Posts

MARUFUKU KUANDAMANA DISEMBA 09- JESHI LA POLISI

Image
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano yanayohamasishwa katika mitandao ya kijamii kwa kuyaita maandamano ya amani ya Disemba 09, 2025 kutokana na kutofuata taratibu kulingana na sheria ya Polisi pamoja na kujaa viashiria vingi vya uhalifu na uvunjifu wa sheria na taratibu. Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Disemba 05, 2025 kwa Vyombo vya habari na msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, imesema hatua hiyo imefikiwa pia kutokana na mbinu za kihalifu ambazo zimebainika wakihamasishana kuzitumia kuanzia tarehe 09 Disemba, maandamano hayo yamekosa aifa za kisheria kuyaruhusu kuweza kufanyika. "Mtu yeyote anayepanga kufanya maandamano sheria inamtaka kuwasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa maandamano hayo kwa Afisa Polisi msimamizi wa eneo husika akiainisha sehemu yatakayofanyika maandamano hayo, muda, madhumuni na maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi mara kwa mara kwenye gazeti la serikali." Imesema taarifa ya Polisi. Polisi pi...

DCEA YAPEWA TUZO YA UMAHIRI KATIKA UTAYARISHAJI BORA WA TAARIFA ZA HESABU KWA MWAKA 2024 ‎

Image
‎Na Mwandishi Wetu  ‎ ‎Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekuwa mshindi wa kwanza na kupewa tuzo ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2024 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu International Public Sectors Accounting Standards (IPSAS) katika kundi la Taasisi za Serikali zinazojitegemea.  ‎ ‎Tuzo hiyo imetolewa tarehe 04/12/2025 na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA APC hotel Bunju jijini Dar es Salaam. ‎ ‎Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo amekipongeza Kitengo cha fedha na uhasibu kwa kufanikisha uandaaji bora wa hesabu uliopelekea kuwa washindi wa tuzo hiyo. ‎ ‎"Niwashukuru watumishi wote wa Mamlaka hasa timu ya fedha na ukaguzi wa ndani kwa kujitoa, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa taarifa zetu za fedha zinaandaliwa kwa kiwa...

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YATWAA TUZO YA UANDAAJI BORA WA TAARIFA ZA FEDHA

Image
Na Mwandishi wa OMH Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imeibuka Mshindi wa Pili – tuzo za Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha 2024 (Kundi la Idara za Serikali Zinazojitegemea) kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Tuzo hiyo ilikabidhiwa usiku wa Alhamisi, Desemba 4, 2025, jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, ikiwa ni sehemu ya kutambua taasisi zinazozingatia viwango, weledi na uwazi katika uandaaji wa taarifa za fedha za mwaka. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Hassan Mohamed, alisema mafanikio hayo yametokana na uandaaji mzuri wa taarifa za kihesabu kwa kufuata miongozo na kanuni.  Aidha, alisema, hilo lisingewezekana bila kujituma kwa watumishi pamoja na uongozi madhubuti wa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu. Ameeleza kuwa OMH, ikiwemo Kurugenzi ya Fedha na Uhasibu, imeendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi, kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuendelea...

WAZIRI WA NISHATI MHE. NDEJEMBI AZINDUA RASMI MITA JANJA

Image
📌Asema ni mageuzi makubwa ya tekenolojia katika kumuhudumia mteja  📌Aelekeza mita hizo kusambazwa katika maeneo yote yenye uhitaji Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter) yenye lengo la kuboresha na kumrahisishia mteja kufanya manunuzi ya umeme moja kwa moja ikiwa ni mageuzi makubwa ya teknolojia yanayofanywa na TANESCO katika kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wateja. Waziri wa Nishati amezindua Mita janja hizo Disemba 05, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na watendaji wa TANESCO. Amesema Mita hizo mpya zinamwezesha mteja kupata umeme mara moja baada ya kufanya manunuzi ya token bila kutumia kifaa cha ziada cha kuingiza namba (CIU), hatua inayolenga kupunguza changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mfumo wa zamani. “Leo tunajivunia hatua kubwa ya kihistoria zilifanywa na TANESCO ikiwa ni moja ya kampuni za um...

SERIKALI YASISITIZA KUJENGA MAZINGIRA YAFAAYO KWA WAFANYABIASHARA NA WALAJI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA AI-KATAMBI

Image
‎ ‎Na Madina Mohammed  ‎ ‎Serikali imesema kuwa itahakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira wezeshi ya biashara, kupata faida, na kuchangia katika ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa. ‎ ‎Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Patribas Katambi, alipomuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Judith Kapinga, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. ‎ ‎Kauli mbiu ya mwaka huu, “Akili Mnemba (AI) katika Kudumisha Ushindani wa Haki na Kulinda Walaji”, inalingana na dhana ya kimataifa ya Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy, ikisisitiza kuwa teknolojia ya AI ni zana muhimu katika kudumisha ushindani wa haki, kulinda maslahi ya walaji, na kuongeza uwazi katika masoko. ‎ ‎“Serikali imejipanga kuwa daraja, si ukuta, kuhakikisha sera zinazolinda walaji na wafanyabiashara zinatekelezwa ipasavyo, hususan katika matumizi ya TEHAMA na AI,” alisema Mh. Katambai, akiweka mkazo katika uwekaj...

MBETO AWATAKA WAAFRIKA WALIOKO NJE KUTUMIA FURSA NA KUWEKEZA TANZANIA

Image
Na Mwandishi wetu,zanzibar Chama Cha Mapinduzi kimewashauri Watanzania wanaoishi Marekani katika Nchi za Falme za Kiarabu na Ulaya kufuata taratibu za kisheria ili kuwekeza miradi ya kiuchumi na Biashara Zanzibar CCM kimeeleza tayari Serikali zake zimeandaa mazingira wezeshi yanayotoa nafasi kwa Watanzania na wageni wenye mitaji ya kuwekeza katika visiwa vya Pemba na Unguja.  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo alipotembelewa na raia toka Canada na Marekani wenye asili ya Afrika.  Mbeto akizungumza na wageni hao ofisini kwake , alitoa wito kwa Watanzania walioko nje na ambao wameshapata uraia wa nchi nyingine,wajitahidi kuwekeza miradi katika Nchi zao za Asili. Alisema kwa Watanzania waliopata uraia wa Mataifa mengine ,wenye mitaji na mipango ya kufanya biashara , wasione woga badala yake ,waje kuja kuwekeza Zanzibar ambako kuna miundombinu ya uhakika.  "Wa...

WATANZANIA WAFURAHISHWA NA META KUZIFUNGIA AKAUNTI ZA MANGE NA MARIA

Image
Wanaharakati Mange Kimambi na Maria Sarungu Tsehai wenye msururu kadhaa wa lawama, malalamiko na kutajwa kuwa sababu ya uvunjifu wa maadili, amani na umoja wa Watanzania wamefungiwa akaunti zao za Meta, kampuni mama ya Teknolojia yenye kumiliki mitandao ya (Instagram, Facebook na WhatsApp). Mange na Maria wanashutumiwa pia kwa kuchochea matukio ya uvunjifu wa amani, mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa siku za hivi karibuni nchini Tanzania, Yakifanyika wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na za binafsi, Wizi, uchomaji moto na vifo vya watu kadhaa kulikotokana na udhibiti wa tukio hilo na umiliki wa silaha kutoka kwa Vituo vya Polisi vilivyovamiwa na Makundi hayo ya kihalifu. Meta imethibitisha taarifa hizo kwa kuandika " Akaunti hizo zimeondolewa kwa kukiuka sera yetu. Haturuhusu watu kuunda akaunti mpya zinazofanana na zile tulizoziondoa awali kwa kukiuka viwango vya juu vya Taasisi ya Meta." Mange na Maria wanatajwa ...