduma hiyo ya usafiri ili kuondokana na adha kubwa wanayoipitia. Kwa nyakati tofauti leo Alhamisi Novemba 27, 2025 wananchi hao wameeleza adha kubwa wanayoipitia sasa ya kupanda magari zaidi ya mawili katika safari ambazo walikuwa wakitumia basi moja pekee la mwendokasi, huku pia gharama zake zikiwa kubwa na zikiongezeka zaidi kutokana na kuongezeka kwa mahitaji. "Sasa hivi hakuna usafiri wa moja kwa moja, lazima uunganishe magari pamoja na bajaji na bahati mbaya bei imepandishwa, bado pia tunakaa muda mrefu kituoni." Amesema Khalid Mbwana, Mkazi wa Kimara. Aidha wananchi hao pia wanaotumia barabara ya Morogoro, Kimara Mbezi, wameeleza namna ambavyo wanatumia muda mrefu barabarani kutokana na msongamano mkubwa wa magari kwenye b...

WANANCHI WALIA NA FOLENI NA GHARAMA KUBWA ZA USAFIRI, WAOMBA MWENDOKASI KUREJESHWA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam wameeleza athari kubwa za kiuchumi wanazokumbana nazo kwasasa katika baadhi ya maeneo kutokana na kukosekana kwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu kama Mwendokasi, wakiiomba serikali kuharakisha upatikanaji wa huduma ya usafiri huo muhimu. Wananchi hao akiwemo Pius Focus, ameeleza kuwa kwasasa hali ya usafiri imekuwa ya shida kutokana na gharama kubwa za nauli zinazotokana na kupanda magari zaidi ya mawili katika umbali waliokuwa wakisafiri kwa Basi moja la mwendokasi, huku pia msongamano mkubwa wa magari ukiwachelewesha katika shughuli zao za kiuchumi na Kijamii. Wameeleza pia kero yao ya nauli za daladala na Bajaji kupandishwa tofauti na awali kutokana na mahitaji ya Vyombo hivyo vya usafiri kuongezeka, wakisema suala hilo limewafanya kutumia fedha nyingi kwenye kulipia gharama za usafiri. Wananchi hao wametoa wito kwa serikali kuurejesha usafiri huo kwa wakati ili pia kuondoa kero ya msongamano mkubwa wa mag...

MWIGULU AAGIZA MADEREVA WA SERIKALI KUHESHIMU SHERIA ZA BARABARANI

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri Mkuu Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameonesha kukasirishwa na namna ambavyo Magari ya serikali yanaongoza katika kuvunja sheria za usalama barabarani, akiagiza Maafisa wa serikali kufuata sheria hizo ama kutoa mapendekezo ya sheria hizo kubadilishwa. Mhe. Nchemba amebainisha hayo leo Jumatano Novemba 26, 2025 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya kwanza ya wiki ya usafiri endelevu ardhini, Hafla iliyofanyika Jijini Dar Es Salaam, akibainisha tabia ya mwendokasi na kutoheshimu sheria na alama za barabarani kwa madereva wa magari ya serikali. "Mhe. Waziri wa uchukuzi kaeni wadau wote mnaohusika ikiwemo Polisi, kama tunaona Vibao, spidi na sheria nyingine za usalama barabarani zimepitwa na wakati tuzibadilishe kama hazitekelezeki ili tuweke zile tunazotumia." Amesema Dkt. Mwigulu. Waziri Mkuu ametaka kusiwe na sheria za wananchi wa kawaida na kuwa na sheria ama taratibu za serikali barabarani, akihoji ikiwa sheria na taratibu za bara...

MAENDELEO NA USTAWI WETU UNATEGEMEA AMANI NA UTULIVU- PM NCHEMBA

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza umuhimu wa kuendeleza kuimarisha amani nchini na utulivu, akisema maisha na uhai wa Kila Mtanzania unategemea uwepo wa amani na utulivu katika ustawi na maendeleo binafsi na ya Taifa. Mhe. Mwigulu amebainisha hayo leo Jumatano Novemba 26, 2025 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Kwanza ya Wiki ya usafiri endelevu ardhini, Mkutano uliofanyika Jijini Dar Es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu isemayo "Nishati safi na ubunifu katika usafirishaji." "Niwaombe Watanzania, niwaombe Vijana wenzangu tuimarishe amani na utaratibu wetu wa kushughulikia mambo yanayohusu Taifa letu." Amesisitiza Mhe. Waziri Mkuu. Katika maelezo yake, Waziri Mkuu ameeleza kufurahishwa na baadhi ya hotuba za washiriki wa mkutano huo kutoka nje ya nchi, ikiwemo namna ambavyo Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye ujenzi wa miundombinu, ikiwemo rekodi ya kuwa nchi ya kwanza Barani Afrik...

WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA UTAFITI WA KINA WA MADINI HANANG*

Image
*Asimamia kwa vitendo lengo la kuongeza eneo la utafiti kutoka 16% hadi 50% ifikapo 2030* *Manyara yafikia 35.21% ya Makusanyo ya Tsh Bilioni 2.2 kama ilivyopangwa na Serikali* *Ni baada ya hotuba ya Mhe. Rais ya kufungua Bunge la 13* *Waziri Mavunde abainisha faida za utafiti kwa jamii na Taifa kwa ujumla,* 📍 Manyara Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ametembelea na kushuhudia utekelezaji wa utafiti wa kina wa madini kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki (drone) katika eneo la Basotu, Wilaya Hanang, mkoani Manyara. Utafiti huo wa jiofizikia unalenga kubainisha maeneo yenye hifadhi ya madini na kuongeza tija katika usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu. Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge Oktoba 13, 2025 ambapo alitaja utafiti wa madini kama kipaumbele kwa mwaka 2025 - 2030 utakaopelekea kufikia angalau asilimia 50 ya uchunguzi wa kina wa madini nchini ifikapo mwaka ...

WATUMISHI WAPYA WA HALMASHAURI YA LONGIDO WAFUNDWA

Image
NA MWANDISHI WETU, LONGIDO Watumishi wapya wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Kauli hiyo imetolewa leo, Novemba 26, 2025, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Nestory Dagharo, wakati akifungua mafunzo maalumu kwa watumishi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri. Bw. Dagharo amewapongeza watumishi hao kwa kupata fursa ya kuajiriwa katika utumishi wa umma, akibainisha kuwa Serikali imewaamini katika kuwahudumia wananchi. Ametaka kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa uadilifu na kuzingatia misingi ya maadili. “Mafunzo haya ni muhimu sana katika kuwajengea uelewa wa kanuni, taratibu na sheria zinazowaongoza kama watumishi wa umma. Cha msingi ni kuhakikisha kila mtumishi anazingatia maadili wakati wote wa kutekeleza majukumu,” amesema Dagharo. Akifunga mafunzo hayo, Bw. Dagharo amewakumbusha washiriki kuyafanyia kazi mafunzo yote waliyopatiwa, na kuwasisitiza was...

TAWA YAGUSA MAISHA YA WANANCHI MEATU

Image
📍Yajenga Zahanati, Madarasa na Ofisi za walimu  📍Kauli Mbiu ya "Kazi na Utu" Yaanza Kutekelezwa Kwa Vitendo na Kishindo  Na Beatus Maganja, Meatu  Wananchi wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu wanatarajiwa kuondokana na adha ya upatikanaji wa huduma za afya na elimu baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kwa kushirikiana na Kampuni ya Kitalii ya Mwiba Holdings Ltd. kuibua miradi ya ujenzi wa zahanati moja katika Kijiji cha Matale, madarasa manne na ofisi mbili za walimu katika Kijiji cha Mbughayabanyha. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia TAWA na wadau wake katika kutatua changamoto za wananchi na kuhakikisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi zinanufaika moja kwa moja na rasilimali za wanyamapori. Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika miradi hiyo Novemba 25, 2025 iliyofanyika katika vijiji hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe. Fauzia Ngatumbura aliipongeza TAWA Kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd...

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA VITUO VYA POLISI VILIVYOCHOMWA MOTO OKTOBA 29 DAR ES SALAAM

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene, amewasihi wananchi kudumisha amani na kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha usalama wa Taifa unaendelea kuimarika. Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo Novemba 25, 2025 katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya vituo vya Jeshi la Polisi vilivyochomwa moto jijini Dar es Salaam, ikiwemo vya Ubungo, Temboni, Mbezi Juu na Salasala, kufuatia madhara yaliyotokana na vurugu za Oktoba 29, 2025. Waziri amesisitiza kuwa uharibifu wa miundombinu ya vituo hivyo umekwamisha utendaji kazi wa baadhi ya vituo, jambo lililosababisha wananchi kushindwa kupata huduma za kawaida kupitia vituo hivyo. Aidha, Mhe. Simbachawene amewaomba wananchi kuendeleza mshikamano na Polisi, akibainisha kuwa mshikamano huo ndio msingi wa kudumisha amani na usalama wa Taifa. Ameongeza kuwa uharibifu wa mali za Serikali na wananchi si hasara kwa Taifa tu, bali pia ni upotezaji wa rasilimali muhimu zinazotumika kutoa huduma kwa wananchi. Aidha, Waziri ames...

HAYAKUWA MAANDAMANO, ILIKUWA NI HUJUMA ZA KIUCHUMI- DKT. MWIGULU

Image
Na Mwandishi Wetu JAMII HURU  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kuilinda nchi yake, akisisitiza kuwa uharibifu uliofanyika Oktoba 29, 2025 ni zaidi ya maandamano, akiita vurugu hizo kama hujuma za kiuchumi. Waziri Mkuu Mwigulu amebainisha hayo leo Jumanne Novemba 25, 2025 wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam, akieleza kuwa miundombinu iliyoharibiwa si mali ya serikali bali ni miundombinu yenye kutumika na Kila Mtanzania katika kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kote nchini. "Miundombinu hii si mali ya serikali, zahanati si mali ya serikali, barabara pia hivyo hivyo ndiyo maana hata ukinunua shati la mtoto wako mchanga, ipo sehemu unachangia miundombinu hii." Amesisitiza Dkt. Mwigulu. Katika hatua nyingine ametaja sehemu ya uharibifu huo uliotokea Oktoba 29, 2025 kuwa ni pamoja na ofisi za serikali 756, Vituo vya mabasi ya Mwendokasi 27,kituo cha u...